Slaa kuupeleka mjadala wa Richmond kwa wananchi

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa amesema mjadala wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond, bado haujafungwa na kwamba chama hicho kinajiandaa kupeleka mjadala huo kwa wananchi kwa kuwa Bunge na Serikali haikuwatendea haki wananchi.

Slaa aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu na kauli hiyo, kuungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni mjumbe wa Bazara la wawakilishi, Juma Duni Haji.

Dk Slaa alisema baada ya Bunge kufunga mjadala huo, yeye na wabunge wenzake wa vyama vya upinzani walikubaliana na kitendo hicho na kwamba mjadala huo, haukuwa wa kamati wala Bunge tena kwa sababu kamati ilimaliza kazi yake.

Alisema kuwa suala la Richmond linafanana la suala la akaunti ya madeni ya nje EPA na kwamba chama cha Chadema hakiwezi kukubaliana na hali hiyo zaidi ya kulifikisha suala hilo mikononi mwa wananchi ili waweze kupima na kuamua watakachokifanya kwa serikali na CCM.

"Mimi kama katibu mkuu wa chama nilishakataa suala hili kufungwa toka siku ile ile, hapa ni sisi wenyewe kuchukua hatua zaidi kama vile kulifikisha suala hilo kwa wananchi kwakuwa nikama lile suala la EPA," alisema Dk Slaa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wananchi, CUF Juma Duni Haji akizungumza jana kuhusu kadhia hiyo alisema baadhi ya wabunge wanaoitwa ni wapambanaji wa vita dhidi ya ufisadi hawawezi kuwa wapiganaji wa kweli kwa sababu lengo lao ni sawa na chama chao.

Alisema kitendo cha Bunge kufunga mjadala wa Richmond kinaonyesha kuwa bado wananchi hawana haki ya kutoa mawazo yao na kusikilizwa na kuwataka wananchi kutumia nafasi hiyo kukiondoa chama tawala madarakani.

Duni alisema mjadala wa Richmond umefungwa kimizengwe katika kipindi kizuri kwa kuwa wananchi wanaelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu na hivyo wanapaswa kutumia kura kuinyoosha serikali.

"Huu mjadala wa Richmond umefungwa katika kipindi kizuri kwakuwa wananchi wanaelekea katika uchaguzi mkuu na hivyo wakiondoe madarakani hiki chama,na hawa wabunge wanaopambana na ufisadi lao ni moja na CCM," alisema Duni.

Naye Mbunge wa Bumbuli William Shelukindo alisema kama kuna wanaharakati wanaotaka kuandamana kupingana na kauli ya Bunge hawezi kuwapinga kwakuwa wana haki ya kufanya hivyo.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi kama wabunge waliridhika na mjadala huo kufungwa, alishindwa kutoa jibu na kusema kuwa anaachia vyombo vinavyusika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom