Slaa ,Kitine & Mwakawago

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,332
29,122
Kama una access na TV turn to Channel Ten Now

Mods pls kipindi kikiisha mwaweza kuiclose hii thread
 
Hao Walao Blast Kila Siku Ni Wale Wale Na Wanakuja Na Hoja Zile Zile

aahh ! gotcha ! kwanza hata inaweza isiwe walimblast, hiyo ni katika uandishi si unajua tena lazima upalilie ili ionekane walimshambulia !
Ni wale wale !
 
Na kwa baadhi yetu tusio na access na TV naomba utupe summary.

samahani nililog off nilimpeleka bibie hospital alikuwa anaumwa kidogo....

Makwaia aliwakusanya hawa jamaa waweze kuongelea kuhusu the need of katiba na masuala ya maadili ya viongozi au kwa lugha nzito UFISADI.

aliyeanzisha ni Slaa ambaye alisema kwa uwazi kuhusu utafiti bayana alioufanya ili kuwa na ushahidi kamili juu ya ile list of shame. Kuhusu Katiba alielezea vile vipengele maarufu vinavyompa madaraka yooooooote rais na umuhimu wa kuyapunguza. pia kuhusu contradictions za vipengele vya katiba na utekelezaji wake akitolea mfano wa Ihefu ambapo DC alichukua uamuzi wa kukusanya mapato (kilazima) na mpaka sasa kiasi cha shs Bilion moja hakijulikani kilipozamia.... shughuli za ulazima na ulinzi wa amani ambazo mtendaji wa kata anaziperfom kikatiba but zinaingiliwa na DC ambapo hapo ndipo mgogoro wa kikatiba huanza....

Kuhusu Mkapa... eeer.... oh yes alimtaja huyu baba. Ni ushahidi dhidi ya umiliki wake wa Kiwira mines akiwa pamoja na shemejie Yona na walafi wengineo. Na vile vile mkataba hatari between Kiwira na Tanesco unaotarajiwa sooon (inaonesha wanaweza kuuza hisa ili kukwepa). Pia ktk daftari la usajili wa biashara inaonesha (kwa mujibu wa Slaa) Mkapa aliandikisha plot yetu ya magogoni as business block i mean yeye kama mjasiriamali anaitumia plot 16 pale magogoni as anuani ya biashara.... Akahoji kwa nini hata kodi ya jengo hakulipia????

Kitine aliendeleza misumari kwa kukumbushia zile rabsha zilizomkuta baada ya kutoa maoni makali juu ya rushwa inayojionesha miongoni mwa viongozi wakuu... maneno haya alisema miaka saba iliyopita lakini akaelezea kuwa akawa framed mpaka akatikisika kisiasa baada ya matamshi yake. akaungana na slaa kumzomea mkapa na serikali yake kwa kuwa na ubinafsi na wizi wa mali za umma.

Niliondoka kumpeleka shemeji yenu hspitali kabla mwakawago hajamwaga cheche... waliokuwepo mpaka mwisho wa kipindi tuendeleze mjadala... enhe mwakawago alichangia nin???? Ikumbukwe kuwa leo Makwaia aliacha ule ujinga wake wa kukatishakatisha hoja.. alionekana kama yupo class vile anasikiliza waalim wake....
 
Sio msiokuwa na TV,

Unaelewa ni rahisi kulicheza DRAFT ukiwa nje kuliko ukiwa ndani. Leo hii nimegundua kwamba wengi wetu humu ndani kwenye Forum hatupo bongo ndio maana. Ila cha msingi lazima muelewe ni rahisi sana kutoa kasoro ukiwa nje kama vyama vyetu vya Siasa vinavyofanya na nakubali kwamba vipo right kufanya hivyo kwa maslai ya Taifa.

Lakini swali linakuja? Kama wao kweli wanatujali sisi wananchi na kwa uwezo waliona wa kisiasa na rasilimali, kwanini wasingeanza kuyatatua wao baadhi ya matatizo wanayoyaona kabla hatujawapa madaraka wanakaaa mpk wasubirie madaraka serikalini? Mimi naamini kwamba Chama kama chama tena pinzani kinafaaa kabisa kuonyesha mfano nje ya uwanja kabla hakijaingia kupewa Madaraka ili wananchi tuweze kupata imani hata wakiingia madarakani kuliko kuuza sura kila siku kwenye majukwa na TV.

Mimi ningependa kuona VYAMA VYA UPINZANI SIO WATCH DOGS ILA NI VYAMA VINAVYOJENGA NCHI KWA NGUVU ZAO KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUPITIA UDHAIFU WA CHAMA TAWALA.
 
Mimi naamini kwamba Chama kama chama tena pinzani kinafaaa kabisa kuonyesha mfano nje ya uwanja kabla hakijaingia kupewa Madaraka ili wananchi tuweze kupata imani hata wakiingia madarakani kuliko kuuza sura kila siku kwenye majukwa na TV.

Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani kwenye hili. labda unisaidie mifano ya nini unaona wanaweza kufanya wakati hawapo madarakani na kwa raslimali zipi? maana walioko madarakani wanakodi za wananchi ambazo wanaweza kutumia jee upinzani watumie raslimali zipi? au unaposema wanauwezo unaongelea wa watu binafsi?
 
vijana mnafanya kazi nzuri sana inabidi niingie chimbo kwa ajili ya kuleta nondo za uhakika kwani nilikuwa naogopa ila zitakuja soon
 
Shida ya Mzee wetu Makwaia sehemu kubwa ya kipindi kile anaongea yeye. Kuna maneno anayotaka ayasikie na sio vinginevyo.
 
vijana mnafanya kazi nzuri sana inabidi niingie chimbo kwa ajili ya kuleta nondo za uhakika kwani nilikuwa naogopa ila zitakuja soon

Karibu sana ndugu mfuatiliaji, hizo nondo tuna zisubili kwa hamu kubwa sana ziweze saidia kumkoma nyani kweupe!
 
Sio msiokuwa na TV,

Unaelewa ni rahisi kulicheza DRAFT ukiwa nje kuliko ukiwa ndani. Leo hii nimegundua kwamba wengi wetu humu ndani kwenye Forum hatupo bongo ndio maana. Ila cha msingi lazima muelewe ni rahisi sana kutoa kasoro ukiwa nje kama vyama vyetu vya Siasa vinavyofanya na nakubali kwamba vipo right kufanya hivyo kwa maslai ya Taifa.

Lakini swali linakuja? Kama wao kweli wanatujali sisi wananchi na kwa uwezo waliona wa kisiasa na rasilimali, kwanini wasingeanza kuyatatua wao baadhi ya matatizo wanayoyaona kabla hatujawapa madaraka wanakaaa mpk wasubirie madaraka serikalini? Mimi naamini kwamba Chama kama chama tena pinzani kinafaaa kabisa kuonyesha mfano nje ya uwanja kabla hakijaingia kupewa Madaraka ili wananchi tuweze kupata imani hata wakiingia madarakani kuliko kuuza sura kila siku kwenye majukwa na TV.

Mimi ningependa kuona VYAMA VYA UPINZANI SIO WATCH DOGS ILA NI VYAMA VINAVYOJENGA NCHI KWA NGUVU ZAO KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUPITIA UDHAIFU WA CHAMA TAWALA.

Kunta kwa pesa ipi waliyo nayo ? Maana hata kuendesha ofisin za mikoani ama wilayani hawawezi ruzuku kutokana na wabunge haitoshi .CCM wana mapesa mengi na hawawezi hata kufanya jambo dogo mkuu .
 
samahani nililog off nilimpeleka bibie hospital alikuwa anaumwa kidogo....

Makwaia aliwakusanya hawa jamaa waweze kuongelea kuhusu the need of katiba na masuala ya maadili ya viongozi au kwa lugha nzito UFISADI.

aliyeanzisha ni Slaa ambaye alisema kwa uwazi kuhusu utafiti bayana alioufanya ili kuwa na ushahidi kamili juu ya ile list of shame. Kuhusu Katiba alielezea vile vipengele maarufu vinavyompa madaraka yooooooote rais na umuhimu wa kuyapunguza. pia kuhusu contradictions za vipengele vya katiba na utekelezaji wake akitolea mfano wa Ihefu ambapo DC alichukua uamuzi wa kukusanya mapato (kilazima) na mpaka sasa kiasi cha shs Bilion moja hakijulikani kilipozamia.... shughuli za ulazima na ulinzi wa amani ambazo mtendaji wa kata anaziperfom kikatiba but zinaingiliwa na DC ambapo hapo ndipo mgogoro wa kikatiba huanza....

Kuhusu Mkapa... eeer.... oh yes alimtaja huyu baba. Ni ushahidi dhidi ya umiliki wake wa Kiwira mines akiwa pamoja na shemejie Yona na walafi wengineo. Na vile vile mkataba hatari between Kiwira na Tanesco unaotarajiwa sooon (inaonesha wanaweza kuuza hisa ili kukwepa). Pia ktk daftari la usajili wa biashara inaonesha (kwa mujibu wa Slaa) Mkapa aliandikisha plot yetu ya magogoni as business block i mean yeye kama mjasiriamali anaitumia plot 16 pale magogoni as anuani ya biashara.... Akahoji kwa nini hata kodi ya jengo hakulipia????

Kitine aliendeleza misumari kwa kukumbushia zile rabsha zilizomkuta baada ya kutoa maoni makali juu ya rushwa inayojionesha miongoni mwa viongozi wakuu... maneno haya alisema miaka saba iliyopita lakini akaelezea kuwa akawa framed mpaka akatikisika kisiasa baada ya matamshi yake. akaungana na slaa kumzomea mkapa na serikali yake kwa kuwa na ubinafsi na wizi wa mali za umma.

Niliondoka kumpeleka shemeji yenu hspitali kabla mwakawago hajamwaga cheche... waliokuwepo mpaka mwisho wa kipindi tuendeleze mjadala... enhe mwakawago alichangia nin???? Ikumbukwe kuwa leo Makwaia aliacha ule ujinga wake wa kukatishakatisha hoja.. alionekana kama yupo class vile anasikiliza waalim wake....

Asante sana msanii kwa kutupa habari hii
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani kwenye hili. labda unisaidie mifano ya nini unaona wanaweza kufanya wakati hawapo madarakani na kwa raslimali zipi? maana walioko madarakani wanakodi za wananchi ambazo wanaweza kutumia jee upinzani watumie raslimali zipi? au unaposema wanauwezo unaongelea wa watu binafsi?

Mkubwa nimekupata vizuri sana, Nipo chimbo ila nitaleta hapa sababu mbadala na wala sikumaanisha watu binafsi maana kama chama ni mtu binafsi basi sidhani kama tunaweza kufika.

Kwa uchache na haraka ila naahidi kwamba nitarudi tena, mfano mdogo wenzetu wa Kenya wanakitu inaitwa HARAMBEE nikama FUND RAISING ambapo watu wanachangia kwa ajili ya suala fulani mathalani Tatizo la Maji, Barabara na mengineyo jamaa wanachangishana mpk school fees watu kwenda kusoma wanaweza kutumia vyombo vya habari kwa wananchi.

Jingine vyama vya Siasa vinaweza kuungana kabisa na civil societies kwa ajili ya kutoa elimu ya mazingira na maendeleo ya wananchi kwa ujumla na watu kuweza kujua haki zao za msingi na wajibu wao katika taifa hili.

Jambo jingine ni madaliko mbadala ndani ya vyama kuonyesha ukomavu wa kisiasa (mtu huyo huyo kila siku yeye tuu kwenye uongozi,leteni sura mpya na vichwa vipya vyenyekuweza kuendeleza sera zilizopo na kuongeza mengine kwa ajili ya manufaa ya chama na taifa kwa Ujumla wake) na kuongeza wajumbe(wanachama) ndani ya chama kwa maana dues zinaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine.

Na la mwisho, wenzetu wa Ghana wameshinikiza serikali yao ku draft new law kwajilii ya kuwapa uwezo wa kuwa na access kwa external fund sasa sijui kama sisi tunayo au la na kama hatuna basi ndio tuanze sasa maana ndio itatoa uwanja kwa wafadhili wa kimataifa kusaidia maendeleo ya nchi yetu na sio kubakia kulalama kila kitu kwa KIKWETE hatutafika kimtindo huu.

Nafikiri kwa uchache nitakuwa nimekutosheleza ila nitarudi vizuri zaidi ya hapa.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu vibariki vyama vya Siasa
Mungu ibariki JF.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom