Slaa ,Kitine & Mwakawago

vijana mnafanya kazi nzuri sana inabidi niingie chimbo kwa ajili ya kuleta nondo za uhakika kwani nilikuwa naogopa ila zitakuja soon

Mkuu umeongea habari njema sana, hapa tunapenda nondo ili kuzinoa akili zetu huku tukijipanga kuliokoa Taifa kutoka kwa chama KIBOVU.

Wanabodi nashukuru kwa apreciations zenu, ila pia nakubali sasa kuwa hata wana-CCM wenyewe wameshakichoka chama chao, kama mtakuwa na nafasi mufuatilie marudio ya kipindi kupata picha halisi. Ila kuna kitu kimoja ambacho ningependa wengi wetu tuelewe, ni kwamba CCM imebobea ktk propaganda na kuna chama kimoja (CUF) nacho kinkuja vizuri katika hilo ila wanafanya vizuri hawakurupukii hoja kama ccm wanavyofanya, hivyo hizi harakati za spika kusema kuwa wanafuatilia masuala kadhaa ndani ya serikali, tupime kama hayo ma-ishu ni mwarobaini wa maendeleo au ndio ile kukurupuka kama simba kwenye windo lake? Bunge lilikuwa wapi wakati wananchi wanalalamika kuhusu pesa zao zinazoibiwa? Na kwa nini Bunge liliridhika na majibu ya serikali kuhusu BOT? mpaka Muungwana akaweka tume? na Mnakumbuka Kejeli ya wabunge wa ccm dhidi ya hukumu against Zitto? mnakumbuka nguvu zilizotumika kutetea uozo ule?? Mnakumbuka kebehi dhidi ya hoja za slaa kuhusu BOT pamoja na vitisho?? Kwa akili zangu za kushoto siamini kama hawa jamaa wamekuwa walokole ktk masuala nyeti...... Imefika mahala Bunge haliwezi kupiga kura kuufumua uongozi wa takukuru ingawa sheria waliitunga wao lakini hawana ubavu nao. Kila kukicha mzee wa watu Utoh (CAG) anawapelekea taarifa za mahesabu pamoja na taarifa za uhuni unaofanywa na idara na maofisa wa serikali kubugia bajeti lakini bunge letu kutufu litaunga mkono hoja na kupiga makofi.... Itafika siku wananchi watagoma ohooo maana tumezoea migomo makazini lakini hayo ni maandalizi tu kama hali haitabadilika mioyo wa watu itaingia upofu na mambo yatakuwa mambo.

Ningeamini kuwa UFISADI siyo sera (ya siri) ya CCM endapo ingewatosa mawaziri waliothibitishwa na kamati ya bunge kuwa walishiriki kufisadi na kuuwekea mbolea. Hebu tujiulize hii CCM ya sasa ni chama cha mipasho? maana tawi mojawapo (tanga) linasema wahujumu watoswe lakini tawi jengine (mwanza) wanawakoromea, kama si mipasho ni nini basi?? wanafanya utani na uhai na ustawi wa Taifa? Na kwa nini mtuhumiwa wa ufisadi afanye chereko ya kuachia ngazi?? kwa nin asibehave na kujitulizia mpaka chunguzi ziishe ndipo aje n chereko zake?? Hizi nderemo za mapokezi ya mafisadi majimboni mwao ni matokeo ya kuwanyima elimu wananchi hivyo hawajui dunia yao imelalia upande upi na madhara ya kushabikia uovu... ndio maana wananchi hawataacha kuwachagua mafisadi kutokana na kanga na tsheti zao za bure na kuwaona kwenye video (TV)...

Pia naona ugumu wa vyama-shindani kuchukua hatamu kwa kuwa kuna vyombo kama Usalama wa Taifa ambao hatujui viapo vyao ni kwa serikali au chama chetu? Kuna marekebisho mengi yanapaswa kufanywa ili kuweza kuamini kuwa sasa tupo ktk multipartism au la hapa ni changa la macho. Kwa nchi zinazipiga hatua nzuri kimaendeleo wanaviwajibisha vyombo kama hivi kwa maslahi ya UMMA na si kwa maslahi ya taifa lisiloonekana. uteuzi wa wakuu wa taasisi za kijasusi huthibitishwa na BUNGE ili kujenga dhana ya kuwajibika kwa jamii.Ukiangalia sasa hivi hii Taasisi yetu imekaa kiunoko na sidhani kama iko supportive sna ktk masuala ya kiuchumi (mambo ya kagoda), wasaidie kuingiza nchi ktk ramani ya kiuchumi ili waweze kuongezewa bajeti ya oparesheni zao..... Yanayotokea Zimbabwe ni mwangwi wa mengi yanayotokea ktk nchi zetu za kiafrika sisi tukiwemo. ugumu mwingine ni mapandikizi ya chama chetu ktk vyama shindani, mtawatambua kwa matendo yao maana wengine wakikamilisha kazi wanarudi home kishujaa. Hivi USALAMA wananshindwa kumsaidia Rais kumpatia CV za wasaidizi wake kabla hajawateua?? na iweje viongozi wasiwe na uoga wa kuiibia hazina huku USALAMA wetu upo??
IPO NAMNA
asanteni kwa kunisoma...
IDUMU JF
 
Comments za mbwa msaliti utazijua akisha pewa kanyama na kuachiwa fupa atamuuma hata rafiki yake .

hahaha we Lunyungu unatuvunja mbavu. just let magugu yakue pamoja na ngano kisha kimbembe chake kitajulikana wakati wa mavuno
 
. Hivi USALAMA wananshindwa kumsaidia Rais kumpatia CV za wasaidizi wake kabla hajawateua?? na iweje viongozi wasiwe na uoga wa kuiibia hazina huku USALAMA wetu upo??
IPO NAMNA
asanteni kwa kunisoma...
IDUMU JF

kwa kawaida jukumu la wana usalama ni hilo, lakini katika nchi yetu, makundi mengi yamesahau kazi zao na kila mmoja anakimbilia kwenye siasa, badal ya wanausalama ku-groom viongozi wao wanaji-groom wenyewe! mfano ni akina apson unafikiri ankupeleka cv ya nani badala ya thomas mwangonda yaani mtoto wake?UBINAFSI UNALIPELEKA TAIFA PABAYA, USULTANI UMERUDI KWA KASI YA AJABU
 
kwa kawaida jukumu la wana usalama ni hilo, lakini katika nchi yetu, makundi mengi yamesahau kazi zao na kila mmoja anakimbilia kwenye siasa, badal ya wanausalama ku-groom viongozi wao wanaji-groom wenyewe! mfano ni akina apson unafikiri ankupeleka cv ya nani badala ya thomas mwangonda yaani mtoto wake?UBINAFSI UNALIPELEKA TAIFA PABAYA, USULTANI UMERUDI KWA KASI YA AJABU

Mkuu Mwikimbi...
Najua USALAMA hawapendi jinsi tunavyowadiskass hapa ila kwa kuwa nchi ni yetu na si yao, ni budi wakubali bila mabadiliko tutaendelea kuwanyooshea vidole vya macho mpaka watoe mibanzi na borits.

Serikali (vyombo vyake) itambue kuwa kelele zetu zinatokana na ukweli tunaouona na si udaku tunaousikia (ccm). Hebu fikiria serikali nzima pale bungeni ikaamua kutetea uozo (buzwagi, BOT, nk) halafu ukweli ulipodhihirika wakajiuzulu wawili watatu badala ya KUWAJIBIKA KWA PAMOJA... huu ndiyo uzandiki tunaousema. Sisi hatutaki mishahara na ten parcent zao, tunataka maboresho ktk sekta zooote tukianzia zile muhimu na tunataka uwajibikaji na siyo ubakaji-uchumi.

Najiuliza ajuza kama Kingunge anafanya nin Bungeni kama sio kudhibiti hoja za wabunge wa chama chake???? Najiuliza pia baada ya kuboronga kwa Mungai ktk wizara zooote alizowahi kuwemo je hakuna wa kumvisha jiwe la kusagia shingoni na kumtosa ktk kilindi? Hivi mtu kama Msolla mwenye TUHUMA kulukulu anaangaliwaje? au mpaka wachunguzi wa nje wachome utambi???????

Hii serikali bwana... we acha tu.....!
 
Back
Top Bottom