Slaa: CCM haina ubavu wa kuwabana mafisadi


A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
859
Likes
4
Points
0
A

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
859 4 0
Willibrod-Slaa.jpg

Dr Slaa

Na Richard Makore

27th November 2012

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, akipunga mkono wakati akikaribishwa na viongozi wa chama hicho Jimbo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kufungua mkutano mkuu wa jimbo hilo ikiwa ni moja ya mikakati ya kuimarisha chama hicho.


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Willibrod Slaa amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake hawana ubavu wa kupambana na mafisadi nchini kwa kuwa wao ndiyo waliochangia kuwaweka madarakani.

Kadhalika, viongozi wa CCM na serikali wametakiwa kuacha tabia ya kwenda kwa wananchi na kuwaomba msamaha kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao waliozoahidi mwaka 2005 na 2010 huku wakiwa mikono mitupu badala yake wanatakiwa kwenda kuwaambia wamefanya nini.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho katika Jimbo la Kigamboni.

Alisema Watanzania wataendelea kuona mafisadi wakitanua huku rasilimali za nchi zikiibiwa kwa kuwa serikali ya CCM haina ubavu wa kukemea uchafu huo ingawa inawajua wote kwa majina.

"CCM na serikali yake hawana ubavu wa kupambana na mafisadi kwa sababu hawa hawa ndiyo waliowaingiza madarakani kwa kutumia fedha chafu," aliwaambia wajumbe hao.

Aliwataja baadhi ya majina ya watu (tunayahidahi) aliodai kuwa walitumia fedha chafu zilizotokana na rushwa kuhakikisha CCM inashinda chaguzi za mwaka 2005 na 2010.

Aidha, alisema licha ya CCM kuwaogopa mafisadi, lakini pia imeshindwa kudhibiti wizi na vitendo vya utoroshwaji wa wanyama wakubwa wakiwamo Twiga ndani ya ndege na kwenda kuuzwa nje ya nchi.

"Haya ni maajabu kuona Twiga mkubwa namna ile anakunjwa na kuingizwa kwenye ndege huku serikali ya CCM ikishindwa kuchukua hatua za kukomesha wizi huo," alisema Dk. Slaa akiwa katika ziara yake ya siku nne ya kutembelea majimbo ya Kigamboni, Temeka, Ilala na Kinondoni.

Kuhusu viongozi wa CCM na serikali kwenda kuwaomba msamaha wananchi, Dk. Slaa alisema hayo ni mapungufu makubwa ya utendaji na kwamba wao walitakiwa kwenda kuzungumza na wapiga kura wao wakiwa na kitu mkononi na siyo kuomba wahurumiwe kwa kushindwa kutimiza ahadi walizoahidi kuzitekeleza baada ya kupewa ridhaa ya kuiongoza nchi.

"Kama ni shule kila mwananchi kwa nafasi yake amechangia kuzijenga, sasa wao walizojenga zipo wapi?" alihoji kiongozi huyo na kuongeza kuwa hilo ndilo swali linaloulizwa na Watanzania wengi katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema Chadema kitaendelea kukusanya mapungufu hayo ya CCM na kuyapeleka kwa wananchi ili mwaka 2015 waiweke pembeni kwa kuwa kimeshindwa kutimiza kilichoahidi mwaka 2005 na 2010.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kwa sasa viongozi wa CCM wanafanya mchezo wa kuigiza kutokana na kurudi kuomba msamaha kwa wananchi badala ya kutekeleza ilani kwa vitendo.

"CCM kimekuwa kama popo, hakijulikani kwa sasa kinafanya nini kwa wananchi, na wananchi nao hawakielewi uhalisi wake na hii ni hatari, mustakabali wa taifa letu hususani katika kutafuta maendeleo," alisema Dk. Slaa

Aidha, Dk. Slaa alisema CCM kiache kuhubiri kwamba Tanzania ni nchi ya Ujamaa na Kujitegemea kwa kuwa baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, mashirika yote yameuzwa na kufanya nchi iwe ya kibepari.

"Mkapa (Benjamin) alianza kuuza kila alichoona mbele yake na sasa nchi imejikuta haina shirika ambalo kila Mtanzania anafaidika nalo kama ilivyokuwa wakati wa Mwalimu Nyerere na hii ilitokana na kuvunjwa kwa Azimio la Arusha na kuanzishwa Azimio la Zanzibar," alisema Dk. Slaa.

AWATETEA WAKAZI KIGAMBONI

Akizungumzia hatma ya wananchi wa Kigamboni wanaotarajiwa kuhamishwa kupisha ujenzi wa mji mpya, Dk. Slaa alisema hajawahi kuona nchi isiyojali watu wake kama Tanzania kwa kuwa inawaondoa watu wake ili kuwafurahisha wawekezaji.

"Mimi nimekaa Canada, pale Canada kuna msitu mkubwa wa hifadhi karibia robo ya nchi ile na mtu haruhusiwi kuugusa kwa kuwa wanasema unatunzwa kwa ajili ya vizazi vijavyo miaka elfu tatu, lakini Tanzania hicho hakuna kila kitu kinakwenda kiholela," alisema Dk. Slaa.

Kuhusu uhai wa Chadema, Dk. Slaa aliwataka viongozi wa Chama hicho kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha watu wanakiunga mkono kuanzia ngazi ya chini.

Aliwataka viongozi wa Chadema ambao hawajui wajibu wao kukaa pembeni kwa kuwa hawataweza kukivusha na kuingia Ikulu mwaka 2015.

Aliwakumbusha viongozi na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kigamboni kuendesha chama kwa kuzingatia Katiba yao na badala ya mtu kuibuka kufanya anachoona kinafaa.

CCM YAJITAPA

Wakati Dk. Slaa akisema hayo, CCM kimesema kuwa ziara iliyofanywa na Sekretarieti mpya ya chama hicho katika mikoa ya Rukwa, Mtwara, Geita na Arusha kimepata mafanikio mengi tofauti na walivyotarajia.

"Kwa sasa tunaendelea vizuri na ziara yetu, mafanikio ni mengi, tukimaliza tutawapa ratiba ni mikoa gani tutakwenda," alisema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) wa Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye.

Aidha, Nnauye, amesema kuwa hakuna Waziri yeyote aliyezomewa katika ziara hiyo tofauti na ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Akizungumza na NIPASHE jana, Nnauye alisema katika ziara hiyo viongozi wote wa CCM walipanda jukwaani kujibu kero mbalimbali za wananchi katika mkutano wa kwanza wa viongozi wapya, ukiongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana, na hakuna Waziri yeyote aliyezomewa.

Alisema habari za Mawaziri kuzomewa ni propaganda za vyombo vya habari.

Wiki iliyopita, mawaziri watatu wa CCM, Christopher Chiza wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Hawa Ghasia (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi) na Naibu wake, Aggrey Mwanri, wakiwa mkoani Mtwara wanadaiwa kuzomewa baada ya kupanda jukwaani kujibu kero mbalimbali za wananchi katika mkutano wa kwanza wa viongozi wapya wa CCM taifa, ulioongozwa na Kinana.

CHANZO: NIPASHE
 
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Messages
7,056
Likes
42
Points
145
MNYISANZU

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2011
7,056 42 145
Well said Dr Slaa. CCM ni alien monster wanaotafuna rasilimali zetu bila kumjali mwananchi wa kawaida. 2015 MUST GO TO HELL.
 
Kimagege

Kimagege

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
283
Likes
1
Points
35
Kimagege

Kimagege

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
283 1 35
Hao ccm ni wafu wanaotembea.si muda mrefu wataanguka na hawataamka tena.
 
C

cencer09

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Messages
2,452
Likes
566
Points
280
C

cencer09

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2012
2,452 566 280
Yote karibuni anayozungumza nimeshazowea kuyasikia sasa naona kama wimbo ila kitu ambacho kimekataa kutoka mawazoni wakuu naomba muwe makini kulifikiria simchezo hata kidogo!
HEBU NIAMBIENI TWIGA NA UKUBWA NA UREFU WAKE AMEINGIAJE KWENYE NDEGE?,kudadadeki hata wengine hapa jf hatujapanda ndege,ccm bwana nanino zao
 
B

Baba Hellen

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2012
Messages
764
Likes
2
Points
33
B

Baba Hellen

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2012
764 2 33
Mafisadi wote hata sura zao zime baadilika kutika katika misingi ya utu
 
B

Baba Hellen

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2012
Messages
764
Likes
2
Points
33
B

Baba Hellen

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2012
764 2 33
Mizizi yake ni rushwa paa lake uonevu kuta zake unafiki hatuki pendi ccm
 
B

Baba Hellen

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2012
Messages
764
Likes
2
Points
33
B

Baba Hellen

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2012
764 2 33
Wakifa wote mi sawa tu ccm hawa mafisadi
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,936
Likes
382
Points
180
Age
85
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,936 382 180
By TUNTEMEKE
UZURI WA KIKAO CHA LEO PALE MWEMBE YANGA NILIKUWEPO TENA MEZA KUU
BABU ANAFANYA ZIARA YA KUTENGENEZA MTANDAO WA KE WA KICHAMA
BABU ANATENGENEZA UONGOZI WAKE(CHAIN OF COMMAND YAKE)

ANAPANDIKIZA UONGOZI USIO TAKIWA NDANI YA CHAMA,MGOGORO UNAOFUKUTA TEMEKE NADHANI IPO SIKU BABU ATARUDI KWA MCHUMBA WAKE AKIWA HOI
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,936
Likes
382
Points
180
Age
85
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,936 382 180
Leo waziwazi anamlazimisha mzee urio(huyu ni mzee aliyejenga jengo la ofisi za chama pale temeke-mwembe yanga) anamlazimisha aondoke kwenye chama kisa ameshazeeka

swali:::dar slaa wewe si upo kwenye koma???very sad nimeona leo alivyokongoroka afya yake,sijajua mchezo gani josephine anaufanya kwa babu.
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,936
Likes
382
Points
180
Age
85
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,936 382 180
ZIARA YAKE HIYO TUTASIKIA MENGI HASA IKIFIKIA KULE MAENEO YA KAWE KWNEYE JIMBO LA HALIMA MDEE AMBAYE YUPO KWENYE UGOMVI MKALI SANA BAADA YA BABU KUNYIMWA PENZI NA HALIMA
BABU AMEUNDA ZENGWE AKISAIDIANA NA JANET YULE DIWANI WA KAWE ILI WAPANDIKIZE MAJUNGU NA FITINA KWA HALIMA ASIKUBALIKE NDANI YA CHAMA
I MEAN ANACHOKIFANYA BABU NI KUBOMOA CHADEMA NA KUJENGA CHADEMA YAKE BINAFSI

HALI HIYO YA HALIMA MDEE KUHALIBIWA JIMBONI KWAKE ILIJIDHIHIRISHA PALE BI.JOSEPHINE ALIPOWAANDAMANISHA WANAWAKE HADI MAKAO MAKUU YA KATIBU MKUU KWA MADAI KWAMBA HAWAMTAKI HALIMA MDEE(Nadhani Dr.slaa analo jibu,Tumain makene unalifahamu hatakama utakataa hapa)
SWALI HALIMA MDEE NA UJASIRI WAKE WOTE ULE WA KUKITETEA CHAMA LEO DR.SLAA ANAMUUNDIA ZENGWE AFUKUZWE????? ETI MWAKA 2015 BI.JOSEPHINE AGOMBEE KAWE
 
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
7,936
Likes
382
Points
180
Age
85
T2015CCM

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
7,936 382 180
Aliyekuwa diwani wa Chadema, Rehema Mohammed ambaye amehamia CCM, akibubujikwa machozi jukwaani wakati akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano huo.amelalamikia kunyanyaswa kijinsia na viongozi wa chadema akiwemo lema na dr slaa

6.-Aliyekuwa-diwani-wa-Chadema-Rehema-Mohammed-ambaye-amehamia-CCM-akibubujikwa-machozi-jukwaani-wakati-akitangaza-kuhamia-CCM-wakati-wa-mkutano-huo.jpg
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
234
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 234 160
Aliyekuwa diwani wa Chadema, Rehema Mohammed ambaye amehamia CCM, akibubujikwa machozi jukwaani wakati akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano huo.amelalamikia kunyanyaswa kijinsia na viongozi wa chadema akiwemo lema na dr slaa

6.-Aliyekuwa-diwani-wa-Chadema-Rehema-Mohammed-ambaye-amehamia-CCM-akibubujikwa-machozi-jukwaani-wakati-akitangaza-kuhamia-CCM-wakati-wa-mkutano-huo.jpg
Naona umegeuka vuvuzela la Tuntemeke. Au ni one and the same?
 
B

blueray

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Messages
2,219
Likes
6
Points
0
B

blueray

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2012
2,219 6 0
ZIARA YAKE HIYO TUTASIKIA MENGI HASA IKIFIKIA KULE MAENEO YA KAWE KWNEYE JIMBO LA HALIMA MDEE AMBAYE YUPO KWENYE UGOMVI MKALI SANA BAADA YA BABU KUNYIMWA PENZI NA HALIMA
BABU AMEUNDA ZENGWE AKISAIDIANA NA JANET YULE DIWANI WA KAWE ILI WAPANDIKIZE MAJUNGU NA FITINA KWA HALIMA ASIKUBALIKE NDANI YA CHAMA
I MEAN ANACHOKIFANYA BABU NI KUBOMOA CHADEMA NA KUJENGA CHADEMA YAKE BINAFSI

HALI HIYO YA HALIMA MDEE KUHALIBIWA JIMBONI KWAKE ILIJIDHIHIRISHA PALE BI.JOSEPHINE ALIPOWAANDAMANISHA WANAWAKE HADI MAKAO MAKUU YA KATIBU MKUU KWA MADAI KWAMBA HAWAMTAKI HALIMA MDEE(Nadhani Dr.slaa analo jibu,Tumain makene unalifahamu hatakama utakataa hapa)
SWALI HALIMA MDEE NA UJASIRI WAKE WOTE ULE WA KUKITETEA CHAMA LEO DR.SLAA ANAMUUNDIA ZENGWE AFUKUZWE????? ETI MWAKA 2015 BI.JOSEPHINE AGOMBEE KAWE
Majungu na uongo mtupu!

CCM kweli mmekwisha, mnachokijua ni kutunga uongo, Majungu, rushwa Na Ufisadi!

Shame on you!
 
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
3,577
Likes
15
Points
135
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
3,577 15 135
Aliyekuwa diwani wa Chadema, Rehema Mohammed ambaye amehamia CCM, akibubujikwa machozi jukwaani wakati akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano huo.amelalamikia kunyanyaswa kijinsia na viongozi wa chadema akiwemo lema na dr slaa

6.-Aliyekuwa-diwani-wa-Chadema-Rehema-Mohammed-ambaye-amehamia-CCM-akibubujikwa-machozi-jukwaani-wakati-akitangaza-kuhamia-CCM-wakati-wa-mkutano-huo.jpg
laani inamsumbua huyu mama
 
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
3,577
Likes
15
Points
135
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
3,577 15 135
ukikosa akili ndio matatizo haya, akili ndogo kuongoza akili kubwa ndio kulikotufikisha hapa
 
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,410
Likes
22
Points
0
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,410 22 0
Ni kweli haina ubavu kuwabana mafisadi na ushahidi elfu kumi upo!
 
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,410
Likes
22
Points
0
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,410 22 0
Ni kweli haina ubavu kuwabana mafisadi na ushahidi elfu kumi upo!
YES! Chadema inaweza kuwabana mafisadi - example ni Dr Slaa na Mwembe Yanga 2007, mafisadi walisambaratika na wengine kutinga mahakamani.
 
mchuziwanyoka

mchuziwanyoka

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Messages
374
Likes
0
Points
33
mchuziwanyoka

mchuziwanyoka

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2011
374 0 33
nikweli amesema lakini muulize amelipia kadi ya ccm mpaka 2015 wakati ya chadomo ajalipa mkumbushe baba colin slaa
 

Forum statistics

Threads 1,237,915
Members 475,774
Posts 29,306,068