Slaa azuiliwa kuhutubia Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa azuiliwa kuhutubia Iringa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by We can, Oct 28, 2010.

 1. W

  We can JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tetesi kutoka Iringa zinasema Slaa kazuiliwa kuhutubia Iringa kwa vile amechelewa kufika. Taarifa za uhakika zinaonyesha kuwa alicheleweshwa maksudi Dodoma ili azima hiyo itimie. Sasa hivi anaomba idhini ya kufanya mkutano kesho-sijui ataruhusiwa au la. Umati uliokuwa huko hauelezeki.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  duh,kazi kweli kweli mwaka huu!na slaa tena?
   
 3. M

  Mutu JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mhhhhhhhhhhhhhh haya unaweza mpiga teke chura ukamwongezea mwendo badala ya kumkomoa
   
 4. A

  Abraham Lincon Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe juu ya hilo. Mara nyingi tunafanya vitu kwa lengo la kumkomoa mtu lakini matokeo huwa tofauti. Tukumbuke, hakuna haki bila wajibu, twende tukapige kura hapo tarehe 31. Mungu ibariki Tanzania.
   
 5. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu kama ushabiki huu umezidi! ninavyokumbuka mimi haikuwa hivyo. jamaa kweli alichelewa mbaka saa kumi na mbili alikuwa bado hajafika, mishale ya saa kumi na mbili ndo helkopta yake ilionekana angani lakini watu tiyari walikuwa wameishatawanyika pia ingekuwa vigumu yeye kuhutubia kulingana na sheria za uchaguzi zinazoagiza kuwa kampeni iwe mwisho saa kumi na mbili. lakini hata hivyo hakikualibika kitu kwani wagombea na viongozi wa chadema waliendelea na kampeni zao kama kawaida huku wakipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa mashabiki waliofurika kumsubili silaa. watu wanasubiri labda kesho kama atahutubia
   
 6. W

  We can JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bw. Mnyikungu, soma link yote vizuri. Nadhani hujaelewa. Umepinga kile unachojipinga mwenyewe. Soma ulichonukuu, na ulichosema. Usipandwe jazba...hali halisi ndo hiyo. Huwezi kuchakachua mawazo ya watu.
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Hadi nimepaliwa kwa kucheka? ni kweli kumpiga chura teke nikumwongezea mwendo sio kumkomoa!!!! mwaka huu!!!!
   
 8. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  we can,na wewe sio muelewa, ninachotaka kusema ni kwaba slaa hajazuiliwa ila alichelewa mno, pia hakutua uwanjani kama kawaida yake, watu walimsubiri mbaka wakatawanyika,wakiwa tiyari wametawanyika ndio waliiona helkopta ikipita angani ikielekea wasikokujua. Sasa sijua kazuiliwa saa ngapi na nani?.
   
Loading...