Slaa awaambia wafanyakazi, Nazitaka kura zenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa awaambia wafanyakazi, Nazitaka kura zenu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BAK, Aug 5, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Slaa awaambia wafanyakazi, Nazitaka kura zenu


  [​IMG]Thursday, 05 August 2010 06:36
  Baptist Mapunda,Songea na
  Charles Mwakipesile, Mbeya


  MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilbrod Slaa amewaomba wafanyakazi nchini kumpa kura zao katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu ili ashughulikie kikamilifu matatizo yao.

  Dkt. Slaa alisema wafanyakazi nchini wana kila sababu kumpa kura zao kwani Rais Jakaya Kikwete alizikataa hadharani wakati akipinga hatua yao kutaka kugoma wakidai nyongeza za mishahara mapema mwaka huu.

  Akihutubia maelfu ya wakazi wa miji ya Songea na Mbeya kwa nyakati tofauti jana, katika ziara yake inayoendelea ya kuomba udhamini wa fomu za urais, Dkt. Slaa, alisema inasikitisha serikali kushindwa kutatua kero za wafanyakazi na badala yake kutumia vitisho katika suala hilo.
  Alisema kitendo cha Rais Kikwete kukataa kura hizo hadharani kimewadhalilisha wafanyakazi na kusisitiza kuwa anahitaji kura hizo ambazo ni zaidi ya milioni tano tofauti na takwimu zilizotolewa za wafanyakazi 350,000 bila kuzingatia kwamba katika idadi hiyo, wafanyakazi hao wana ndugu na jamaa wanaowategemea.

  "Rais Kikwete alitamka hadharani, akawaambia wafanyakazi kwamba hata msiponipa kura zenu Oktoba nitapata kwa wengine. Sisi CHADEMA tunasema kura hizo tunazihitaji sana ili zituwezeshe kusaidia nchi iondokane na lindi la umaskini. Labda mwenzetu ana njia zingine kupata kura lakini sisi tunazitaka hizo," alisema Dkt. Slaa.

  Alisema inasikitisha wafanyakazi wanapodai haki zao za msingi, badala ya serikali kushughulikia kero zao inaibuka na kuwatisha.
  "Wafanyakazi waliambiwa wakiandamana watapambana na dola. Sasa kama baba wa familia ameshindwa kushughulikia matatizo ya watoto wanaodai haki zao, anawatisha, tupate baba mwingine anayejali watoto wake," alisema Dkt. Slaa.

  Aliwataka Watanzania kuamua kufanya mabadiliko kwenye uchaguzi wa Oktoba kwa kuiondoa CCM madarakani ambayo tangu uhuru imeshindwa kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli badala yake, wanazidi kuwa masikini siku hadi siku.

  "Watu waamke wakubali mabadiliko, watadanganywa hadi lini? Tangu uhuru hakuna maendeleo ya kweli, CCM haiwezi kufanya lolote jipya sasa, kuendelea kuichagua ni kuchagua umasikini achaneni nayo," alisema Dkt. Slaa.

  Alisema Watanzania wameichoka CCM na hawana mapenzi ya kweli, badala yake wanatumia bendera zake kinafiki kwenye maeneo ya biashara kuficha kasoro zilizopo.

  Akielezea kuteuliwa kwake kugombea nafasi hiyo, Dkt. Slaa, alisema awali alisita lakini alikubali kutokana na uchungu alio nao kwa Watanzania wenzake na namna wanavyoteseka kwa umasikini huku nchi ikiwa na utajiri mkubwa unaoliwa na wachache.

  Aliahidi kuendeleza mapambano ya ufisadi kwa nguvu zote hadi uovu huo utakapotokomezwa nchini.
  Alisema akiwa bungeni hakuwaogopa wabunge kwa kuwa ni wenzake alifichua jinsi wanavyopata mshahara mnono wa sh. milioni saba kwa mwezi huku wakilipiwa mafuta lita moja kwa sh. 2500.

  Alisema ndio maana wafanyakazi wengi nchini wanalipwa mishahara midogo kutokana na wabunge kulipwa mamilioni ya fedha ambayo yeye na wenzake wa CHADEMA walipinga jambo hilo.
   
 2. m

  masasi Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  slaa ni silaha ya sumu kwa ccm na serikali yake,vijijini wameonyesha mwamko wa kisiasa kwa kuwabwaga viongozi wenye porojo na usanii,tuamke watanzania na tufanye mabadiliko ya kweli taifa linaangamia,slaa ni mtu makini apewe kila aina ya support huku tukiweka kando itikadi zetu
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Nashauri CHADEMA waandae vitu vingine vingi vya msingi vinavyotueleza watafanya nini tofauti na monster CCM. Waviweke kwenye lugha itakayoeleweka kwa mtanzania wa kawaida. Pia CHADEMA, pre-empty njama zote CCM watakazotumia si tunawajua hawa jamani.

  Dr. Slaa go...go....
   
Loading...