Slaa atoa jibu: Kikwete ndio anamlinda Mwema

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
HOJA nzito zinazoendelea kuibuliwa na viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu utendaji wa Rais Jakaya Kikwete, zinaonekana kuwa mwiba na kuikoroga serikali yake. Wakati hoja ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ya uteuzi wa baadhi ya majaji wasio na sifa ikiwa bado haijapatiwa majibu ya kuridhisha, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, naye amepigilia msumari mwingine akisema Rais Kikwete anamlinda Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema.

Dk. Slaa aliibua hoja hiyo wakati akizungumzia mauaji mbalimbali yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya raia wema, akisema hali hiyo ni matokeo ya IGP Mwema, kulindwa na mkuu wake, na hivyo kushindwa kuwachukulia hatua wahusika.Wakati hoja hizo zikiibuliwa, wasaidizi waandamizi wa Rais Kikwete wakiwemo mawaziri na watendaji wengine, wameonekana kupwaya, wakishindwa kuhimili mikiki ya kutoa majibu yenye kufafanua kile kinachohojiwa.

Akizungumza jana jijiji Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano mkuu wa chama hicho Jimbo la Kinondoni, Dk. Slaa alisema kama IGP Mwema anashindwa kuchukua hatua juu ya matatizo yanayojitokeza, ikiwamo mauaji na kujeruhi wanayofanyiwa wananchi na polisi, rais anapaswa kuchukua hatua kwa lengo la kuiokoa nchi.

Huku akirejea matukio kadhaa ya mauaji na mateso mbalimbali yaliyofanyika katika mikoa ya Tabora, Morogoro, Iringa, Arusha, Mara, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam na maeneo mengine, Dk. Slaa alisema sheria zipo wazi juu ya suala hilo katika kuunda tume ya kimahakama katika kupata ukweli wa madhila hayo. "Nyote mnajua kuwa haki katika nchi yetu imekuwa bidhaa adimu, matukio ya kutisha yanajitokeza kila siku, viongozi wenye dhamana na maisha yetu wanakaa kimya, katika hili kama rais hajui sheria si ana watu wanaomsaidia, hivi haoni hata haja ya kuunda tume huru ya kimahakama?" alihoji.

Alisema kuwa kutokana na ukimya wa rais, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwachukulia hatua Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP Mwema, makamanda wa polisi wa mikoa ya Iringa na Morogoro, CHADEMA watakutana kabla ya Krismasi na kutoa msimamo wa nini kifanyike kutetea haki ya wananchi. Dk. Slaa alisema madhumuni ya CHADEMA ni kukuza, kulinda na kutetea haki za binadamu, hivyo wanapaswa kuhakikisha wanafuatilia ukandamizaji wa watu katika misingi ya rangi jinsia, ukanda, rika na itikadi, jambo alilodai limewashinda CCM. "CCM leo kila wanaposimama wanaomba waendelee kuungwa mkono ili watawale…wameacha yale yaliyo katika katiba ya nchi na kusahau maandiko yaliyo nyuma ya ilani ya chama," alisema.

Chikawe amgwaya Lissu

Wakati Dk. Slaa akiibua tuhuma nzito kwa Serikali ya Rais Kikwete, zenye kuhitaji majibu stahili, Waziri wake wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, ameshindwa kutolea ufafanuzi hoja zilizoibuliwa na Lissu kuhusu baadhi ya majaji, aliodai waliteuliwa bila kufuata utaratibu. Chikawe ambaye kimsingi ni miongoni mwa wasaidizi wa Rais Kikwete, anayepaswa kuitetea serikali yake, alipoulizwa juu ya hoja hiyo aliishia kusema, "hoja za Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba, Tundu Lissu nimezisikia, nimezisoma na sina maoni yoyote juu ya hilo." Akizungumza na Tanzania Daima jana, Waziri Chikawe alisema: "Ungekuja ofisini, nipo safari kwa sasa, hata hivyo hoja za Lissu nimeziona, nimezisoma na sina ‘comment' kwa sasa."

Ni waziri huyo huyo, ambaye aliliambia Bunge kuwa Tume ya Mahakama inamshauri rais wakati wote na kwamba hakuna ukiukwaji wowote uliofanyika katika uteuzi wa majaji. Alisema haijatokea hata siku moja rais akamteua jaji wa Mahakama Kuu bila kuzingatia mapendekezo ya Tume ya Uajiri ya Mahakama. Awali akijibu hoja za Lissu bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, ambaye jana simu yake iliita bila majibu, alimuonya Lissu kuwa ataburuzwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge kwa ‘taarifa potofu anazoziwasilisha bungeni'.

Lakini mapema wiki hii, Lissu alirejea hoja yake na kusisitiza kuwa alishatoa maelezo hayo hata katika Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi. "Nilieleza jinsi rais alivyofanya uteuzi wa baadhi ya majaji pasipokupata ushauri wa Tume ya Utumishi wa Mahakama. Wamekuwa wakijibu kiujumla, mimi niliwataja kwa majina yao na hata hili nilieleza katika Kamati ya Ngwilizi ambayo taarifa yake haikuwekwa hadharani pasipo sababu za kueleweka," alisema.

Alipotafutwa jana, Lissu ambaye pia ni mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni, alisema kuwa kwa sasa serikali haiwezi kusema chochote zaidi ya kukubali, kwani tayari ameshawapa ushahidi kwenye Kamati ya Bunge. Alisema hoja yake kuwa kuna ukiukwaji wa katiba inaungwa mkono na nyaraka za ndani ya serikali na hasa Ofisi ya Rais, Ikulu yenyewe, ambayo Desemba 6, 2007, mkutano kuhusu ajira ya majaji waliostaafu ulifanyika Ikulu chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Kiongozi wakati huo, Philemon Luhanjo.

Lissu aliongeza kuwa, wajumbe wengine walikuwa pamoja na Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika na Naibu wake, Sazi Salula, Katibu Mkuu Utumishi George Yambesi, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Sophia Wambura na Susan Mlawi wa Sekretarieti ya Baraza la Mawazi.

"Serikali iseme suala hili ni la kweli au si la kweli, na wale niliowataja kuwa hawana sifa kwa mfano ya elimu serikali iseme wamesoma wapi, na kwanini kulikuwa na kikosi kazi kwa ajili ya majaji wanaoajiriwa kwa mkataba ikiwa mimi sijasema kweli," alisema.
Alisema kuwa anazidi kuuliza inawezekanaje jaji asome shahada ya kwanza ya Sheria Chuo Kikuu Huria sasa, kwamba aliteuliwaje kuwa jaji, maana hiyo ndio sifa ya msingi?
 
b2.jpg


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo Jumatano Oktoba 31, 2012. Katika salamu zake, Mbowe alimsifia rais Kikwete ambayue pia ni Mwenyekiti wa CCM, Kwa kutimiza ahadi yake

@&@&@&@&@&@&@&@&@&@&@&@&@

Nakumbuka ngoma ya Lizombe maarufu kule mkoani Ruvuma enzi hizo sijui kama wangali wanaimba hivyo hadi leo;
"Nikiwepo mwenyewe machoni hamnisemi, nikionoka kidogo nyuma mwanisengenya."
Hawa viongozi wa Chadema wakutanapo na Kikwete ni kuchekacheka kama yeye na kumsifia oh umejenga barabara nchi nzima kama kamanda Mbowe alivyomsifia hivi karibuni jimboni kwake Hai na sifa nyingi za kumvimbisha kichwa, lakini matatizo mengine kama hayo katu hawathubutu kuyaibua mbele yake.

Sijawahi kumsikia kiongozi ye yote wa Chadema baada ya kukutana ana kwa ana na Kikwete aliyewahi kumwuliza kulikoni mauaji haya, na mengineyo.
 
ila kweli, kwa matukio ya polisi yanayoendelea nchini ni rahisi kuamini.!
 
This story is overrated!! .... anamlinda kivipi? Na sifa za mtu kuwa jaji ni zipi?
 
Siyo tu kwamba Kikwete anamlinda Mwema, anamtumia pia. Ukitafakari ile hotuba aliyoitoa kwenye mkutano kuhusu kutumiwa polisi kubeba CCM ni wazi kwamba Kikwete ndiye aliyeamrisha kusimamishwa kwa mkutano wa Chadema Arusha, hatua iliyopelekea kuuawa watu watatu na polisi wanatumika kudhibiti mikutano ya Chadema kutokana na amri ya Kikwete. It is that simple.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Birds of the same feather flock together!
Hata ukiwa mwadilifu kwa kiwango gani ukishaingia kwenye hii serikali you will dance on the same tune!
 
Kikwete hawezi kumwajibisha IGP Mwema kwa sababu ya undugu ambapo inasemekana ni mtu na shemeji yake kabisa...,...Hivyo ili nchi irudi kwenye misingi yake kunahitajika chama kingine tofauti na CCM Kiongoze dora.
 
Kikwete hawezi kumwajibisha IGP Mwema kwa sababu ya undugu ambapo inasemekana ni mtu na shemeji yake kabisa...,...Hivyo ili nchi irudi kwenye misingi yake kunahitajika chama kingine tofauti na CCM Kiongoze dora.

Domy kipi sasa maana naona kwa sasa kila chama kina undugunaizeshen,ccm nako wanabebana na chadema pia wanapakatana,,,,,
 
Last edited by a moderator:
Candid Scope,

Una uhakika na unachosema? Wanapokutana kuna mengi sana wanayaoongea huwa off record. Wakati mwingine, (na inategemea na namna ya mikutano hiyo) huwa siyo mahali muafaka kuongea hayo. Lakini ukweli ni kwamba kwa yale yanayokera baada ya muda mrefu wa ukimya wa JK, basi hapo ndipo akina Slaa huyaweka hadharani.

JK ni mtu anayependa sana eti matatizo yaishe kimya kimya tu na kuna siku tabia hii itakuja kumcost sana.
 
kwa hiyo mkuu unataka kama wamekutana kwa jambo la barabara wazungumzie mauaji ya raia? Kweli nyie ndo mnaoifanya siasa uadui. Unataka kwa mfano wakikutana kwenye mazishi waanze kuzungumzia mauaji ya raia? Kila jambo lina pahali pake!

Kwa haraka haraka, nilikosa jibu. Asante umetoa majibu mazuri
 

Una uhakika na unachosema? Wanapokutana kuna mengi sana wanayaoongea huwa off record. Wakati mwingine, (na inategemea na namna ya mikutano hiyo) huwa siyo mahali muafaka kuongea hayo. Lakini ukweli ni kwamba kwa yale yanayokera baada ya muda mrefu wa ukimya wa JK, basi hapo ndipo akina Slaa huyaweka hadharani.

JK ni mtu anayependa sana eti matatizo yaishe kimya kimya tu na kuna siku tabia hii itakuja kumcost sana.

Kwenye red:

Usemayo ni kweli mkuu. Katika ule mkutan wa Ikulu kati JK na viongozi wa CDM wakati wa mjadala wa kuunda sheria ya mchakato wa katiba mpya hapo ndipo viongozi wa CDM walipofyatuka mbele ya rais -- hasa kuhusu polisi kukamatakamata viongozi wa CDM na kuwaonea haya wale wa CCM zinapotokea vurugu katika mikutano ya vyama hivyo.
 
Dr Slaa amenena ukweli. JK anamlinda sana Mwema kutokana na ushemeji. Wasipowajibishana sasa tutawawajibisha 2015.
 
This story is overrated!! .... anamlinda kivipi? Na sifa za mtu kuwa jaji ni zipi?

mbona sifa za JAJI zimeelezwa sana hapa,ulikuwa wapi? kwa kukusaidia ni kwamba ili uwe JAJI inatakiwa angalau uwe na CERTIFICATE ya sheria.
 
Back
Top Bottom