Slaa aongelea kilichomtoa Kabourou

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa, amezungumza na KLH News leo na kuzungumzia kwa kina kilichomtoa Kaborou Chadema na hali ya kisiasa na kimaisha ya Tanzania! kwa uwazi anasema juu ya majaribio ya CCM kuwarubuni wanachama wa Chadema kujiunga na chama hicho tawala!! Mazungumzo yatarushwa Ijumaa.

Usikose!
 
Nitumie namba yako kwenye PM na nitakuwa tayari kusikiliza maoni yako... na kukuhoji... mahojiano si kwa watu maarufu tu
 
Mzee Mwanakijiji said:
Nitumie namba yako kwenye PM na nitakuwa tayari kusikiliza maoni yako... na kukuhoji... mahojiano si kwa watu maarufu tu

Shukrani.Nitakutumia namba.
 
Samahani wazee niliwaahidi kuwaletea mahojiano na Dr. Slaa lakini kutokana na kupatikana kwa hotuba ya Mhe Rais kikwete basi ninawaletea hotuba hiyo leo Ijumaa na Jumatatu nitawaletea mahojiano yangu na Mhe. Dr. Wilbroad Slaa, Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Karatu.
 
Tunaomba hapa tutumie neno Ndugu JK na ndugu Slaa badala ya Uheshimiwa ama tutumie Mr.JK ama Mr.Slaa .Mnaonaje tukiachana na mawazo ya uheshimiwa ?
 
Mugishagwe... kuna Protocol za kimataifa... watu hao wamechaguliwa na Watanzania na kuitwa waheshimiwa ni haki ya yao.. sio kupendelewa au tusi... Hata kama hatukubaliani nao, kuna protokali nyingine haziumizi!! Nafikiri kumuita mtu "Bwana" ndio baya zaidi!!! na kumuita mtu Mr. so and so... ni kasumba!!
 
Inaelekea jamvi hili lina magwanda wengi sana....

Hebu nambieni tuone: wenzenu magamba wanawakumbuka sana waasisi wao
hata kama kuna mabaya waliyafanya hapa na pale. Wanakuza mazuri ya waasisi wao.

Walid Aman Kaburu atakumbukwa kwa lipi CDM? Na Mary Kabigi?
 
wafuasi wengi wa chadema wameingia chama hicho mwaka 2010 kwa ushawishi wa maaskofu walid kaburu watamjua wapi?
 
Muasi hakumbukwi na zaidi stahili yake huwa nikunyongwa hasa kwakipindi akihasi wakati wa vuguvugu la mapinduzi utakiwa hata kaburi yake isionekane!!
 
fisadi hilo,hao watu ni wale ambao hawatakiwi kwenye jamii kwani hawana msimamo na wako ki maslahi yaidi.alipewa vijhela mbuzi na sisiemu akaasi na kujiunga nao katika kuliangamiza taifa.hana lolote wala hatuhitaji kumuweka kwenye kumbukumbu zetu.
 
He....

Nyakageni...mara hii ushasahau kwamba Kaburu ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuweka jina la CDM bungeni? Na kwamba kabla ya hapo hii CDM yako ilikuwa tu kama TPP Maendeleo. He, we vipi!

Ukumbuke pia alikuwa mtu wa kwanza kwa huku bara kufanya vyama vya upinzani vieleweke vinaweza kuingia bungeni. Mi nafikiri nyie magwanda mnalazimika kumuenzi Kaburu kwa sana tu... Hivi ukitengana na mke ndo hata mazuri yake unataka yafutwe kwenye ramani ya ukoo?



mchumia tumbo wa nini? Traitor
 
hana cha kukumbukwa msaliti huyo. aliyokuwa analalamikia alipokuwa cdm kwani yamesharekebishwa mbona anarudi tena kwenye magamba
 
wewe unataka Waldi Aman Kabouru akumbukwe kwa ajili ya kuwasaliti wana Kigoma@? Heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo wake, Kabouru ni kinyonga alisababisha watu kufa kwa ajili yake,lakini yeye alipohongwa tu, na wana Magamba sifa yake ilifutika mra moja.haipo sababu ya kumkumbuka,kinyonga huyo.
 
wewe unataka Waldi Aman Kabouru akumbukwe kwa ajili ya kuwasaliti wana Kigoma@? Heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo wake, Kabouru ni kinyonga alisababisha watu kufa kwa ajili yake,lakini yeye alipohongwa tu, na wana Magamba sifa yake ilifutika mra moja.haipo sababu ya kumkumbuka,kinyonga huyo.

Kaborou ni msaliti na hata huko Magamba amekaa sio kwa itikadi ya chama bali kwa kununuliwa na Makamba na kupewa ubunge wa Afrika Mashariki kwa kupitia kuhonga wabunge kutumia fedha za mafisadi papa. Makamba hayupo tuone kama zile fedha za kuhonga zitapatikana na kumpitisha safari hii!!Aliwalisha pilau ya maji machafu ya Lake Tanganyika watu wa Kigoma wakampa ubunge akaja kuwasaliti kwa vipande thelathini vya fedha. Hafai kabisa kukumbukwa anafaa kunyongwa.
 
Dr.Walid Aman Walid (Kabourou) ndio mtanzania wa kwanza kuwa mbunge wa kwanza kuchaguliwa kutoka Chadema na kambi ya Upinzani kwa ujumla mwaka 1994 baada ya uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha mbunge wa kigoma mjini Marehem Rajab Mbano,ndie mtanzania wa kwanza kukaa kwenye bench la upinzani bungen akiwa mbungee pekee toka kambi ya upinzani
 
Kaburou hana lolote la kukumbukwa, harafu watu wanasema cdm ilianzishwa na wachaga! Mkt mtei, mmkt ngwilulupi, kabigi nk
 
Akumbukwe kisa alikuwa mbunge wa kwanza kutoka upinzani? acheni ujinga na pia mwache ande zake, hakumbukwi ng'o.
 
Back
Top Bottom