BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,116
Slaa ang'ang'ania nyaraka za siri
Basil Msongo
Daily News; Sunday,June 29, 2008 @00:01
Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa (Chadema) yupo tayari kufungwa miaka 20 jela na anaamini kuwa serikali ikificha nyaraka kwa lengo la kuficha maovu ni dhambi kwa Mungu na si haki kwa Watanzania. Ijumaa jioni Dk Slaa alitangaza bungeni kuwa ana nyaraka za serikali na yupo tayari kukamatwa.
Mbunge huyo aliwaonyesha wabunge nyaraka alizonazo na akasema Sheria inayozuia watu kutokuwa na nyaraka hizo haihalalishi wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, mikataba mibovu, na maovu mengine yanayodaiwa kuwapo serikalini. Dk alilieleza Bunge kuwa anaifahamu sheria hiyo lakini anazitafuta nyaraka hizo ili kutetea maslahi ya Watanzania.
Aliyasema hayo wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya matumizi kupitia vifungu kwa vifungu bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na taasisi zilizo chini ya Mamlaka hizo kwa mwaka wa fedha 2008/2009. Dk Slaa alilieleza Bunge kuwa anazipata nyaraka hizo kwa Watanzania wenye dhamira safi kwa nchi yao na kwamba usiri wa serikali unaliumiza taifa hivyo hatakaa kimya.
Alieleza Bunge kuwa anazo nyaraka hizo na atakapotakiwa kuzitoa atazitoa kwa viongozi wa Serikali akiwamo Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Dk Slaa alisema kitendo cha yeye kuweza kuzipata nyaraka hizo zikiwamo kutoka Benki Kuu Tanzania (BOT) ni uthibitisho wa kuanguka kwa mfumo wa Serikali na akaiuliza Serikali, ni nyaraka zipi anazoweza kuzisoma bungeni na zipi zisizoruhusiwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Sera na Uratibu, Philip Marmo, alimjibu kwa kusema kuwa, hakuna kanuni ya Bunge inayoweka mipaka ya nyaraka hizo hivyo inahitajika busara ya Spika wa Bunge kuhusu suala hilo kwa kuzingatia mila na desturi ya mabunge mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa Marmo kanuni haziko wazi lakini Dk Slaa anafahamu kuwa anavunja sheria kwa kuwa anaifahamu sheria inayomzuia kuwa na nyaraka za serikali. Waziri Marmo alitoa mfano kuwa, Dk Slaa ana nyaraka za kikao cha bodi ya wakurugenzi wa BOT cha Juni 6 mwaka huu na sehemu ya muhuri imekatwa ili kuficha ushahidi.
Alisema nyaraka hiyo ya BOT imeandikwa ' Mp tafadhali nimeondoa muhuri kwa usalama wa maofisa wetu." "Kwa hiyo mheshimiwa Spika Mheshimiwa Slaa hahitaji kufundishwa maana ya siri…….mheshimiwa Slaa hahitaji kufundishwa nini nyaraka za Serikali au la" alisema Marmo na kusema kuwa kuwa nyaraka kama hiyo ni kosa la jinai.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Matumizi ya Bunge iliyopitia vifungu vya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Anne Makinda, alisema nyaraka za Serikali zinaaweza kupatikana kwa utaratibu halali na kwamba, hali ya sasa ya nyaraka hizo kupatika ovyo ni uthibitisho kuwa ndani ya Serikali kuna tatizo. "Nchi yoyote heshima yake ni siri zake zinazotolewa ndani ya utaratibu husika" alisema Makinda.
Alhamisi wiki hii Bunge lilitangaza kuwa wabunge wakikamatwa mitaani kwa kuwa na nyaraka za Serikali watashitakiwa kama wananchi wengine kwa kuwa ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kuwa na nyaraka hizo. Naibu Spika wa Bunge Anna Makinda alitoa msimamo huo baada ya Waziri Marmo kuomba muongozo wa Spika baada ya wabunge kusema wana nyaraka za Serikali.
"Ukikutwa na kitu cha namna hiyo mitaani ni shauri yako wewe" alisema Naibu Spika bungeni wakati wabunge wakichangia hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2008/2009. Marmo alisema kuwa na nyaraka za Serikali ni kosa la jinai, na kwamba anayepatikana na hatia hiyo anaweza kufungwa miaka 20 jela.
"Na duniani kote nyaraka hizi hazijadiliwi bungeni katika mijadala ya wazi"alisema Marmo na kuhoji itakuwaje kama wabunge hao wakikutwa nazo mitaani. Marmo aliuliza kama wabunge wanazipata nyaraka hizo bungeni au zinawafikia kimiujiza na akataka Spika aeleze itakuwaje kama vyombo vya dola vikiwachukulia sheria.
Waziri huyo aliuliza hivyo baada ya Mbunge wa Viti Maalum (CUF) Mkiwa Kimwanga kutangaza bungeni kuwa ana nyaraka aliyoiandika Katibu Mkuu Ofisi ya Rais kwenda kwa mwekezaji akimuagiza jambo linaliowahusu wafanyakazi wa kiwanda.
Marmo alisema kitendo cha wabunge kutangaza kuwa wana nyaraka za serikali ni makosa ya wazi ya jinai na wakikutwa nazo mitaani pia ni kosa na wanaweza kufungwa jela.
Makinda alisema kwa kuwa wabunge hao hawakuziweka mezani, na walizisoma bila ruhusa ya Spika, Bunge halizitambui kwa kuwa hazikuwa rasmi na kwamba, hata wabunge wanapotaka kusoma hotuba za mawaziri inabidi waweke mezani na wapate ruhusa ya Spika wa Bunge. Naibu Spika wa Bunge, alisema, endapo Mbunge anataka kusoma kitu chochote wakati akizungumza bungeni anapaswa kuweka maandishi hayo mezani na aombe ruhusa ya Spika ndipo asome.