Slaa Anasa Waraka Mzito! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa Anasa Waraka Mzito!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, Sep 23, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ni ule wa kuimaliza CHADEMA!

  na Janet Josiah na Charles Ndagula, Moshi


  MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametangaza kunasa waraka wa siri ulioandikwa siku nne zilizopita, ambao pamoja na mambo mengine unawaagiza watendaji wakuu wa serikali kufanya kila wawezalo kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashinda uchaguzi.

  Dk. Slaa mwanasiasa mwenye rekodi ya kunasa taarifa mbalimbali nyeti za serikali, alitangaza kuhusu kuuona waraka huo wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika Manispaa ya Moshi.

  Akizungumzia suala hilo, Dk. Slaa alimtahadharisha mgombea wa urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha anachukua hatua ya kuvidhibiti vyombo vyake vya usalama ili visimwage damu isiyo na hatia kwa sababu tu ya kutaka kushinda urais kwa gharama zozote zile.

  Dk. Slaa aliyekuwa akihutubia katika Uwanja wa Mashujaa mjini hapa, alisema dalili zimeanza kujitokeza katika mikoa mbalimbali aliyopita, ambako kumekuwapo na matukio ya watu kuonewa na viongozi wa serikali.

  Akifafanua, alisema waraka huo unaokwenda kwa vyombo vya usalama, wakiwemo wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, unawataka wafanye lolote ili kuhakikisha CCM inashinda.

  “Ninao waraka ulioandikwa Septemba 19 (Jumapili iliyopita), mwaka huu na leo ni siku ya tatu, unakamilishwa na kusambazwa kwa viongozi hao kuwakumbusha kuwa lazima wahakikishe CCM inashinda, sikuupata hapa hapa, ila tayari umesambazwa nchi nzima,” alisema Dk. Slaa.

  Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho, kwa nafasi yake anatoa tamko hilo ili kumtahadharisha Rais Kikwete kuacha mara moja hujuma hiyo, na kuwa dalili zinaonyesha kwamba Watanzania wameamka na wanahitaji mabadiliko.

  Alisema pamoja na kupata hujuma hizo, chama chake kimejipanga vyema kukabiliana na mashambulizi ya CCM na serikali yake, kwa kuweka mfumo imara wa ulinzi kwa viongozi wao na wapiga kura wao.

  Alivitaka vyombo vya usalama kuacha kuhujumu msafara wake pamoja na watendaji wake, ambao wanatangulia katika vituo ambavyo anafanyia mikutano ya kampeni, kwa kuwa leo serikali ni ya CCM na kesho serikali itakuwa ya CHADEMA.

  Dk. Slaa alitoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa za polisi kutaka kuwakamata vijana wa chama hicho, ambao wanapima viwanja vya kufanyia mikutano yao, ambavyo helikopta itaweza kutua kwa urahisi (GPS).

  Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa vijana hao, Gwakisa Gwakisa, alikiri kutaka kukamatwa na polisi hao na kudai kuwa alipowaona alifungua mlango wa gari na kukimbia pamoja na wenzake wachache na kuacha gari la chama hicho, ambalo lilichukuliwa na polisi.

  Hata hivyo, Tanzania Daima ilipomuuliza Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, alikiri kuwa wanalishikilia gari la CHADEMA na kwamba wanamsaka mpima ramani ili wamkamate.

  “Bado tunamtafuta mpima ramani wa chama hicho ili baadaye tutoe taarifa kwenu nyinyi waandishi wa habari,” alisema RPC Ng’hoboko.

  Akizungumzia tukio hilo, Dk. Slaa amewataka polisi kuwaacha Watanzania wanaotimiza mapenzi yao bila kuwabughudhi na kwamba kero hizo mwisho ni Oktoba 31.

  Akiwahutubia wananchi hao mara baada ya kutoa tamko la chama chake, Dk. Slaa aliwaomba wawachague wagombea wa chama chao ili waweze kufufua viwanda ambavyo vimekufa kutokana na sera mbovu za CCM.

  “Ndugu zangu wana Moshi, ichagueni CHADEMA kwa kuwa CCM imeshindwa kuwaletea maendeleo, kwa kushindwa kufufua viwanda vyenu kama vile kiwanda cha ngozi, magunia, vyuma na viwanda vingine,” alisema Dk. Slaa.

  Mapema akimnadi mgombea huyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, aliwataka Watanzania kuufanya mwaka huu kuwa wa maamuzi na si wa utani, kwa kuwachagua wagombea makini wa chama hicho.

  “Mwaka 2010 hatudanganyiki ndugu zangu wa Moshi…kwa kuwa tutaingia Ikulu na watu makini kama Dk. Slaa, kwa kuwa na nyie ni makini, hivyo mtatuchagua.

  “Kwa kuwa CCM ilitumia woga wenu Watanzania kuwatawala na kuwanyanyasa, lakini sasa Watanzania mmeondokana na woga…lakini imani kubwa ipo kwenu wana Moshi, kwa kuwa mmechangia mafanikio ya wana CHADEMA,” alisema Mbowe.

  Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano makubwa yaliyoanzia katika ofisi za wilaya za chama hicho zilizopo katika Kata ya Majengo na kupita katika barabara za Ghala na Mawenzi, maarufu kama Double Road, Florida hadi katika viwanja vya Mashujaa, huku waandamanaji wakisindikizwa na helikopta iliyokuwa ikiyahamasisha kwa saa nzima.


  Source: Tanzania Daima.
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Haya bwana,

  Hawa jamaa mwaka huu watasababisha matatizo makubwa. Waache watu wapige kura kwa amani wasije kutuletea masahibu kama yale ya Kenya 2007.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ikulu patamu ndugu yangu, acha mchezo!

  [​IMG]
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata pangekuwa patamu namna gani, watu wanatakiwa kujua kuwa pale ni makao ya muda. Hata Nyerere aliondoka. Shida ninayoanza kuipata kuona dalili za Wakwere kutaka kujifanya permanent tenants, ukizinagati kuwa hata sifa za kupita kwa hiyo milango ya Jumba takatifu hawana.
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Si mchezo Muulizeni Anne Kilango alifanya shopping akijua atakuwa First Lady!
   
 6. s

  sheka leonard Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama wanasambaza waraka wanataka kumwaga damu isiyo na hatia Mungu ibaariki TZ. Mungu mbariki Dr SLAA
   
 7. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  CCM waacheni watanzania waamue nani awe rais wao na mbuge wao na si kutumia mabavu. Kutumia mabavu maana yake ni kuwa mnataka vyeo si kwa kuwatumikia watanzania bali kwa faida zenu wenyewe huku wananchi wakiendelea kuogelea kwenye dimbwi la umaskini katika nchi iliyojaa maziwa na asali (utajiri wa kila namna).
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mungu awe nasi katika kutuvusha salama kati ya hawa mbwa mwitu kuelekea nchi ya asali na maziwa. Naam, nchi ya ahadi
   
 9. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  tuna hamu kweli na huo waraka.....nadhani utawapa wananchi nini cha kufanya baada ya SISIEMU kuiba kura zetu
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Sep 23, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Itabidi Dkt Slaa atupatie waraka huo mapema!
   
 11. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Huko nilishapita, na katika Thread yangu kama wiki mbili zilizopita niliandika kuwa huko anaungwa mkono na 65% ya wakati wa Moshi, hii ni kutokana na takwimu nilizofanyia utafiti. Halikadhalika huko Mara, lakini kivumbio n i mi9koa iliyobaki na vijijini.

  Hata kwa helkopta hawezio kubadili Picha.

  Chagua maendeleo, sio mapenzi ya moyo.
   
 12. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Naanza kuona nchi ipo katika, wasiwasi...naam na sasa Mkuu wa Majeshi anatangaza 'HALI YA HATARI' umeme unakatika ghafla nchi nzima, wanawake wanakimbia na watoto...wanaume wakiwa baa wanalaani kukatika kwa umeme na mara ghafla magari ya polisi yanatenda nchi nzima na sasa Taifa halina amani. Barabarani kuna maiti kadhaa za vijana waliokuwa wakiandamana kudai uhuru wa uchaguzi.....
  ahaa, kumbe ni ndoto nilikuwa nikiota.
   
 13. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  CCM wanajua kuwa wamo ktk big trouble ndio maana wanataka kutumia mabavu in all cost! Mungu Bariki Tanzania na watu wake!na uwadidimize majinunu ccm!!
   
 14. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  plz ndoto hii isitokee....hope Jk ataondoka kwa amani
  akifanya ivyo atakumbukwa milele kama kambarage
   
 15. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Ikulu si kichaka cha walanguzi, wahuni. kama unataka kufanya uhuni, nenda kafanye mabarabara yako telee!
  Ukipewa kazi ya kuongoza nchi lazima ujiheshimu,
  Mtu anayekimbilia Ikulu, na anatumia vijicenti kuhonga, huyo hatufai na wakuogopa kama ukoma,
  Ikulu ni mahala patakatifu,
  kila nisikiapo maneno haya, natamani Baba wa Taifa arudi aje kujionea mwenyewe jinsi Ikulu ilivyogeuzwa kuwa pango la Walanguzi,
   
 16. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hey there,

  Uuuwiii,

  ndo nimeweka kwenye ile post yangu nyingine kuwa tumwambie Bwana Luis Ocampo wa mahakama wa The Hague, na hizo nyaraka tupeleke nakala kama ushahidi ili Mkwere akamatwe kama Charles Tailor au atafutwe kama Omar El Bashir
   
 17. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Duh! Propaganda za Chadema. No way, anyway
   
 18. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kuwa Mkwere siyo tatizo hata kidogo, tunachohitaji sisi watanzania ni kuwa na viongozi waadilifu, wanaoguswa na umasikini wa watanzania, wenye uchungu na Taifa lao na si kuweka viongozi vibaraka wanaopola mali zetu na kuzikimbizia ktk mataifa yaliyoendelea.ukweli kwa namna hii hatutofika kwa mwendo huu wa konokono
   
Loading...