Slaa amtaka Shimbo kueleza zilikokwenda sh bil 155 za Meremeta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa amtaka Shimbo kueleza zilikokwenda sh bil 155 za Meremeta

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 4, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mgombea urais kupitia Chama cha Maendeleo na Demokrasia, Dk wilbrod Slaa amerusha kombora kwa mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, kumtaka awaeleze Watanzania zilikoenda Sh Bilioni 155, zilizopotea katika mradi wa kampuni ya kuchimba dhahabu ya Meremeta ambao unadaiwa ni mali ya jeshi hilo.

  Alisema hatoogopa vitisho na yuko tayari hata kuuawa kwa kupigwa risasi ili mradi haki itendeke na kumtaka Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo, kuwaeleza Watanzania zilikoenda sh bil. 155, zilizopotea katika mradi wa kampuni ya kuchimba dhahabu ya Meremeta.

  Dk. Slaa alimtaka jenerali huyo wa jeshi kuwatendea haki Watanzania kwa kueleza ukweli namna fedha hizo zilizogunduliwa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zilivyotumika, waliohusika na wizi huo na hatua zilizochukuliwa dhidi yao.

  Alibainisha kuwa CAG, alitoa taarifa ya wizi huo bungeni na wala si maneno ya kuokoteza mtaani au yake (Slaa) ambapo sh bil. 155 zilipotea baada ya kuibiwa katika mgodi wa dhahabu wa Buhemba.

  "Nampa changamoto Jenerali Shimbo aeleze zimeenda wapi…wizi ni wizi tu hata kama umetokea jeshini, Watanzania ambao ndio walipa kodi wanayo haki ya kujua fedha hizo zilikoenda na hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika," alisema.

  Mgombea huyo alisema siyo kweli kuwa kutoa taarifa ya upotevu huo ni kuingilia siri za jeshi kwani Watanzania hawataki kujua masuala yanayohusu medani za kivita kama vile idadi na aina ya vifaru, mizinga, bunduki, mabomu wala ndege za kijeshi na uwezo wa JWTZ.

  Alibainisha wanachotaka kujua ni wahusika walivyofanikiwa kuchota mabilioni hayo ambayo mpaka hivi sasa serikali imekuwa ikiupotosha umma juu ya matumizi yake kwa madai ni siri ya jeshi.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa, amewataka wakazi wa wilaya ya Kyela kutumia demokrasia kumchagua mgombea urais, ubunge na udiwani wanayemtaka.

  Alisema iwapo wakazi hao wanataka kumpa ubunge mgombea wa CCM, Dk. Harrison Mwakyembe, yeye (Slaa) hana tatizo ili mradi kura za urais wampe kama wanavyomuaidi.

  Alisema iwapo Dk. Mwakyembe atachaguliwa ni vyema wakamweleza kuwa mambo ya CCM yaishie nje na siyo bungeni kwa kuwa serikali yake itakuwa na wabunge wengi wa upinzani.

  "Kama mtamchagua Dk. Mwakyembe na mimi nikawa Rais wake tutafanya kazi vizuri sana kwa kuwa wote tunapingana na mafisadi," alisema Dk. Slaa.

  Chanzo: Tanzania Daima
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sensible argument!...Wajeshi ukiwagusa hapo wanalalama kwamba unaongelea siri za jeshi!...OMG, jeshi si ni la wananchi?...au ni la chama tawala?
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  MEREMETA: The inside story
  THE involvement of the Tanzania People's Defence Forces (TPDF) in the controversial Meremeta Limited formally ceased in 2005/06 after the joint venture company between the government and South African investors was officially dissolved, impeccable sources have revealed to THISDAY.

  Insiders familiar with the whole saga say that, contrary to Prime Minister Mizengo Pinda's claims in the National Assembly last week that the now-defunct company was a classified military project, the army was never involved in subsequent deals involving TANGOLD and Deep Green Finance.

  According to these sources, Meremeta Ltd was initially registered in the Isle of Man, United Kingdom in April 1997, and received certificate of registration number 3424504.

  Going by official government records, Meremeta was registered as a 50-50 joint venture project between the Tanzanian government and Triennex (PTY) Limited of South Africa.

  However, other strong evidence indicates the presence in Meremeta's affairs from the outset of at least two British legal firms, London Law Services Ltd and London Law Secretarial Ltd, both described as 'nominal shareholders.'

  In October 1997, the company was given certificate of compliance number 32755 by the Business Registration Licensing Authority (BRELA), allowing it to formally operate in Tanzania.

  Working in collaboration with the TPDF at the Buhemba open pit gold mine in Mara Region, Meremeta officially began gold mining operations in February 2003, with its operations being heavily financed by Tanzanian taxpayers through the Bank of Tanzania (BoT).

  In 2005, the Meremeta company announced it had produced 2,075 kilogrammes of gold at a cash cost of $384 per troy ounce of gold.

  Apart from the Buhemba gold mine, Meremeta also held the Kilamongo and Mwizi deposits, both located south of Buhemba, and the Nyasanero deposit.

  But then in 2006 – only a year after officially beginning gold production the company declared bankruptcy, and was formally dissolved.

  ''With the dissolution of Meremeta, both the TPDF and the South African company (Triennex) formally pulled out of gold mining activities at Buhemba,'' said one of our well-informed sources, adding: ''So officially, any military involvement in the Meremeta project ended in 2006 when the company was declared bankrupt.''

  Insiders further say the initial involvement of the TPDF in the Buhemba gold mining operations was aimed at raising funds to finance its cash-strapped vehicle manufacturing division – Tanzania Automotive Technology Centre, better known as the Nyumbu project.

  It is understood that Meremeta was also set up to assist in developing the country's informal gold mining sector.

  Official government records show that as Meremeta Ltd was winding up its operations, the BoT paid more than $118m (approx. 150bn/-) to Nedcor Trade Services Limited after having guaranteed a loan from the South African firm to Meremeta.

  The BoT raised the funds to pay off the loan to Meremeta through a controversial 155bn/- Treasury bond, in a transaction that raised serious queries from auditors.

  Following the liquidation of Meremeta Ltd, the Ministry of Energy and Minerals announced in Parliament that a wholly-owned government company, TANGOLD Limited, had been formed and assumed all Meremeta company assets, including the Buhemba gold mine.

  Investigations by THISDAY have already established that the BoT paid another $13.34m (approx. 17bn/-) to TANGOLD through an account at the National Bank of Commerce Limited's Corporate Branch in Dar es Salaam.

  TANGOLD was initially registered as an offshore company in Mauritius in April 2005, with its address listed as Suite 520, Barkly Whart, Le Caudan Waterfront, Port Louis.

  In February 2006, the company was registered in Tanzania, with its local shareholders including former BoT governor Daudi Ballali (now deceased); the then Minister for Infrastructure Development, Andrew Chenge; and the Permanent Secretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja.

  Other TANGOLD shareholders are the current PS in the Ministry of Water and Irrigation, Patrick Rutabanzibwa; and the then permanent secretary in the Ministry of Livestock Development, Vincent Mrisho.

  Although the Ministry of Energy and Minerals claimed that TANGOLD was 100% owned by the government, it has failed to explain why the company was registered in Mauritius and not Tanzania, and why its articles of association give the listed shareholders permission to transfer all or part of their shares to their next of kin.

  TANGOLD is also not listed at the Treasury Registry among companies partly or wholly-owned by the government, and has thus not been subjected to statutory auditing by the Controller and Auditor General (CAG).

  When addressing the National Assembly in Dodoma last Friday, premier Pinda appeared evasive to the point of fumbling in his attempts to answer queries from opposition members of parliament regarding Meremeta, TANGOLD and Deep Green Finance Limited.

  His reference to the controversial Meremeta question as a ''military affair and therefore one of national security'' in particular only served to raise more questions rather than provide any answers to the mystery.

  Source: ThisDay
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Jamani tusiliingilie Jeshi katika kazi zake, hata kama mkuu wa majeshi na rafiki zake wakigawana pesa za walipa kodi tusiwaulize hawa watu, ni siri maana maadui wakijua hili watajua kwamba jeshi letu badala ya kununua silaha linagawana pesa hivyo tunaweza kushambuliwa na maadui, Tusiwaguse kabisa hawa watu waendelee kuilinda hii amani tunayojivunia
   
 5. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Kazi kweli kweli ndio aina ya wapinzani tulionao hawa...
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu kama uchaguzi ukiwa ni about issues na sio vyama, sidhani kama kuna haja ya kuangalia huyu yuko chama gani au huyu ni rangi gani. Kama issue ni ufisadi, na wewe kutoka chama hiki unapambana na issue hiyo, na yule kutoka chama kile anapambana na huo huo ufisadi, nongwa iko wapi?

  Au upinzani maana yake ni kupinga kila kitu hata mazuri? Unajua kuwa mazuri tunayoona leo kutoka opposition yanaungwa mkono na wabunge wengi wa CCM, au unajua kuwa ni watu wa hukohuko CCM ndio waliotoa msada mkubwa kwenye kufichua ufisadi?

  Kwa maoni yangu mpinzani anayepinga kila kitu hata kizuri si mpinzani bali ni mpuuzi. Cha muhimu sana kwetu ni Tanzania yetu, so vyama.
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Watazitapika tu subiri 31 oct
   
 8. J

  Jafar JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Your argument above is nonesense. No one, no one is eligible to steal anything, even God the most high denies theft.
  Shimbo should now speak the truth about MEREMATA, if he was bold enough to speak on POLITICS why is/was silent on MEREMETA?
   
 9. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Wamelinda amani gani? kama wanajua kulinda amani mbona wanyarwanda wanavuka mpaka na kuvamia raia na kuteka magari? wajui chochote hawa. Watanzania tumechoka bana!
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Mkuu; Ezan was only being sarcastic!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,475
  Likes Received: 19,863
  Trophy Points: 280
  Unasemaje? Wewe pumbafu kabisa . Mods fungia hii mutu.
   
 12. M

  MC JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45

  Either haujui unachokisema au uko kwenye Pay row ya Rostam, what the hell are you talking about??xx!!$&
   
 13. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kweli eza, tusije tukalisababishia matatizo jeshi letu.
   
 14. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  majibu yote octoba 31
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Bwe he ehe..u r such a JOKER..

  Naanza kuamini kuwa avatar ya mtu ina mafungamano na mtumiaji wa ID.
   
 16. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duh!
  huyu jenerali hakujua kuwa anajilengesha kwenye tundu bovu..keshanasa sasa, na hapo hawafurukuti tena.
  Hayo ndiyo malipo ya uovu.
   
 17. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Amani nafikiri iko kwako wewe na mafisadi binafsi ile amani ya kuita amani siioni, kuna pori huko mikoaya Kagera,Kigoma kuna jamaa waishi humo na silaha nzito na wasafiri waopita njia hiyo kila leo wanaibiwa na kufanyiwa vitendo vya ajabu, hapo Dar kuna maeneo watu hawalali kila leo kuingiliwa na majambazi na kuawa na kukatwa mapanga kama polisi wangukuwa na wanatoa takwimu uliza kila mwezi matukio ya watu wasio na hatia wachapa kazi wanauawa na kutiwa majeraha na vilema kwa ajili ya ujambazi. Hivi mambo yanakera sana
   
 18. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwenye hoja mzito kama hizi malaria sugu lazima ajifiche mbali sana.
  Na mkimuuliza tu, lazima aseme mna mnyanyapaa na kumtenga.
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwa kuwa amejiingiza kwenye siasa kuna haja Shimbo akaijibu hiyo oja ili turudishe imani kwa Jeshi maana ni hela nyingi sana izo.
  Hao wana hofu Slaa akiingia madarakani waliokwapua fedha kwa mgongo wa meremeta wataambulia Lupango?
   
 20. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu Jenerali alikurupuka kuongea na waandishi wa habari masuala ya kisiasa bila kupima upepo na nyakati za majeshi kuingilia siasa zimekwisha, sasa wapinzani na wanaharakati wanampiga virungu , CCM na gazeti la MTANZANIA wanamuunga mkono kwa watu walineutral tayari anaonekana aliongea kwa manufaa ya nani?
   
Loading...