Elections 2010 Slaa ampiku Kikwete Kyela

Rugemeleza

JF-Expert Member
Oct 26, 2009
668
136
Hivi ndivyo mambo yanavyozidi kunoga. Angalizo ni katika kupiga na kulinda kura tu!


Slaa ampiku JK Kyela
• Waahidi kumpa urais yeye, ubunge Mwakyembe

na Janet Josiah


amka2.gif
KATIKA mazingira ya kisiasa ambayo hayajapata kutokea tangu kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, juzi jioni alilazimika kumnadi mgombea ubunge wa Kyela kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe. Hali hiyo ilitokea baada ya Dk. Slaa aliyekuwa katika jimbo hilo la uchaguzi kutaka kusikia maoni ya wananchi wa Kyela kuhusu namna watakavyopiga kura za kumchagua rais na mbunge.
Tukio hilo lilikuja baada ya Dk. Slaa kupanda jukwaani na kuwauliza wananchi waliokuwa wamefurika katika mkutano wake wa kampeni ni mgombea gani wa urais waliyekuwa wakimuunga mkono na kwa kauli moja wakamjibu wakisema ‘ni wewe Dk. Slaa’ na ilipofika katika ubunge wakamjibu kwa sauti ya pamoja ‘Mwakyembe’.
Jibu hilo la wananchi lilisababisha Dk. Slaa akubaliane na masharti aliyopewa na wapiga kura hao wa Kyela na akawataka waende kwa Mwakyembe kumueleza kwamba atakuwa tayari kufanya naye kazi katika serikali yake ijayo atakayoiunda baada ya kutangazwa mshindi wa urais Novemba mwaka huu, iwapo tu (Mwakyembe) ataacha kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete.
“Kama mnamtaka Mwakyembe nitaweka masharti… mwambieni lazima afuate masharti yangu. Kwamba afuate masharti ya rais tunayempenda… lazima atetee maslahi ya wananchi kwanza kabla ya kutetea CCM...Nataka mbunge ambaye nitaweza kumtuma kazi. Mwambieni kuwa, Dk. Slaa anaenda kuchukua urais, kama huwezi kufanya naye kazi, katiza nimchukue Eddo (Makata),” alisema Dk. Slaa.
Eddo Makata ndiye mgombea ubunge katika jimbo la Kyela kwa tiketi ya CHADEMA ambaye alipopewa nafasi ya kuhutubia alisema alikuwa tayari kusubiri miaka mitano iwapo tu Dk. Mwakyembe atakuwa tayari kumnadi Dk. Slaa katika kampeni zake.
Akizungumza kwa kujiamini huku akishangiliwa na wakazi wenzake wa Kyela, Makata alisema yeye si mwanasiasa mbinafsi na kwa hiyo anawapa uhuru wananchi wa Kyela kumchagua mbunge wanayemtaka japo kwa masharti waliyompa.
“Kama Dk. Mwakyembe atamnadi Dk. Slaa na mimi nitasubiri hadi 2015. Nitayaheshimu maamuzi yenu,” alisema.
Akimzungumzia Mwakyembe katika mkutano huo, Dk. Slaa alisema alikuwa tayari kufanya naye kazi kutokana na kutambua kwake kwamba amekuwa akinyanyaswa na kupigwa vita ndani ya CCM kutokana na msimamo wake wa kutetea wananchi.
Akionyesha kumuunga mkono mgombea wake wa ubunge, Dk. Slaa alisema, “Mimi si mwamuzi, wananchi chagueni mbunge mnayemtaka…na wewe Eddo, Kama Mwakyembe ataendelea kumnadi Kikwete, endelea na kampeni ukimnadi Slaa.”
Dk. Mwakyembe ni mmoja wa wabunge wa CCM waliojipambanua kama wapambanaji wa ufisadi na ndiye aliyeongoza Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wenye utata wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond, ambayo hatima yake ilimlazimisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu wadhifa wake miaka mitatu iliyopita.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema Dk. Mwakyembe anatambulika miongoni mwa wapiga kura wake kama shujaa wao, ambaye wiki iliyopita alifanya kazi ya ziada kuwaomba wana Kyela wawe watulivu wakati Rais Jakaya Kikwete alipokwenda kuomba kura.
Jana Dk, Slaa aliendelea na mikutano yake katika majimbo ya Mbeya Vijijini na Mbeya Mjini, akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Mbalizi, aliwataka waichague CHADEMA ili iwapelekee dira ya maendeleo na siyo ahadi za bajaji 400 kwa kina mama wajawazito ambazo aliziahidi Kikwete akiwa katika kampeni zake.
“Wananchi wa Mbalizi, mmeandika mabango kuwa Kikwete ‘bye bye’ na bajaji zake … na mimi nasema bye bye kwa kuwa wananchi wamechoshwa na sasa wanataka mabadiliko, si bajaji,” alisema Dk. Slaa.
Alisisitiza kuwa iwapo ataingia Ikulu, serikali itaifanya elimu ya lazima kwa kila Mtanzania kuwa kidato cha sita, na italipiwa na serikali; na kwamba wananchi watatibiwa bure kwani ndizo huduma wanazostahili kwa kodi wanayolipa.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Kweli Ngoma inogile, Dr Mwakyembe kazi kwako, najua ugumu upo kidogo hapo, lakini, bakia kuwatete wananchi wako, achana na group politics, la sivyo, mtachafuliwa wote.
 
Kwa kweli Slaa ni makini, anaangalia kwanza wananchi kwanza! Heri Kikwete angekuwa hivi!
 
"Kama mnamtaka Mwakyembe nitaweka masharti… mwambieni lazima afuate masharti yangu. Kwamba afuate masharti ya rais tunayempenda… lazima atetee maslahi ya wananchi kwanza kabla ya kutetea CCM...Nataka mbunge ambaye nitaweza kumtuma kazi. Mwambieni kuwa, Dk. Slaa anaenda kuchukua urais, kama huwezi kufanya naye kazi, katiza nimchukue Eddo (Makata)," alisema Dk. Slaa.

Dr. Mwakyembe huna namna ila kumtema JK maana amekuwa ni mzigo CCM na hauziki. Usipomtema JK na ubunge kwa kheri.

BYE BYE JK NA BAJAJI ZAKO KARIBU DR. SLAA NA UTAWALA BORA.

TUMECHOSHWA NA HONGO ZA CCM
 
Unajua Slaa anajua wazi kuwa wapiga kura kwake ni kama mteja so customer is a king/queen matakwa yao kwanza.
Ingawa kwa CCM ni kinyume hawatambui umuhimu wa wapiga kura wao kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
JK anakosa kura kyela kwa sababu ya kumback up Mwakipesile kama RC wakati watu walimwambia amtoe akadharau.
Naona akadhani watu wa kyela vichwa vya kuku watasahau kama wakwele kumbe laaaaaaaaaaah
 
This is a message for 2015. Mwakyembe take it. Gari ulilopanda halifai kurepea tena... Jipange sawasawa, shuka na 2015 (au kabla ya hapo), panda gari jipya...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom