Slaa Akata Anga Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa Akata Anga Morogoro

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masanilo, Aug 30, 2010.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Slaa akata anga Morogoro


  LEO Dk. Willlibrod Slaa alikuwa mkoani Morogoro, katika wilaya za Mikumi na Mvomero. Mikutano imefana. Amesisitiza haja ya Morogoro kuwa na wabunge wa upinzani ili kuongeza uwajibikaji katika halmashauri za mkoa huu, na katika nchi nzima kupitia Bunge; na kudhibiti wizi wa fedha za umma.

  Akiwa Mikumi, alimlipua mwenyekiti wa kamati ya kampeni za CCM, Abdulahman Kinana, akisema kigogo huyo ana mkono katika biashara chafu za makampuni ya meli; akamtaka ajielekeze katika masuala ya kitaifa badala ya kumwandama yeye (Slaa). Akasisitiza kwamba ana ushahidi wa kauli zake, kwani hana historia ya kukurupuka.

  Kauli hiyo ya Dk. Slaa inakuja siku moja baada ya Kinana kujibu mapigo ya makada wa Chadema, hasa Mabere Marando, ambao waliwataja hadharani vigogo wanaohusika na ufisadi mkubwa, huku CCM ikilalamika kwamba chama hicho cha upinzani kinatoa matusi.

  Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za Chadema, Marando alisema vigogo waliohusika na wizi wa EPA ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, Rostam Azizi na Edward Lowassa, akasema waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi ni dagaa wanaoonewa ili kuficha madhambi ya wahusika wenyewe wa ufisadi.

  Juzi Kinana alijitokeza na kumbeza Dk. Slaa, kwamba anatumia lugha ya matusi kwenye kampeni kinyume cha makubaliano waliyosaini. Dk. Slaa jana alisema mtu akiiba anaitwa mwizi; na kwamba kumwita hivyo si matusi

  Source: Ngurumo
   
 2. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Rev. Natamani kila mtu ajue hizi habari ila ndio hivyo tena. News ya ch-ten haikuwa na hii kitu nikajua mzee kapumzika. Wao walikuwa na makamba akilalamika eti mtu akimtukana baba ako huwezi muacha! Sasa sijui jk ni baba ake na makamba! Fanyeni mpango mwingine maana naona hali ya hewa sio nzuri radi imeanza na mvua itashuka si mda!
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaaa kazi imeanza
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nimependa hiyo ya mtu akiiba anaitwa mwizi.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  unajua CCM sijui wakoje mtu mwizi ni mwizi tu ..au wanataka mwizi tumwite honey and sweetheart
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kinana ameyataka Mwenyewe! I hope hii ni salamu kwako Mjomba
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kuongea kenyewe hawezi anajidai kuwachokoza akina Slaa atajuta
   
 8. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Du! Sasa kumekucha . . . . tutasikia mengi . . .
   
 9. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kweli kumekucha! Kama kinana ndio msafi akaachwa awe mtetezi maana yeye hawezi guswa! Kumbe kanyaga bomu haya limelipuka! Inaitwa Nikanyage bahati mbaya nikulipue makusudi! Dr. endelea kula vichwa!
   
 10. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Imagine Komba wa TOT yuko Upinzani na sasa ametunga wimbo kuhusiana na hii issue . . .

  Kuna mbunifu yeyote anyeweweza kushusha verses hapa . . .
   
 11. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #11
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Chadema need to respond ccm smearing machine on time and felociously, chadema ndo wanaongea issue ya ufisadi ccm wanawapaka matope wametoa matusi, that is dirty politics ccm wanayoitumia na chadema inabidi wawe very smart to brash away ccm mud, hizo tricks za smearing campaign ndo bush alizokuwa anatumia in 2000 and 2004 kwa kumtumia spin master wake anaitwa carl rove, kuwapaka matope al-gore and later john kerry, lakini obama alisoma kitabu chao cha dirty politics and smearing campaign ambacho mcain alikuwa atumia vilevile in 2008 but it did not work
  kwa sababu obama was responding quickly and setting the record straight na alikuwa na surrogates kibao ambao walikuwa wana flood media, hivyo basi chadema inatakiwa kuwa na strong surrogates kwenye kila kanda wao kazi yao ni kujibu mashambulizi na smears zote ccm wanazozitoa.

  Ccm wanatumia kila liwezekanalo chadema wasipate uhalali wa kuzungumzia ufisadi na mbinu chafu waliyokuja nayo ni kuwa label chadema kama radicals na wahuni, kumtuhumu mtu au chama kuwa kimesema matusi na lugha chafu is very wrong, they need to demand serious explaination matusi gani na lugha chafu gani? Wakishindwa kurudia hayo matusi then need to apologize na wananchi wafahamishwe kuwa ccm wana hofu ya kuwa exposed madhambi yao ndo maana wanatumia tricks za kutupaka matope, vyama vya upinzani jukumu lake ni kutafuta udhaifu ya chama kilichopo madarakani na kuutumia kuwanesha na kuwashawishi wananchi kuwa weakness za ccm ni hizi ndo maana hakistahili kurudishwa madarakani, ccm walichotakiwa kufanya ni kujibu hoja kwa hoja kwa vielelezo, this is strugle for power sio kutoa ahadi kibao ambazo ulizotoa nyuma hujatekeleza,
  ccm wasijalibu ku set issue za uchaguzi za kuzungumzia kila chama kitakwenda na issue zake and then watanzania tutaamua. Unajua ccm wameishiwa kabisa ndo maana wanaleta sababu zisizo kuwa na msingi wao ndo wamezua kuwa chadema wamesema matusi
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sasa ndiyo naanza kuelewa kwa nini CCM wanasisitiza lugha za ustaarabu wanaogopa kuumbuliwa madhambi yao, Kinana naye kesho aseme katukanwa kwa kuambiwa ukweli kuwa ana mkono kwenye biashara chafu ya meli. Kwani kusema ukweli ni matusi au wanafikiri sisi hatujui matusi ni kitu gani, wao wajibu hoja wasikimbilie kutukanwa au waende mahakamani.
   
 13. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #13
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CHADEMA inabidi wawe na surrogates kila kanda wa kujibu matope ya CCM within 24hours, CCM wanachokifanya ni kuwachanga wananchi waache kuzumgumzia masuala mazito waongelee upuuzi wa hicho wanachodai ni matusi
   
 14. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kama namuona vile Kinana!! Amekanyaga bomu.

  However, ni vizuri CHADEMA kuweka records staright ili kwenda sawa na wakati. Inabidi Abdulhaman Kinana akose la kusema!!

  Go Slaa...
   
 15. T

  Tom Lyimo Member

  #15
  Aug 30, 2010
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ufisadi au kuitwa wezi sio lugha za matusi jamani wanataka lugha gani zitumike!
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nimefurahia sana hili alilosema baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.

  " Kila nilipokuwa nikitaka kung'atuka, walikuwa wakiniambia Mwalimu andelea tu, hii nchi bado ni changa na umeitoa mbali, nchi haitaendelea bila wewe. Nami niliendelea, hadi pale nilipokuja kugundua kumbe nchi changa wanayoiongelea ni FAMILIA ZAO, na hazitaendelea bila mimi kuwepo madarakani, maana walikuwa hawana uhakika kama RAIS ajae atawaacha katika nafasi walizokuwa nazo" Julius Nyerere
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Slaa just call a spade a spade and not a spoon.

  CCM na kundi lao ni wezi na wanahitaji kuitwa wezi. Hivi wanategemea tuwaite vipi?
   
 18. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  REV Masanilo nishakula Ndovu sijui kama nitaweza kuweka msisitizo niotaka. Kinana kakiri kuwa meli iliyokamatwa China ikiwa na meno ya Tembo kutoka Tanzania, ni mali yake kwa kumiliki hisa 7,500 kati ya hisa 10,000 za maeli hiyo. Sasa ni kwanini tuansumbuliwa kichwa na huyu mtekaji meli wa Kisomali?

  Watanzania kibao wako Keko, Segerea na Ukonga kwa kukutwa na mali za wizi majumbani, ofisini katika magari n.k. Iweje majeshi ya kimataifa yakute mali ya iliyoibiwa Tanzania katika meli ya Ndg Kinana na Jeshi letu la polisi lshindwe kuchukua hatua za kufaa za kumuunganisha katika kesi hiyo kama wanayowafanyia watanzania wanokutwa na mali za wizi? Iweje huyu kikbaka wa Kisomali aliyekutwa na nyara za Tanzania alipopanga asihusishwe katika kesi hiyo? Hivi Mwema kaenda likizo kipindi hiki nini?
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Jatropha,
  Mwema yupo. Lakini kuna watu hawaguswi Bongo. Chenge ni mfano mmojawapo.
   
 20. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Alafu Chadema wote mnafanana akili. Kama vile babu wa babu zenu alikuwa mmoja na alikufa kwa kifafa!
   
Loading...