Elections 2010 Slaa akashitaki wapi kama sio kwa wananchi waliomchagua jamani???? Sheria haimruhusu.

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
Sheria ya nchi inakataza mtu au kikundi cha watu kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uraisi hata kama kuna ushahidi thabiti kuhusu kasoro za uchaguzi. Lakini katika hali isiyo ya kawaida CCM walikuwa makini kuweka sheria hii kwa kuwa walijua fika 2010 au kabla ya hapo wangewekwa pembeni... They were corruptly intelligent to sign this law.. Walijua fika kuwa ambaye atakataa matokeo watamwita mzushi, mchochezi na aliyetepeta kihoja!!

Nini kifanyike kama kuna ushahidi kamili kuhusu kuibiwa kura:: Nenda zunguka nchi nzima waambie wananchi kuwa kura ziliibwa na wasiyemtaka kashika hatamu.. Pia njia ya maandamano(sio fujo kama wanavyodhani CCM) ni njia sahiihi.
Pili nenda kashitaki mahakama za afrika mashariki ikiwemo kupinga shera kandamizi kama hizi.
Tatu kushitaki kwa nchi marafiki na kuonyesha ushahidi tosha.. Misaada itasitishwa (Zanzibar ilitokea hii mpaka wakatii amri). si kuubaya lakini kwa mustakabali wa nchi...

Operesheni sangara makini nchi nzima kuhakikisha majimbo yote sasa yanaamka hasa kati ya tanzania na kusini mashariki mwake. Mimi nadhani kwa sasa kufanya vurugu si jema saana lakini kukataa kwenda sherehe za kuapishwa na matokeo ilikuwa sahii kwa kuwa wewe Slaa si mnafiki.. Mi nadhani CHADEMA wana kila cha kushukuru kwa kazi nzuri ya Slaa aliyofanya na ambayo ataendelea kufanya kwa kuwa uchaguzi:israel: ni saa yoyote tokea sasa na si miaka mitano kama wengi tunavyodhani basi si vibaya Operesheni kama hizi zianze sasa.

Mimi nadhani nimeshawasilisha!!!!
 
Me chochote anachoamua Dk juu ya hii tume ya uchaguzi ya 2010 naunga mkono. Kwani kweli kasoro nyingi tumeziona, angalia mbeya, shinyanga,mwanza na hata kawe
 
Back
Top Bottom