Slaa akanusha vikali taarifa za Rostam kuunga mkono CDM Arumeru; Vita ya Saikolojia kuendelea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa akanusha vikali taarifa za Rostam kuunga mkono CDM Arumeru; Vita ya Saikolojia kuendelea!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 28, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Kulikuwa na taarifa zimeenezwa na hata kuwafanya baadhi ya watu kuamini - kimsingi wakitilia mashaka msimamo wa CDM na mafisadi. Dr. Slaa ametoa maelezo mafupi juu ya hilo:

  Kuelekea siku hizi chache zilizobakia kutakuwa na majaribio ya kuteka akili za wapiga kura kwa kutangaza taarifa mbalimbali na tusishangae kama vyombo vya habari vya serikali vikatumika kutoa taarifa ambayo itachelewa kusahihishwa ambayo itatoa madai fulani. Madai hayo yaweza kuwa ni yale ya kuonesha kuwa matokeo tayari yako wazi kwa CCM kushinda kwa mfano "CCM yaelekea kushinda". Mbinu kama hii tumewahi kuona ikitokea sehemu nyingine ambapo watu wanakata tamaa na kuacha kupiga kura kwa sababu tayari CCM itashinda.

  Mojawapo ya vitu vinavyosumbua sana ni hisia kuwa hakuna jinsi ya kushinda kwani CCM ina serikali, vyombo vya dola, Tume n.k na hivyo kushinda itakuwa kazi sana. Matokeo yake baadhi ya watu wanaweza kuamini kabisa kuwa kura zao hazina maana yoyote kwani hata wapige kura vipi bado "zitachakachuliwa". CDM haina njia nyingine ila:

  a. Kuonesha ugumu wa kuiba kura za wabunge hasa kama watu wanapiga na kuwa tayari kulinda kura hizo - watu wajue ni lazima matokeo ya kila kituo yatangazwe hadharani na wananchi wanayo haki na ruhusa ya kupiga picha matokeo hayo na kuyatangaza mahali popote.

  b. Kura zote zinahesabiwa kwenye vituo; hakuna kuhamisha masanduku kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine "ili zihesabiwa". kura zote zinahesabiwa kwenye vituo zilipopigiwa na baada ya kukamilisha matokeo ni LAZIMA yawekwe nje ya kituo kwa mtu yeyote kuyaona.

  c. Mawakala wa vyama ni sauti ya chama hicho kwenye chumba cha kura; hivyo chama kinatarajiwa kuwa na mawakala waadilifu, wenyeji na watu wanaojua maeneo hayo na ni jukumu lao kuhoji, kuuliza jambo lolote ambalo wanaona haliendi sawa. Kwa mfano, kwenye chumba cha uchaguzi hairuhusiwi kuleta sanduku jingine la kura kutoka nje mara baada ya vifaa vyote kuchunguzwa mwanzo wa siku ya kupiga kura. Mabadiliko yoyote ya utaratibu mawakala wanaruhusiwa kunukuu na wakiwa makini waweze kuandika chini.

  d. Wakati wa kuhesabu kura mawakala ni lazima wawe na sehemu yao wenyewe ambapo wanahesabu kura na kujumlisha. Matokeo ya kujumlisha kura hayawezi kutofautiana hata kwa kura moja! Kama wamehesabiwa watu 1000 kupiga kura zote ni lazima ziwe 1000 (halali, zilizoharibika n.k). Mawakala ni lazima wahakikishe kura zinajumlishwa kwa usahihi na kuwa makini wanapohesabu na kuamua kura zilizoharibika.

  Vyovyote vile ilivyo, CDM wanapaswa kuwa makini na vita ya saikolojia inayoendelea.
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  bado watakuja na taarifa nyingi sana, si ajabu hata gazeti la habari leo na TBC wakatoa breaking news kuwa Dr.Slaa atorokwa na mchumba wake, mbowe atoa bastola kumtishia Dr.slaa kikaoni, aaagh! ni mengi tu tutayasikia ambayo hata hayahusiani na uchaguzi, kweli hii ni vita.
   
 3. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hisia kuwa hakuna jinsi ya kuishinda CCM ati kwa kuwa ina Serikali, vyombo vya dola, Tume ya Uchaguzi n.k ni hisia potofu na inayotakiwa kupigwa vita kila kona ya nchi kwani ingekuwa hivyo tusingeshuhudia majimbo makubwa na muhimu kama Arusha, Ubungo, Kawe, Mbeya na mengineyo yakichukuliwa na upinzania tena kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi uliokuwa unaihusu nchi nzima na sio jimbo moja kama tunavyoshuhudia huko Arumeru.

  CDM wanatakiwa kuelewa kwa undani ujanja unaotumiwa na CCM kwa sasa ya kutaka kuhamisha mawazo na akili za wananchi na viongozi wa upinzani kwa ujumla kwa kuanzisha hoja ambazo hazina mantiki yoyote zaidi ya kutaka kuwagawa wananchi na viongozi wa upinzani kwa lengo la kutaka kupandikiza chuki na mifarakano miongoni mwao.
   
 4. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kumbe Dr Slaa naye mbishi na mwongo. RA ameonwa hivi hivi akitembelea kambi zao, hii inakuwa kama Mtikila alivyoenda kuomba kusaidiwa na huyo huyo RA kisha .......
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  ameonekana akizungumza na Dr. Slaa?
   
 6. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hizo kambi za CDM ama viongozi wa CDM ziko wapi na zimeanzishwa lini!!!!!
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanakijiji is too low for you kufanya Argumement na Maiti hai!!.....
   
 8. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwenzio ni mdadisi ila wewe mahaba ya CDM yamekuelemea na hutaki kujua ukweli
  Amka
  OTIS
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Siwezi kuidadisi maiti....is belongs to the grave yard.
   
 10. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Sio kuzungumza na Dr Slaa ila akitembelea kambi za CDM. Kutembelea kambi ya CDM, ukapokewa vizuri, ukatoa hoja, ikasikilizwa na ikakubaliwa ina maana imebarikiwa kutoka kwa viongozi wa juu wa chama hicho, hivyobasi ni vigumu kumtangamanua Dr Slaa na tukio la RA kutembelea kambi hizo.
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuweka ushahidi wa picha kama zile za kina Maji marefu?......
   
 12. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Maiti hai, du, inasumbua kueleweka ......!
   
 13. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Sio kila jambo lazima picha .... think deep and scout around!
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Sasa unadhani maiti huwa inaelewa nini?......
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  One the most flawed reasoning... yaani kutoka kimoja hakiendi kwa kingine.
   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  How can you support what u want us to believe! evidence is only the way to proof the truth. not blah blah!
   
 17. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Inaonesha wewe ni afande! ngoja nimwite advocate wangu ili nikijibu awe karibu kusikia majibu yangu
   
 18. F

  FOEL Senior Member

  #18
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Matola, heshima mbele sana kiongozi.

  Hii ni post ya nne au tano nakutana na habari ya picha za maji marefu, unaweza kuziweka hapa ambao tumepitwa tuzione na issue yenyewe ilikuwa inahusu nini mkuu, kama vipi tuwekee hata link ya hiyo habari, samahani kwa usumbufu mkuu.
   
 19. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Who taught you that photos are the only reliable evidence my dear!
   
 20. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkubwa na Mzee Mwkjj ni wewe tu umeshindwa kuunganisha, mbona hiyo inaeleweka na kuunganika sana tu!
   
Loading...