Slaa airushia UVCCM kombora • Asema yupo tayari kupimwa akili nzuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa airushia UVCCM kombora • Asema yupo tayari kupimwa akili nzuri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 23, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  Slaa airushia UVCCM kombora
  • Asema yupo tayari kupimwa akili nzuri

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, amesema yupo tayari kupimwa akili nzuri alizonazo za kupambana na wanaotafuna rasilimali za taifa.
  Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili juzi, Dk. Slaa alisema kuwa yeyote mwenye kutetea rasilimali za taifa zisitafunwe na walafi wachache waliopo ndani ya Chama Cha Mapinduzi hawezi kuwa na matatizo ya akili.
  Kauli hiyo aliitoa baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kuitaka serikali imkamate kiongozi huyo na kumpeleka katika hospitali kumpima akili.
  Katibu Mkuu wa UVCCM (taifa), Martin Shigela, alisema wameamua kutoa kauli hiyo baada ya kujiridhisha kuwa kiongozi huyo wa upinzani hakutakiwa kukataa matokeo ya urais kwa kudai kura zake zimechakachuliwa (kuibwa).
  Aliongeza kuwa Dk. Slaa ni miongoni mwa vinara waliochangia kuhamasisha vijana wafanye maandamo yaliyopigwa marufuku na Jeshi la Polisi mkoani Arusha, ambako vijana watatu walifariki dunia na zaidi ya 20 kujeruhiwa.
  Umoja huo ulisema Dk. Slaa amekuwa akitoa kauli mbalimbali za kichochezi ili kuwafanya wananchi wasiiamini na kuipenda serikali ya CCM chini ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete.
  Akijibu mashambulizi hayo ya UVCCM, Dk. Slaa amesema yuko tayari kupimwa akili zake nzuri alizonazo kutokana na kuwa mstari wa mbele kuibua hoja nzito dhidi ya serikali.
  “Unakwenda kunipima akili kwa kitu gani? Mimi naona nipimwe kwa akili nzuri, maana siku zote nimekuwa nikisimama kidete kutetea rasilimali za nchi, likiwamo suala la Dowans kutolipwa.
  Sasa kati ya mimi, Shigela na vijana wenzake wa CCM, nani akapimwe akili zisizofaa?” alihoji Dk. Slaa.
  Alisema umaarufu wa mtu na umakini wake unatokana na ujengaji wa hoja na anavyozitetea pamoja uungwaji mkono wa jamii, hivyo haoni sababu kwa watu wa aina hiyo wapimwe akili.
  Aidha, mkoani Mwanza, Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, (CHADEMA), amemtaka Rais Jakaya Kikwete, asome alama za nyakati, ili asije kuitumbukiza nchi katika migogoro na machafuko ya umwagaji wa damu kama ilivyotokea nchini Zimbabwe, Kenya na Ivory Coast.
  Alimtaka Rais Kikwete kuwaongoza Watanzania kwa misingi mizuri na kufuata matakwa ya Katiba ya nchi, vinginevyo atasababisha kutoweka kwa amani na upendo ulioachwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.
  Mbunge huyo alitoa kauli hiyo juzi jimboni humo wakati akiwahutubia mamia ya watu katika mikutano miwili tofauti ya hadhara ya kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura na kumwezesha kuwa mbunge.
  Highness alisema dalili zinavyoonekana hivi sasa zinaashiria serikali kushindwa kuwaongoza vema Watanzania, jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi. “Namtumia salamu Rais Kikwete ahakikishe analiongoza taifa letu kwa kufuata Katiba ya nchi, asije akalizamisha kwenye machafuko kama yaliyotokea Kenya, Zimbabwe...hatutaki kuona wananchi wetu wanapigwa mabomu na kuuawa na polisi,” alisema.
  Highness alitumia fursa hiyo kulaani mauaji yaliyotekelezwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha, Januari 5, mwaka huu wakati wakiwazuia wanachama na viongozi wa CHADEMA kufanya maandamano ya amani.
  Alisema ni heri serikali ikajikita zaidi katika uboreshaji wa maendeleo ya wananchi, ikiwa ni pamoja na kutatua kero na matatizo mengi yanayolikabili taifa.
  Aliongeza kuwa ni vema Rais Kikwete akalionya Jeshi la Polisi liache kufanya kazi kwa misingi ya kisiasa kama inavyoonekana sasa.
  Highness aliwahakikishia wananchi wa Jimbo la Ilemela kuwa ahadi zote alizoahidi atazitekeleza, ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha polisi Kata ya Bugogwa-Igombe, kuboresha sekta ya elimu, barabara, maji na afya.
  Katika mikutano aliyoifanya Highness, wananchi walimtaka mbunge wao huyo kuhakikisha anaporudi bungeni asimame kidete kupinga dhamira ya serikali ya kutaka kuilipa Kampuni ya Dowans sh bilioni 94.
  Wananchi hao wamemtaka mbunge huyo asimamie suala hilo ili fedha hizo zielekezwe kupeleka maendeleo kwa wananchi na zisaidie kupunguza umaskini.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  Nimeshangazwa sana na kamati kuu ya CCM kutowakemea UVCCM kwa kutumia lugha za matusi dhidi ya Dr. Slaa ..................lugha ambazo ni za kiuchochezi na ambazo kama zisipotumika busara na utashi viongozi wengi wa CCM wataanza kutukanwa hadharani kama kujibu mapigo ya UVCCM.........................

  Kitendo cha Kamti KUu kukaa kimya kunaashiria ya kuwa wao ndiyo waliowatuma UVCCM kumtukana Dr. Slaa...........................na inashangaza polisi kupiga ganzi kwenye suala nyeti kama hili na hivyo kututhibitishia ya kuwa wapo upande wa watawala wa leo na wala siyo kutenda haki hata chembe..........................
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kwa jinsi walivyoandika lile tamko likiwa na mapungufu mengi ya kimantiki, kiuelewa na tyiping errors, UVCCM wamejionyesha kuwa ni genge fulani la wahuni. Inaonekana CCM iliamua kwa makusudi kuweka vilaza kwenye uongozi wa CCM ili wasiweze kuwa tishio la madaraka kwao.
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  siku zote kumtukana mtu aliyekuzidi sana umri ni utovu mkubwa wa adabu na maadili. dr slaa wasamehe hawa hawajui watendalo baba
   
 5. d

  dos santos JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  hakuna haja ya kupimwa akili matendo na maneno yake yanamhukumu. Kupora mke wa watu na kumzini halafu anatuambia ni mchumba wake. Ni kama mrema tusubiri tuone
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  UVCCM ni pumba.
   
 7. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hao makuhadi wa ccm mwisho wao umekaribia!! iko siku watatafuta chaka
   
 8. c

  cerezo Senior Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  akili zako zimechakachuliwa
   
 9. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Vp mkuu? Umesahau kwenye kampeni meseji za kuhatarisha amani,za kugawa watu kidini na makabila zilitumika kumwokoa ckeckbob Jk lakini usalama wakawa wanashangilia(Cheap politics).Matokeo yake leo baadhi ya madhhebu yanagombana kuhusu dini wakisahau kuwa adui wao ni JK na mafidi wanzake.Je ni mashekh wangapi watalipwa kwenye hela za Dowans,wako bize na adui wao katoliki,jk na maswaiba(mgombanishaji) wanachekelea umasikini unapaaa.Cheap politics and its results on psycho-politics
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hivi kukichukia chama tawala kunahitaji uchochezi kweli??Kila mwenye akili timamu anatambua njia wanayotupeleka sio na ambao bado wanaikumbatia ndo haswaa wanahitaji kupimwa akili!Sijui inakuaje hawaoni matatizo yetu na walio/ wanaoendelea kusababisha pamoja na kuyaendekeza!Aibu iliyoje kua na vijana wasio na mwamko kama hao wa uvccm!Kweli taifa la kesho kwa upande huo hatuna!!
   
 11. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  1.dos santos, tuseme kuwa wewe ni mwanamke:
  Umeolewa lakini baadaye mumeo kakutelekeza wala hakuhitaji tena na ameamua kumwoa mwanamke mwingine. Kwa bahati ukampata mwingine na mkaamua kuoana naye na anakupenda. Je, huyo mumeo wa pili utamwita mporaji wa wake za watu? utafurahi kusikia watu wakikuambia urudi kwa yule mume wa kwanza kwamba huyo uliyenaye unazini naye?

  1.dos santos, tuseme kuwa wewe ni mwanaume:
  Mke wako wa kwanza umeachana naye kwa sababu unazojua mwenyewe lakini umekubali uachane naye. Baadaye ukamwoa mwingine. watu wengine suala hilo linawahusu vipi?ukiachana na mke wako unahitaji kuwataarifu watu. Hivi ulipokuwa unalala na mkeo raha na taabu unazopata huko lazima watu wayajue?


  Ukitazama hoja zinazomhusisha Dr. Slaa na suala la uzinifu halina maana yoyote zaidi ya uzinifu ulio katika akili za wanazungumzia suala hilo. Tanzania hatujawa na desturi ya kuzungumzia ndoa za viongozi, lakini kwa Dr. Slaa inaonekana kama suala la maana. Hatukatai sana kwamba kama Dr. Slaa na Josephina hawajaoana kihalali kwamba si halali kuishi kama mke na mume vinginevyo itakuwa na picha mbaya mbele ya jamii na kwa mujibu wa imani yao. Lakini kufuatilia maisha binafsi ya Dr. Slaa kiasi hicho inaonyesha ufinyu wa akili wala hatumtendei haki. Fikiria kama wewe ni mwanaume au mwanamke na suala hilo linakuhusu wewe, utajisikiaje? Hata kama tukijadili suala hilo kwa sababu yeye ni kiongozi lakini katiba yetu haijazungumza lolote kuhusu maisha ya ndoa ya viongozi wala maadili ya viongozi wa umma haizungumzii maisha ya ndoa ya viongozi.
   
 12. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mimi nina swali: Hivi anayetuna na nayetukanwa nani anatakiwa kupimwa akili? Je Mtu mwenye akili timamu anatukana? UVCCM imewaaibisha vijana!
   
 13. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Hapo sawa kabisa!!!!
   
 14. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Umeabisha utu wako maana inaonekana hata hujui hata haki zako nina wasiwasi wewe bado upo na fikira za Ki-tanganyika!!!
  Pole Dos Santos
   
 15. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,812
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  wewe ni muhuni? Kwa namna ya usawa Dk Slaa na Dk Kikwete wanatakiwa wajadiliwe kwa hoja au ndio kweli JF imevamiwa. Kuipenda kwako CHADEMA au Dk Slaa kusiwazuie watu wasitoe madukuduku yao, tuambie basi kama haiko hivyo ikoje, hata mimi sielewi yaliyotokea kwa Rose Kamili mke wa kwanza wa Dk Slaa ambaye ni mkatoliki. Nijuavyo ndoa ya mke mmoja haiwezi kuongezewa mke mwingine, Mushumbusi siioni ndoa yake itafanyika wapi. Maisha binafsi ya atakayekuwa kiongozi mkuu nchi kama yeye ni lazima tuyajue kwa uzuri. Tanzania ni nchi yetu sote: si ya CHADEMA wala CCM, si ya waislamu pekee wala wakristu vinginevyo JAMII FORUM ibaki kuwa ya CHADEMA tu. Mwe!
   
 16. Mbeu

  Mbeu Member

  #16
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aisee inachekesha kweli, hawa ni vijana kweli mbona IQ yao iko chini namna hiyo. nasikitika kusema wanaogopa kufikiri kati yao na Dr. Slaa nani anapaswa kupimwa akili Slaa anatutetea sisi wanyonge wao UVCCM wanatetea Mafisadi. hii yote ni njaa kali ya vijana. inaelekea nyinyi mnapewa vijisenti kutetea haya MAFISI yanayo tufilisi. kijana anaye ona mbele hawazi toa tamko BOVU kama hilo, kwa hali ya kawaida i have to question your integrety. amini nakwambia over 70% of youth are solidly behind Dr. Slaa ukiona kijana anatoa kauli zisizo na msingi kama za UVCCM ujue baba, mama au mjomba is among the corrupt figures in the nation, au yeye mwenyewe anahongwa vijisenti ili aropoke kama KASUKU bila vina.
   
 17. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #17
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  KAPORA?!?!? KWA KUTUMIA SILAHA GANI!!! kuku,ng'ombe,tv and other non living things are capable of being ROBBED or STOLEN, MTU MZIMA HAIBWI WALA HAPORWI, Kila binadamu ana haki ya kumpa penzi anayemchagua yeye na kubadilisha mwenza wake anapoamua, ili mradi wamechaguana wao wenyewe, two consenting adults, na hakuna Josephine mwingine, by the way na YULE ALIYEBAKA MTOTO WA SHULE AKIWA HEADMASTER NA AKAFUKUZWA, naona yeye ndiye ana akili nzuri hadi anapewa cheo alicho nacho
   
 18. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  mbona unalazimisha??? lini dk alimwoa Rose Kamili? Dk alivyotoka upadrisho tena huku wakimng'ang'ania abaki kutokana na hadhi yake ya kiuongozi alikwenda kuishi na Rose Kamili ili aanze shughuli zake apendazo za siasa kwa kuwa alikwishaanza toka akiwa Songea pale Seminary. Lakini wakati anahama mwaka 1995 kwenda CDM Rose alikataa kuhama akiwa anasubiri cha bure toka CCM akashinda udiwani na mumewe ubunge. Lakini mwaka baadae walitofautiana saana kimtazamo na hakuna hata siku moja walipanda kanisani kuodheshwa.
  Na si kweli ndoa ya kikristo haijunjiki!! Wanasema ikithibitika umezini nje ya ndoa basi hakuna ndoa tena. Bwana Mashimbo alizini nje ya ndoa kwa hiyo kila kitu kilipanganyika na Dk akiwa katika pilika pilika zake akakutana na SINGLE mama Mashumbushi.. Basi yakatimia kama maandiko yasemavyo!!
   
 19. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 1,827
  Trophy Points: 280
  Na yule aliyebaka mwanafunzi ndo jiniazi wenu? tena mmempa hadi heshima kuwa Katibu mkuu wa Chama.
  kama ni Chama tawala hapo mnatoa fundisho gani kwa walimu wetu wanaotulelea watoto wetu huko mashuleni?
   
 20. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Hayo maneno yao tushayazoea..hata baba yao Makamba na Mjomba wao Tambwe Hiza ndo walimu wao,akiongea Mtikila wanamshtaki kwa uchochezi
  Ukimpuuza mpika majungu mwishowe yatamrudia mwenyewe
   
Loading...