Slaa aichongea CCM kwa viongozi wa dini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa aichongea CCM kwa viongozi wa dini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 30, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Slaa aichongea CCM kwa viongozi wa dini

  Exuper Kachenje

  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alikutana na viongozi wa dini na kuwaeleza maoni ya chama chake jinsi CCM ilivyoanza kucheza rafu kwenye mchakato unaoendelea wa uchaguzi mkuu nchini.

  Viongozi hao walimtembelea mgombea huyo wa urais kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam na kumueleza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya mpango wao wa kutembelea wagombea urais kwa vyama mbalimbali kwa lengo la kuwafikishia ujumbe wa haki.

  Lakini baada ya kuwasikiliza, Dk Slaa alianza kuvurumusha lalamiko moja baada ya jingine.

  “Nimefarijika kwa viongozi wa dini kuja," alisema mgombea huyo urais kwa tiketi ya Chadema. "Ni jukumu lao kuangalia amani ambayo huko nyuma ilitaka kuvunjika. Tunajua uchaguzi ni wa muda mfupi na amani haiji kutoka mbinguni."

  Dk Slaa, ambaye chama chake kimekuwa kikidai kuwa CCM imekuwa ikicheza rafu dhidi ya Chadema, alianza kueleza mtazamo wake kuhusu mchakato wa uchaguzi.
  "Wameeleza; tumetoa mawazo yetu; haki ikikiukwa zaidi hasa kutokana na CCM inavyofanya sasa, sisi hatutakaa kimya. Haki isipopatikana au isipotendeka na polisi kushindwa kuilinda amani na amani ikatoweka; wa kulaumiwa ni CCM,” alisema Dk Slaa.

  Alidai kuwa upo ushahidi wa wazi wa CCM kuvunja Maadili ya Uchaguzi na Sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati chama hicho ndio msimamizi wa mfumo huo kutokana na kuongoza serikali.

  “Tumeeleza kuwa vurugu kwenye uchaguzi huja baada ya matokeo; tumeombwa kuyakubali matokeo baada ya Nec kuyatangaza, lakini tunazo taarifa na waraka tumeunasa kuwa serikali imeagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha chama fulani kinashinda,” alisema Dk Slaa.

  Aliongeza kusema: “Ni mwendawazimu kwa mtu kuyakubali matokeo katika uwanja usio sawa. Kwa hiyo viongozi wa dini wachukue jukumu la kuhakikisha uwanja sawa unakuwepo katika kampeni.

  “Tunazo pia taarifa kwamba serikali imetuma timu kuzunguka kuwatisha watu, hata viongozi wa dini kwa madai kuwa wanaunga mkono upinzani, hili halikubaliki. Tulichoahidi tutaelimisha watu kwa kuzingatia wajibu wao na kujua haki zao, lakini wanapochokozwa, ninyi mnajua saikolojia ya makundi, hatuwezi kuizuia.”
  Ujumbe wa viongozi hao wa dini za Kiislamu na Kikristo waliwakilishwa na ujumbe wa watu 12 ukiongozwa na askofu Paul Ruzoka wa jimbo Kuu Katoliki la Tabora chini ya uratibu wa Peter Maduke, ambaye ni mratibu kamati hiyo.

  Viongozi wengine walioshiriki mazungumzo hayo na Dk Slaa jana ni Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhadi Salum, Sheikh Abdalah Rashid ambaye alimwakilisha Mufti Issa bin Shaban Simba, Sheikh Thabit Norman Jongo aliyemwakilishi Mufti wa Zanzibar na Askofu Thomas Laizer wa KKKT jimbo la Arusha.

  Wengine Askofu Joseph Shao wa jimbo Katoliki Zanzibar, Askofu John Nkola wa Kanisa la Africa Inland Church (Shinyanga), John Mapesa wa Jumuiya ya Kikristo (CCT) Dodoma, Juma Chum (CCK-TC), Padre Daniel Mfowi (Zanzibar), Padre Mbegu kutoka Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC).

  Kabla ya Dk Slaa kueleza mtazamo wake kuhusu mwenendo wa uchaguzi, ujumbe huo ambao unaunda Kamati ya Viongozi wa Dini ya Haki na Amani, ulimtaka Dk Slaa kuzingatia haki, maelewano, mshikamano na amani katika kampeni zake za kuusaka urais.

  “Dhumuni na shabaha ya kuzungukia vyama vya siasa hasa wagombea urais, ni kuwaomba wahakikishe kampeni zao zinazingatia haki, maelewano, mshikamano amani na utulivu,” alisema Askofu Ruzoka.
  Askofu Ruzoka alisema kuwa kamati hiyo imeamua kufikisha ujumbe huo kwa mgombea urais huyo wa Chadema ikiamini utawafikia pia wagombea wote wa ubunge na udiwani wa chama hicho.

  Kwa mujibu wa Askofu Ruzoka, kamati hiyo pia imeviandikia barua vyama vingine vilivyosimamisha wagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao kuviomba viwape fursa ya kuzungumza navyo, lakini hilo litafanyika kama vyama hivyo vitakubali.

  “Ziara yetu imeanzia hapa (Chadema) na kuendelea kwenye vyama vingine kadiri vyama hivyo vitakapotukaribisha,” alisema askofu Ruzoka.

  Kwa mujibu wa askofu Ruzoka tayari kamati hiyo imefanya ziara ya aina hiyo visiwani Zanzibar na kukutana na mgombea urais wa visiwa hivyo kwa tiketi ya CUF, Seif Sharrif Hamad na rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
  Alisema kamati hiyo iliundwa na kuanza kufanya kazi mwaka 2002.

  Kamati hiyo ilikemea kampeni za kuchafuana na zinazogusa maisha binafsi ya wagombea wakisema hazipaswi kupewa nafasi katika mchaguzi huo badala yake vyama vitangaze sera na malengo yake ya kuomba uongozi.
  Kwa mujibu wa kamati hiyo, si sahihi kwa wagombea kuzungumzia maisha binafsi ya watu katika kampeni zao kwani endapo jambo hilo likiachwa, hakuna mgombea atakayekuwa salama.

  “Wagombea waeleze wataifanyia nini nchi hii, wananchi wasikilize sera za vyama. Kila mmoja akiandamwa binafsi kwenye kampeni, hakuna aliye salama," alisema askofu John Nkola.

  Aliendelea kusema: "Mambo binafsi hayana nafasi kwenye kampeni, kinachotakiwa ni sera.”

  Akizungumzia mkutano huo, Dk Slaa alisema amefarijika na ujio wa viongozi hao wa dini aliowaelezea kuwa wamefanya hivyo kutimiza jukumu lao.

  “Nimefarijika kwa viongozi wa dini kuja. Ni jukumu lao kuangalia amani ambayo huko nyuma ilitaka kuvunjika. Tunajua uchaguzi ni wa muda mfupi na amani haiji kutoka mbinguni," alisema Dk Slaa.

  Naye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa waliwaeleza viongozi hao wa dini hofu yao kuhusu mchakato wa uchaguzi na madai yao juu ya jinsi CCM inavyoitumia serikali kuuharibu.
  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,409
  Likes Received: 414,712
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya magazeti mengine hayaelezei vizuri kama Mwananchi.

  Uhuru, Habari leo yanatoa msisitizo kuwa viongozi wa dini waiasa Chadema kukubali matokeo. Kauli inayoashiria ya kuwa viongozi wa dini wanatarajia Chadema itashindwa kwenye uchaguzi huu jambo ambalo hakuna ajuaye.
   
 3. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru sana viongozi wa dini kwa kuchukua hatua hiyo. Hata hivyo wanapaswa kukemea CCM kwa uvunjaji wa sheria za uchaguzi na haki za binadamu katika mchakato wa kampeni za uchaguzi. Kwa sababu wananchi wanaonekana wamechoka CCM, wakifanya maamuzi tofauti, lazima CCM watii na kukubali matokeo!!
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nimeshahamasisha vya kutosha watu waachane na magazeti ya udaku na udakuzi wa habari.
   
 5. d

  david2010 JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ndugu Zangu Watanzania Nasikitiswa na baadhi ya vyombo vya habari au magazeti kwani walichoandika haina Maudhui / Ujumbe uanoeleweka au inawatatanisha watu kwani wanavyosema kuwa'' Chadema Chakubali Matokeo''wanamaanisha kuwa wameshajua kuwa wanashinda au wanashindwa? mimi nilivyosoma habari kupitia Gazeti makini la Mwananchi limeelezea vyema iliyokuwa kwamba viongozi wa dini walimtembelea Dr slaa kwa ajili ya ujumbe wao wa haki katika kampeni mpaka Uchaguzi na Dr aliwashukuru hao watumishi hao pia alitoa maoni yaake kuhusu CCM kama Chama kinachotawala kinavyovunja sheria ya Uchaguzi na ilivyoanzisha vurugu hivyo aliwataka waufikishe ujumbe huo kwa CCM kama ilivyokuwa lengo la Watumishi hao kuwafikia wagombea wote wa urais wa vyama vya siasa vyote. na ujumbe wao wa haki na kudumisha Amani.
  Soma habari hii hapa
  Slaa aichongea CCM kwa viongozi wa dini Send to a friend
  Wednesday, 29 September 2010 18:58
  0
  digg

  Exuper Kachenje
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alikutana na viongozi wa dini na kuwaeleza maoni ya chama chake jinsi CCM ilivyoanza kucheza rafu kwenye mchakato unaoendelea wa uchaguzi mkuu nchini.

  Viongozi hao walimtembelea mgombea huyo wa urais kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema jijini Dar es Salaam na kumueleza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya mpango wao wa kutembelea wagombea urais kwa vyama mbalimbali kwa lengo la kuwafikishia ujumbe wa haki.

  Lakini baada ya kuwasikiliza, Dk Slaa alianza kuvurumusha lalamiko moja baada ya jingine.
  "Nimefarijika kwa viongozi wa dini kuja," alisema mgombea huyo urais kwa tiketi ya Chadema. "Ni jukumu lao kuangalia amani ambayo huko nyuma ilitaka kuvunjika. Tunajua uchaguzi ni wa muda mfupi na amani haiji kutoka mbinguni."

  Dk Slaa, ambaye chama chake kimekuwa kikidai kuwa CCM imekuwa ikicheza rafu dhidi ya Chadema, alianza kueleza mtazamo wake kuhusu mchakato wa uchaguzi.
  "Wameeleza; tumetoa mawazo yetu; haki ikikiukwa zaidi hasa kutokana na CCM inavyofanya sasa, sisi hatutakaa kimya. Haki isipopatikana au isipotendeka na polisi kushindwa kuilinda amani na amani ikatoweka; wa kulaumiwa ni CCM," alisema Dk Slaa.

  Alidai kuwa upo ushahidi wa wazi wa CCM kuvunja Maadili ya Uchaguzi na Sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati chama hicho ndio msimamizi wa mfumo huo kutokana na kuongoza serikali.
  "Tumeeleza kuwa vurugu kwenye uchaguzi huja baada ya matokeo; tumeombwa kuyakubali matokeo baada ya Nec kuyatangaza, lakini tunazo taarifa na waraka tumeunasa kuwa serikali imeagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha chama fulani kinashinda," alisema Dk Slaa.
  Aliongeza kusema: "Ni mwendawazimu kwa mtu kuyakubali matokeo katika uwanja usio sawa. Kwa hiyo viongozi wa dini wachukue jukumu la kuhakikisha uwanja sawa unakuwepo katika kampeni.
  "Tunazo pia taarifa kwamba serikali imetuma timu kuzunguka kuwatisha watu, hata viongozi wa dini kwa madai kuwa wanaunga mkono upinzani, hili halikubaliki. Tulichoahidi tutaelimisha watu kwa kuzingatia wajibu wao na kujua haki zao, lakini wanapochokozwa, ninyi mnajua saikolojia ya makundi, hatuwezi kuizuia."
  Ujumbe wa viongozi hao wa dini za Kiislamu na Kikristo waliwakilishwa na ujumbe wa watu 12 ukiongozwa na askofu Paul Ruzoka wa jimbo Kuu Katoliki la Tabora chini ya uratibu wa Peter Maduke, ambaye ni mratibu kamati hiyo.

  Viongozi wengine walioshiriki mazungumzo hayo na Dk Slaa jana ni Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhadi Salum, Sheikh Abdalah Rashid ambaye alimwakilisha Mufti Issa bin Shaban Simba, Sheikh Thabit Norman Jongo aliyemwakilishi Mufti wa Zanzibar na Askofu Thomas Laizer wa KKKT jimbo la Arusha.

  Wengine Askofu Joseph Shao wa jimbo Katoliki Zanzibar, Askofu John Nkola wa Kanisa la Africa Inland Church (Shinyanga), John Mapesa wa Jumuiya ya Kikristo (CCT) Dodoma, Juma Chum (CCK-TC), Padre Daniel Mfowi (Zanzibar), Padre Mbegu kutoka Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC).

  Kabla ya Dk Slaa kueleza mtazamo wake kuhusu mwenendo wa uchaguzi, ujumbe huo ambao unaunda Kamati ya Viongozi wa Dini ya Haki na Amani, ulimtaka Dk Slaa kuzingatia haki, maelewano, mshikamano na amani katika kampeni zake za kuusaka urais.

  "Dhumuni na shabaha ya kuzungukia vyama vya siasa hasa wagombea urais, ni kuwaomba wahakikishe kampeni zao zinazingatia haki, maelewano, mshikamano amani na utulivu," alisema Askofu Ruzoka.
  Askofu Ruzoka alisema kuwa kamati hiyo imeamua kufikisha ujumbe huo kwa mgombea urais huyo wa Chadema ikiamini utawafikia pia wagombea wote wa ubunge na udiwani wa chama hicho.
  Kwa mujibu wa Askofu Ruzoka, kamati hiyo pia imeviandikia barua vyama vingine vilivyosimamisha wagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao kuviomba viwape fursa ya kuzungumza navyo, lakini hilo litafanyika kama vyama hivyo vitakubali.

  "Ziara yetu imeanzia hapa (Chadema) na kuendelea kwenye vyama vingine kadiri vyama hivyo vitakapotukaribisha," alisema askofu Ruzoka.

  Kwa mujibu wa askofu Ruzoka tayari kamati hiyo imefanya ziara ya aina hiyo visiwani Zanzibar na kukutana na mgombea urais wa visiwa hivyo kwa tiketi ya CUF, Seif Sharrif Hamad na rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
  Alisema kamati hiyo iliundwa na kuanza kufanya kazi mwaka 2002.

  Kamati hiyo ilikemea kampeni za kuchafuana na zinazogusa maisha binafsi ya wagombea wakisema hazipaswi kupewa nafasi katika mchaguzi huo badala yake vyama vitangaze sera na malengo yake ya kuomba uongozi.
  Kwa mujibu wa kamati hiyo, si sahihi kwa wagombea kuzungumzia maisha binafsi ya watu katika kampeni zao kwani endapo jambo hilo likiachwa, hakuna mgombea atakayekuwa salama.

  "Wagombea waeleze wataifanyia nini nchi hii, wananchi wasikilize sera za vyama. Kila mmoja akiandamwa binafsi kwenye kampeni, hakuna aliye salama," alisema askofu John Nkola.
  Aliendelea kusema: "Mambo binafsi hayana nafasi kwenye kampeni, kinachotakiwa ni sera."
  Akizungumzia mkutano huo, Dk Slaa alisema amefarijika na ujio wa viongozi hao wa dini aliowaelezea kuwa wamefanya hivyo kutimiza jukumu lao.

  "Nimefarijika kwa viongozi wa dini kuja. Ni jukumu lao kuangalia amani ambayo huko nyuma ilitaka kuvunjika. Tunajua uchaguzi ni wa muda mfupi na amani haiji kutoka mbinguni," alisema Dk Slaa.
  Naye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa waliwaeleza viongozi hao wa dini hofu yao kuhusu mchakato wa uchaguzi na madai yao juu ya jinsi CCM inavyoitumia serikali kuuharibu.
   
 6. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Sasa upele umepata mkunaji, kifupi ni kwamba CCM kwisha kwani viongozi wa dini lazima watafanyia kazi hawataziacha tAARIFA zipite hivi hivi.Naamini DR.Slaa atakuwa ameongea objectively kwa maana kwamba atakuwa ametoa documentary evidences za nyaraka hizo kwa waheshimiwa wale.Ingawaje amekwisha kataa kuzitoa hadharani.Ndiyo maana Dr.sLAA AMEWAPA NAO ASSIGNMENT KWAMBA''"Nimefarijika kwa viongozi wa dini kuja. Ni jukumu lao kuangalia amani ambayo huko nyuma ilitaka kuvunjika. Tunajua uchaguzi ni wa muda mfupi na amani haiji kutoka mbinguni," alisema Dk Slaa.
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wameniudhi viongozi wa dini wanapokataza maswala binafsi ya wagombea wetu yasijadiliwe. Kwani maswala binafsi ni UZINZI peke yake? Wanataka kuviandika upya vitabu vitakatifu? Nafahamu wengi wetu zile Amri kumi za Mungu tumebakiza chache sana. Hili halituzuii kuwajadili wanaotaka kutuongoza. Viongozi wa dini watusaidie kupata watu SAFI.
   
 8. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu hayaandiki yale unayoyataka kuandikiwa? :becky:
   
 9. e

  emalau JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,177
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  Tatizo viongozi wa dini wamekariri, nilishatoa mada hapa JF ikiwa na kichwa - amani au haki kwanza? badala ya kuweka msisitizo kwenye haki wanasisitiza amani bila kufikiri kwamba amani ni zao la haki. Sasa hivi tunaona jinsi viongozi wanavyoamishwa kama adhabu ya wao kutaka kutenda haki. Huko Arusha kiongozi ameamishwa, hai, moshi na wengine watafuatia. Sasa hawa viongozi wa dini kama sio kasuku ni nini? wasitegemee matunda bora wakati hawajamwagilia maji wala kupalilia. Wimbo wa amani ubadilishwe tuimbe haki kabla ya amani.
   
 10. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Inaa maana wewe ungelipenda haki kwanza kabla ya amani?? Hivi ni haki gani unayoweza kuipata wakati kukiwa hakuna amani? Nitajie mahala pamoja ambako hakuna amani lakini kuna haki.....
   
 11. e

  emalau JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,177
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  Omarilyas, Nina maana kwamba usitegemee amani wakati haitendeki, haki ikitendeka na ikaonekana kwamba inatendeka amani itakuwa ni kitu automatic. Kama Dr. Slaa alivyosema jana kwamba ukubali matokeo ni matokeo ! Think deeply about that since this is the home of great thinkers.
   
 12. e

  emalau JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,177
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  Omarilyas, Nina maana kwamba usitegemee amani wakati haki haitendeki, haki ikitendeka na ikaonekana kwamba inatendeka amani itakuwa ni kitu automatic. Kama Dr. Slaa alivyosema jana kwamba kukubali matokeo ni matokeo ! Think deeply about that since this is the home of great thinkers. Ukiwa baba mwenye nyumba watoto wanakuona unakula nyama choma bar na nyumbani wanakula vidagaa lakini hawakuulizi kitu wanakaa kimya usifikiri hapo nyumbani kuna amani, that is the time bomb It is the matter of wait and see !
   
Loading...