Slaa achaguliwe tu mwaka huu. Cheki contribution yake. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa achaguliwe tu mwaka huu. Cheki contribution yake.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Profesy, Sep 7, 2010.

 1. Profesy

  Profesy Verified User

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135


  .....hapa patamu kweli......!
   
 3. Profesy

  Profesy Verified User

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Au sio Mkuu. Yani watu wanatakiwa waone haya mambo.
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,381
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  watanzania mnasubiri wakati kila takwwimu ziko wazi................mnataka wakati gani zaidi wa lkumpata mgombea makini km slaa?.......chukueni hatua sasa.........this is our golden opportunity let us use it effectively......
   
 5. Profesy

  Profesy Verified User

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wanasema action speaks louder than words na nimeona kwamba Slaa alikua sio anaongea ongea tu. mmemuona ROSTAM na LOWASSA? Hawana ata aibu kujiita wabunge. SAD SAD SAD :confused2:
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,381
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Rostamu na lowasa walikuwa busy na kuandaa mtandao..........sielewi wabunge amabao hawashiriki kabisa kuchangia hoja bungeni wanachukuliwa hatua gani.................hivi hatua gani zinachukuliwa.?
   
 7. S

  Selemani JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kuwa na mgombea makini hakumaanishi mafanikio katika utawala. Ni wale maaskari wa miamvuli na infrastructure of governing ndio vinawezesha utawala bora. Pia, kuwa mtunga sheria na kuwa CEO wa nchi ni vitu tofauti. Also, nini sera za Slaa katika kilimo, afya, viwanda, usafiri--and how are they different from CCM. Haya ndio maswali ya msingi babu.
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  RA,EL na Mwinyi huwa wanakuwa bussy na nini bungeni?
  Alafu posho wanachukua?
   
 9. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145

  Dr. Slaa anastahili achaguliwe kwa juhudi alizoonyesha bungeni na hata katika Jimbo lake la Karatu.

  ______________________________________________
  Pick the flower when it is ready to be picked. - Chinese Proverb
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  Halafu nasikia kwenye kura za maoni Lowassa kapata kwa kura elfu 40.
   
 11. Profesy

  Profesy Verified User

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Cha kwanza wanataka watoe mafisadi ndani ya serikali. Hivi CCM wana agenda yeyote kama hio? ukisha jibu hapo nitakutumia sera za CHadema kwa ujumla.
   
 12. D

  Dopas JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Asante kwa takwimu ya kina. Uwezekano wa kuitoa ccm madarakani mwaka huu upo ikiwa wananchi wataondoa woga wa kufanya uamuzi sahihi siku ya kupiga kura.
   
 13. Profesy

  Profesy Verified User

  #13
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Au watu waende wakapiga kura pia badala ya longolongo
   
 14. C

  Commitment Member

  #14
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakupongeza kwa swali nzuri, soma au pitia katiba ya chadema utaona sera safi na za kutekelezeka.

  Kama kweli u mtanzania mwenye uchungu na nchi yako natumaini utasoma na kujionea tofauti ili uchukue hatua.
   
 15. MAWANI

  MAWANI Member

  #15
  Sep 7, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Dk Willibrod Peter Slaa

  Dk Willibrod Peter SLAA
  1. Anachokisimamia
  • Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, uamakini na uwajibikaji katika uongozi wa nchi na utendaji serikalini.
  • Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti.

  2. Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari
  • Dk Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965.
  • Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung'unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

  3. Mafanikio ya Dk Slaa Kielimu na Kitaaluma
  • Dk Slaa ana shahada na stashahada zifuatazo Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome Stashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari
  • Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari
  • Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho

  4. Mafanikio ya Dk Slaa Kikazi na Kitaalamu
  Dk Slaa amefanya kazi katika maeneo na sehemu mbalimbali. Baadhi ya nyadhifa alizoshika na kazi alizofanya ni hizi zifuatazo:
  • Mkurugenzi Mtendaji, Chama cha Wasioona Tanzania, 1992-1998
  • Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), 1985-1991
  • Mkurugenzi wa Maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu), 1977-1979 na 1982- 1985.
  • Padri wa Kanisa ikatoliki kuanzia 1977 hadi 1991.

  5. Vitabu alivyoandika
  • Utimilifu wa Msichana (1977)
  • Utimilifu wa Mvulana (1977)
  • Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981)

  6. Ufasaha katika lugha nane (8)
  Dk Slaa anajua kuzungumza na kuandika lugha nane za kimataifa zifuatazo:
  Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.

  7. Uzoefu wa Dk Slaa Kisiasa
  Dk Slaa ana uzoefu wa muda mrefu katika shughuli za kisiasa. Baadhi ya nyadhifa
  alizoshika ni hizi zifuatazo:
  • Mbunge wa Karatu kwa miaka 15, kutoka 1995 hadi 2010
  • Katibu Mkuu wa CHADEMA, 2002 hadi sasa
  • Makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, 1998-2002
  • Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu wa CHADEMA kutoka 1995 hadi sasa

  8. Uzoefu wa Dk Slaa Kitaifa na Kimataifa
  • Dk Slaa ana uzoefu mbalimbali kitaifa na kimataifa kama ifuatavyo
  • Mjumbe wa kuwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la Afrika, Carribean na Pacific-EU (ACP-EUC Joint Assembly), 1996-2000
  • Mjumbe Kamati ya Uongozi (ACP-EU Joint Assembly)
  • Mjumbe katika Bunge la SADC kutoka 1998 hadi 2010
  • Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la SADC (Inter Parliamentary Cooperation and Capacity Building Committee) kutoka 1998 hadi 2010
  • Naibu Kiongozi wa Kamati ya Upinzani Bungeni, 2006-2010 na
  • Mwenyekiti, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Bunge la Tanzania, 2008-2010

  9. Mafanikio kisiasa na kiutendaji
  Dk Slaa amekuwa mbunge wa Karatu kwa miaka 15 mfululizo. Karatu ni moja ya
  wilaya hapa nchini zenye mafanikio makubwa ikiwemo miundo mbinu bora, maji
  na huduma nyingine za kijamii. Dr. Slaa anataka kutumia uzoefu wake wa miaka
  15 ya ubunge wa Karatu kwa ajili ya taifa zima.
  Ndiye Katibu Mkuu aliyefanikiwa zaidi kuijenga CHADEMA. Kwa kushirikiana na
  viongozi wengine ameweza kuipitisha CHADEMA katika changamoto mbalimbali
  na kukifanya kuwa chama kilicho tayari kushika uongozi wa taifa.
  Bila kujali vitisho vya watawala aliibua rasmi kashfa za ufisadi mbaya kuliko zote
  zilizowahi kutokea hapa nchini zikihusisha wizi wa fedha za umma katika Benki
  Kuu. Madai yake mazito Bungeni yalimlazimisha aliyekuwa Gavana wa Benki
  Kuu nchini kutoroka nchini.

  10. Baadhi ya vipaumbele vya Serikali itakayoundwa na Dk Slaa
  Kuanzisha mchakato wa kuandika upya Katiba ndani ya siku 100 baada
  ya kuunda serikali
  Kupambana na kuwashughulia mafisadi katika nafasi zote, ikiwa ni
  pamoja na kuhakikisha fedha zote zilizoibwa zinarejeshwa na wahusika
  wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
  Kuhakikisha kuwa kilimo chetu kiwe bora na cha kisasa, chenye faida
  na kinachofikia viwango vya kimataifa katika kuvuna, kuhifadhi, kusafirisha
  na kuuza mazao mbalimbali.
  Kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora katika
  ngazi zote
  Kuanzisha utaratibu wa kuwalipa pensheni wazee wote wenye umri wa
  miaka 60 na kuendelea nchi nzima na kurekebisha mfumo wa malipo ya
  pensheni kwa wastaafu
  Kuanzisha utaratibu mpya wa upandaji mishahara kwa watumishi wa
  umma na wa sekta binafsi utakaohakikisha kuwa mishahara inapanda
  kadri gharama za maisha na mfumuko wa bei unavyopanda.

  Chagua Mabadiliko, Mchague Dk Slaa ili arudishe tunu za taifa letu:
  Uzalendo, Maadili, Uadilifu na Umakini.
   
 16. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Watanzania wangapi wanaingia hapa JF na kuziona hizi Takwimu?

  Any way, unaweza kusema ni almost watanzania 20,000. Je katika hao wangapi ni wapiga kura i.e wamejiandikisha na wanashahada za kupigia kura?

  Lets be realistic.
   
 17. M

  Mnyagundu Senior Member

  #17
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 3, 2008
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mheshimiwa hivi u Dr.wake ni wa kupora wake za watu, du hii ni kali ya mwaka. yeye si Dr. Makombora si angetungua kitu kipyaa????? sasa akina OBAMA wa USA halahala kuja TZ na ma firstlady wenu atakapoingia hekaluni kwani watatunguliwa kwa staili ya B52.
   
 18. Profesy

  Profesy Verified User

  #18
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi unataka tuanze kuongea kuhusu Kikwete hapa? Kua mwizi wa mke wa mtu si kitu ambacho kita affect sera zake wala performance. We sema tu unawasiwasi kwamba sasa hivi watu wameamka. Na nilivyo post hii ni for the sake of performance, mtu gani ni mchapakazi. Nina wakika ata JK alikua apigi kazi bunge kama Dr Slaa (real doctor sio wakupewa kwa maneno).

  Alafu ujue udaku ambayo hauna wakika nao usitangaze kwenye forum kama hii utachekwa mkuu.
   
 19. MAWANI

  MAWANI Member

  #19
  Sep 7, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waht I can Comment is that Slaa ni mchapakazi ukilinganisha na Kikwete. Sasa tukiongea masuala ya binafsi kama ndoa na umalaya hatuna anayeweza kupona; kuanzia kwa JK, kwa makamu, mawaziri wote na wabunge wamepitia hayo. kwa ujumla Jk anaongoza kati ya maraisi waliowahi kuiongoza TZ kwa kuwa mharamia wa small houses incl. wake za watu nje na ndani ya nchi. watu wana data.
   
 20. Profesy

  Profesy Verified User

  #20
  Sep 8, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii kitu tunatakiwa tukiitume kwenye magazeti waonyeshe nani ndio anajalia watanzania kwa ujumla.
   
Loading...