Vipaumbele!! kama vipaumbele vyeti ni kuendelea kuwa soko la bidhaa chakavu kutoka nchi kama hizo unategemea nini? Kama vipaumbele vyetu ni kuwaona wezi kama wapiganaji unategemea nini? Kama vipaumbele vyetu ni kuwanyanyasa walimu, watu wanaosaidia kuondoa ujinga vichwani mwa watoto wetu unategemea nini? Kama vipaumbele vyetu ni kuomba omba kila kukicha unategemea nini? Kama vipaumbele vyetu ni kuzungumzia udini, ukabila na ukanda unategemea nini? Kama vipaumbele vyetu ni umimi na kila aina ya utendaji mbovu bila kuangalia hapo baadae watoto wetu wataishi vipi, unategemea nini?
Vipaumbele vya maana havieleweki kwetu, ni kama tumeshindwa kutumia karama tulizonazo kwa kukosa viongozi wabunifu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.