SKOL na viraka vya barabara vya kichina ni dhulma kwa walipa kodi wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SKOL na viraka vya barabara vya kichina ni dhulma kwa walipa kodi wa Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Songambele, Jun 18, 2012.

 1. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,438
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Ndugu wananchi mie ni mkazi wa Tabata - Segerea, mwisho wa mwaka jana kulikuwa na ukarabati wa barabara kwa kukata vipande vipande na kuweka viraka vya rami. Hata mwaka haujaisha yupo mkandarasi mwingine BECCO anaziba viraka hivyo hivyo kwa style ile ile ya SKOL kutoka Tabata Bima - Mpaka Baracuda.

  Ukilinganisha na SKOL walionekana wamekamilika kwa vifaa na wafanyakazi lakini huyu wa sasa anaoneka yeye anavifaa vichache zaidi. Sina utaalamu wa ukarabati wa barabara lakini mtindo huu wa kuchemsha rami na kuziba viraka unaonekana kabisa ni uharibifu wa pesa za walipa kodi kama wahusika hawatakubali kutoa value for money ni bora wakaacha hayo mashimo mpaka itakapo patikana pesa ya kufanya ukarabati wa maana na hizo pesa zingeenda kuweka rami katika barabara zingine.

  Kwa kuwa hiki ni kipindi cha bajeti wabunge wetu wa Dar tafuteni magnifier lens kujua pesa za ukarabati wa barabara zilitumikaje kwa mwaka uliopita na kwanini SKOL wasirudi tena kutengeneza hii barabara kwa gharama zao kama Magufuli alivyo komaa kwa barabara ya Kilwa?

  Halafu kampuni inanjunga mnaipa kazi nyingine sehemu nyingine na kutegemea majibu tofauti.
   
 2. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu mimi nadhani manispaa za Ilala na Temeke zimezidi kwenye ukandarasi wa kimangu-mashi. Barabara zinakatwa kuwekwa viraka, wanaruka hapa wanatengeneza pale ilmradi wawaachie mashimo na iwe guarantee kurudi tena kutengeneza. Kule Majimatitu Mbagala sijui likampuni lipi limepewa kukarabati rami. Ile barabara nasikia iko chini ya TANROAD inakwenda hadi kuzunguka karibu na Pugu Kajiungeni. Lakini hii ya Mbagala Mwisho hadi kuelekea Chamazi ni usanii mtupu, ilmradi usumbufu kinachotengenezwa hakijulikani
   
 3. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kila kazi za barabara dar wanapewa skol. hii itakuwa kampuni ya riz1 lazima!
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Fuatilieni kwa makini na mtaujua ukweli nyuma ya pazia.
  Kampuni imenunua vifaa vingi sana na mtaji wake haujulikani umetoka wapi.
  Pili hawana wataalam wa barabara, lami waliyojenga miezi sita iliyopita kule Ukonga kuna viraka tayari.
   
 5. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,438
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Basi hakuna hata wa kuwakagua jamani?
   
 6. m

  mmteule JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  kama kipo kitu kinachoniumiza kichwa basi ni utendaji kazi wa hii kampuni ya SKOL kwakweli ni full kichef chefu..... barabara ya bima segerea imekuwa kama tego lao...... tangu mwaka 2002 hadi leo mwaka 2012 wanakula fungu kupitia barabara hii.... roho inaumia sana kuona wanaziba kiraka leo baada ya siku kadhaa kinakuwa handaki wanapewa ulaji tena mchezo umekuwa huohuo kwa miaka kumi sasa... tangu niko mtoto mpaka leo ni mtu mzima nawaona tu. dah kweli hii ndio tzie.
   
 7. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,224
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Wote hao makandarasi ni wasanii tu. Barabara ya Nyerere (kutoka airport kwenda Gongo la mboto) ambayo ilipanuliwa na SKOL mwaka juzi imeanza kuchakaa. Ukifika pale Airwing zilipo ofisi za TTCL tayari lami ishawekwa viraka, hata miaka miwili haijapita.
   
 8. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,171
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hata mie nilishindwa kushangaa kuwaona tena mwaka huu na wakati mwaka jana niliwashuhudia wakifanya same ushuzi
   
 9. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapana, ni ya RA na Riz1. Inasemekana hata CCM wana mgao katika tenda za kampuni hii. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
   
Loading...