Skills (ujuzi) upi ni muhimu kwa vijana kuwa nao kwa kipindi hiki cha hali ngumu?

Mimi mstaarabu

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
258
566
Skills au ujuzi upi ni muhimu kuwa nao kijana wa kitanzania mwenye umri kuanzia 18 na kuendelea labda mwisho35 (awe ana soma au yupo mtaani.)vyovyote vile ilimradi kijana.

Nia na madhumuni ya uzi huu ni kwamba kujulishana skills mbali mbali za kusomea au kujifunza ili kuendelea kupigania maisha yetu ya kila siku.

kama mnavojua kipindi cha miaka ya nyuma maisha yalikuaje na kipindi cha miaka hii ya sasa maisha halivobadilika yani bila ujuzi au kipaji chochote hauwezi kutoboa na kama umesoma basi ajira kama huna connection pia ni changamoto.

skills chache ninazozijua ni hizi ila naomba muongezee na nyingine: kwa vijana wote wakike na wakiume

1. kujua kupika..utafungua restaurant
2: kujua kusuka au kunyoa...utafungua saloon
3: kujua kushona...utashona nguo hata za maharusi
4: kujua makeup...utapamba watu na hata maharusi
5: kujua kuendesha gari...utakua dereva hata wa UBER

Na mengine nitajieni
 
Kujua biashara utafanya lolote kutokana na soko degree ya kitaa inalipa kuliko ya chuo
Kikubwa ijue teknolojia ya computer zaid itakusaidia
 
21st Century Skills ni muhimu kwa yeyote, zaidi kwa Vijana. 21st Century Skills zinaendana sawia na hali mbalimbali za dunia ya sasa na dunia inayojongea.

Kupitia 21st CS tunapata Life and Career Skills, Learning and Innovation Skills, Information, Media and Technology Skills. Kusudio la kufikia 21st CS ni vyema kufahamu misingi ifuatayo Standards and Assessment, Carriculum and Instruction, Professional Environments ambayo ni shina kuu.

Kupitia learning and career skills natarajia kuona vijana (hasa waliofika shule) kuwa na;-

  • Uwezo wa kufikiri kiundani
  • Kutatua tatizo/changamoto
  • Ubunifu na vumbuzi
  • Uwezo wa kuwasiliana
  • Ushirikiano

Baada ya hapa ni vyema kijana akahusika kufahamu masuala ya kidigitali kama;-

  • Information Literacy
  • Media Literacy
  • ICT Literacy

Baada ya haya ni wazi kijana atakuwa amepiga hatua katika Productivity 'Uzalishaji' na Accountability 'Uwajibikaji'.

Ukiwa na uwezo wa kung'amua lugha kadha wa kadha 'Foreigh Languages', Sanaa ya utendaji 'Performing Arts', Fine Arts na Mafunzo ya ufundi 'Vocational Studies' ni wazi hutosindikiza watu katika maisha.

Kikubwa haya yaambatane na ujuzi wa Kiingereza, Hesabu, Sayansi, Maarifa ya Jamii na Sayansi ya Kompyuta.

Zingatia! Hii Mode | Create, Circulate, Connect na Collaborate.
 
FOREX ndio njia halisi ya kupata hela bila kupoteza nguvu za mwili au kuchomwa jua. Muhimu uweze kupambana na tamaa na stress kali za uku, na ukubali kuwekeza hela unayoweza kupoteza.

Mtu mwenye elimu ya Form 6 basi anaweza kusoma Forex na kuielewa. Miezi sita ya kusoma kwa masaa yasiyopungua mawili kila siku inatosha kuanzia.

Ukishaizoea unakuwa kama mzoefu wa kubeti. Hawa wanaobeti huwa naona wanasema Man U ya sasa hivi sio ya kumpiga Chelsea, kwanza fulani leo hayupo. Sasa kwenye Forex ukishazoea miezi kama 15 uko utaanza kuelewa kila tukio duniani lina effect gani kwenye exchange ya pesa. Utazijua Fundamental, Supply and Demand au strategy yoyote unayoielewa sana kupitia demo.

Angalizo: Kama unajua hukujaaliwa uwezo wa akili, uvumilivu na una uroho USIJIPE UGONJWA WA MOYO.
Sio unakuta mtu anataka 'kucheza' Fx ukimuuliza Federal Reserve Bank, Bloomberg, NSE vyote hajui wakati ni vitu vinatakiwa kujulikana kwa mtu yeyote anayesikia habari za kimataifa. Mtu huyohuyo ukimuuliza TK master anakutajia Tuisila Kisinda, basi huyu anafaa kazi nyingine maana kila discipline ina watu wake.
 
Absolutely Chief.

Kuna mambo mazito umeyaweka hapa kama mtu hana six sense organs ni ngumu kukuelewa

Hivyo kwa nukta yako nahisi mjadala ungeishia hapa.

Pia ungetolea ufafanuzi kuhusiana na haya:-

  • Uwezo wa kufikiri kiundani
  • Kutatua tatizo/changamoto
  • Ubunifu na vumbuzi
  • Uwezo wa kuwasiliana
  • Ushirikiano

Haswa kwenye “uwezo wa kufikiri kiundani”

yatakuwa na manufaa snaa
 
Absolutely Chief.

Kuna mambo mazito umeyaweka hapa kama mtu hana six sense organs ni ngumu kukuelewa....
Uwezo wa kufikiri kiundani ‘Critical Thinking’. Tahabia au hulka ya kupenda kufahamu na kuhoji, kushughulisha ubongo, kuchakata mifumo na fikra katika perceptions tofauti (Tafiti). Sio kila kilichoandikwa au kinachosemwa ni sahihi au sio sahihi, isiwe Ndiyo au Hapana.

Kutatua Changamoto ‘Problem Solving’. Tatizo halikuwepo, lipo au limetokea ni namna gani unalitatua?!, Kimbinu, Maarifa or whatever tatua changamoto au tatizo kwa kuwa na mikakati au mifumo wezeshi. Weka jitihada matokeo yatapatikana. Wanauza juisi, sambaza juisi kisasa acha kutumia glasi tumia disposable cups, fikia wengi.

Ubunifu na Vumbuzi ‘Creativity and Innovation’. Kufanya jambo kwa utofauti, kufanya jambo nje ya mipaka au kuanzisha jambo katika mfumo mpya. Unasifika kwa chakula kizuri, ongeza ubunifu fanya delivery. Ni fundi mzuri wa ushonaji! Yes anza kuongeza thamani nguo na uzaa zaidi.

Uwezo wa Kuwasiliana ‘Communication Skills’. Fahamu lugha, fahamu namna ya kupokea na kuwasilisha hoja, tambua wahusika wanaopokea mawasiliano yako. Usionge na government officials as unaongea na mchumba, usionge na billionaire as if unaongea na wacheza singeli! tambua mipaka ya maongezi, tambua hali tofauti wakati wa mawasiliano. Sikiliza zaidi.

Ushirikiano ‘Collaboration’. Ushirikia, Jumuiya, affiliate... Shirikiana katika jambo kupata kitu tofauti au kufika hatua fulani. A - ni mtaalamu wa Sayansi ya Kompyuta, B - ni mtaalamu wa picha mchocheo (Graphics), C - ni mfanyabiashara wa nguo, shirikiana kutengeneza mfumo wa mauzo kimtandao kwa kugawana majukumu.
 
Ahsante kwa uzi huu mujarabu,

Kwa kipindi tulichonacho,Kijana yeyote asisahau ujuzi wa kushawishi,Yaani negotiation Skills.

Ni wengi tunakutana nao,Lakini kwa kiasi gani unaweza kumtoa hatua moja kwenda nyingine ,hilo linabaki kwa alie na ujuzi wa kufanya hivyo pekee.

Hata kama unabiashara,Kama huna uwezo wa kushawishi watu Bado itakua ni kazi Bure na katika kutoka kimaisha.

Ujuzi huu unaweza kujifunza kwa kusoma Vitabu vinavyoelezea namna nzuri ya kuishi na watu,Kufanya miamala,kuzungumza mbele za watu na mfano wake.
 
FOREX ndio njia halisi ya kupata hela bila kupoteza nguvu za mwili au kuchomwa jua. Muhimu uweze kupambana na tamaa na stress kali za uku, na ukubali kuwekeza hela unayoweza kupoteza.

Mtu mwenye elimu ya Form 6 basi anaweza kusoma Forex na kuielewa. Miezi sita ya kusoma kwa masaa yasiyopungua mawili kila siku inatosha kuanzia.

Ukishaizoea unakuwa kama mzoefu wa kubeti. Hawa wanaobeti huwa naona wanasema Man U ya sasa hivi sio ya kumpiga Chelsea, kwanza fulani leo hayupo. Sasa kwenye Forex ukishazoea miezi kama 15 uko utaanza kuelewa kila tukio duniani lina effect gani kwenye exchange ya pesa. Utazijua Fundamental, Supply and Demand au strategy yoyote unayoielewa sana kupitia demo.

Angalizo: Kama unajua hukujaaliwa uwezo wa akili, uvumilivu na una uroho USIJIPE UGONJWA WA MOYO.
Sio unakuta mtu anataka 'kucheza' Fx ukimuuliza Federal Reserve Bank, Bloomberg, NSE vyote hajui wakati ni vitu vinatakiwa kujulikana kwa mtu yeyote anayesikia habari za kimataifa. Mtu huyohuyo ukimuuliza TK master anakutajia Tuisila Kisinda, basi huyu anafaa kazi nyingine maana kila discipline ina watu wake.
Forex hata girls?
 
Forex hata girls?
Haina jinsia. Provided that una akili zinachangamka na huna tamaa, I think wanawake ni watulivu na wako makini zaidi kuliko sie wanaume ila kwa vile mnapenda sana hela sijui itakuwa disadvantage hapa. Usiwe greedy kutaka faida haraka na usitake maisha yako kuyaweka uko, ila inalipa ukijipa elimu.

Hakikisha akili yako haina impurities. Huwezi kuwa shabiki wa Zuchu sijui Kajala, mlevi, mambo mengi kisha ukawa successful uku. Unatakiwa uwe na vitu vichache na uwe na ratiba nzuri sana. Kusoma uku ni kila wakati.
 
Bro, Positively

Forex wewe binafsi imekuingizia TZS ngapi na ulitumia mtaji kiasi gani? Ndani ya muda upi?

Kuweza kushawishi kwamba 'ah oke kumbe Armata anayoeleza ni ushuhuda'.
 
Bro, Positively

Forex wewe binafsi imekuingizia TZS ngapi na ulitumia mtaji kiasi gani? Ndani ya muda upi?

Kuweza kushawishi kwamba 'ah oke kumbe Armata anayoeleza ni ushuhuda'.
Mara ya mwisho kutoa hela ni last week Jumanne nilitoa 200k na chenji. Nilikuwa na test hivo tokea hiyo siku sijatrade mpaka leo ila kesho nitaweka dola 50 kwa ajili ya outing weekend. Sijawahi hesabu jumla nimeweka shingapi na nimetoa shingapi mpaka nikikaa nikajumlisha.

Forex kwangu ni boom la pili. Sio biashara, wala sitafutii maisha huku, natafuta hela ya kuishi mjini wala sijawahi deposit zaidi ya $100. Nikiiva na kuwa na muda wa kutosha ndio niwaze kuweka milioni uko.
 
Ume Tongue Twist sana hizi paragraph mbili kiasi nashindwa kuelewa. By the way! Kimakadrio (Maana hufahamu kiasi ulichoweka) unadhani umetengeneza faida, balance au hasara.

$100 = 231,000
 
Back
Top Bottom