Skendo: Watu watatu wakamatwa wakifanya biashara ya kusafirisha watu hai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Skendo: Watu watatu wakamatwa wakifanya biashara ya kusafirisha watu hai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Jul 26, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]
  [h=3][/h]POLISI mkoani Kigoma inawashikilia watu watatu wakiwemo wafanyakazi wawili wa basi la Osaka linalofanya safari kati ya Kigoma na Dar es Salaam, wakituhumiwa kufanya biashara haramu ya kusafirisha watu hai.


  Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Fraiser Kashai aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kwamba juzi saa 10 jioni askari wa upelelezi wakiwa katika doria, waliona basi la abiria katika kijiji cha Heru Juu wilayani Kasulu likikusanya watu kwa ajili ya kuwasafirisha.


  Alisema katika kufuatilia hayo askari hao wa upelelezi waligundua basi hilo lilifika kijijini hapo kwa ajili ya kuwachukua abiria 44 ambao walikuwa katika mpango wa kuwasafirisha kuwapeleka Msumbiji kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za kukata mbao.


  KWA HABARI KAMILI BOFTA HAPA GUMZO LA JIJI
   
Loading...