Skendo la Ununuzi wa Rada ya Tanzania Laingia Hatua Nyingine Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Skendo la Ununuzi wa Rada ya Tanzania Laingia Hatua Nyingine Uingereza

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Sep 12, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wakala wa ununuzi wa rada ya Tanzania, Shailesh Vithlani Tuesday, September 08, 2009 9:27 AM
  Skendo la ununuzi wa rada ya ulinzi ya Tanzania toka kwa kampuni ya BAE Systems ya Uingereza imechukua sura nyingine nchini Uingereza baada ya BAE kupewa mwezi mmoja kukiri kosa lake na kulipa faini na kesi hiyo iishe au kufikishwa mahakamani. Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza imeipa mwezi mmoja kampuni ya Uingereza ya BAE Systems ambayo iliiuzia Tanzania rada ya kijeshi, kukiri kosa lake au kufikishwa mahakamani

  Ununuzi wa rada hiyo uligubikwa na rushwa kubwa na taifa la Tanzania liliuziwa rada hiyo kwa mamilioni ya dola zaidi ya bei halisi ya rada hiyo.

  Mbali na rushwa kutumika katika ununuzi wa rada ya Tanzania, BAE pia inatuhumiwa kutumia rushwa katika kukamilisha uuzaji wa ndege moja ya kijeshi kuiuzia nchi ya Afrika Kusini na uuzaji wa ndege nyingine ya kijeshi ambao haukufanikiwa kwa Jamhuri ya Cheki.

  Kutokana na skendo hilo SFO imeipa mwezi mmoja BAE kukiri makosa yake ya kutumia rushwa kufanikisha madili yake na kulipa faini ya mamilioni ya paundi na baada ya hapo kurekebisha mienendo yake.

  Kama BAE itashindwa kufanya hivyo basi itachukuliwa hatua zaidi za kisheria na itapandishwa kizimbani. Hata hivyo hatua hizo za kisheria zitakuwa dhidi ya kampuni ya BAE na si viongozi wa kampuni hiyo.

  Awali SFO iligundua kuwa mkataba wa ununuzi wa rada wa mwaka 1999, kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uingereza ya BAE Systems uligubikwa na rushwa kubwa.

  Ununuzi wa rada hiyo ulifanikishwa na wakala Shailesh Vithlani ambaye aliifanya Tanzania itoe TSh bilioni 16 zaidi ya bei halisi katika ununuzi wa rada hiyo.

  Vithlani inasemekana alipewa dola milioni 12 (zaidi ya TSh. bilioni 12) kama kamisheni ya kufanikisha dili hilo na inasemekana aligawana pesa hizo na maafisa saba wa ngazi za juu katika serikali ya Tanzania.

  Vithlani alitoroka Tanzania miaka mitatu iliyopita akiwa nje kwa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka na alikamatwa mwaka huu nchini Uswizi alikokuwa akijificha.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3028890&&Cat=1
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Tafadhali naomba kuelimishwa, kwa kampuni hii kupigwa faini inamaana hawa mafisadi wetu chenge, rashid na huyu mhindi wa vodacom [ somaia]ndio wamesave au vipi?
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Ndugu bulesi hii ni nchi ya ajabu sana Duniani, wakati waingereza wapo bize na hii kesi, huku kwetu hao jamaa wanapeta kama kawaida na wanaendelea na issue zao bila kuwa na hofu yoyote
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kituko, hapo umenena! Hivi ndivyo vituko vya Bongo Darisalam. Siyo tu kwamba wahusika wanacheka bali wengine wanapewa vyeo na ulaji zaidi. Mfano Chenge alipewa ujumbe wa kamati ya maadili ya chama (ethics committee) baada ya kuthibitishwa pasipo shaka yoyote kuwa alichukua change ya kutosha na kugawana vijisneti kidogo na wanzake. Labda hiyo kama iitwe ya kupambana na maadili (anti-ethics committee of CCM). Pia Idrisa anaendelea kutesa na kututesa na Tanesco. Lakini mbaya zaidi ni kuwa mkuu wa nchi yuko "very happy" hadi anatoa meno yote 32 kwenye luninga inayotazamwa na wananchi wanaoozeana kuwa umasikini. Kweli masikini ni maiti anayepumua na kutembea!
   
Loading...