Siyoi Sumari na Nassari wawekeana pingamizi ubunge Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siyoi Sumari na Nassari wawekeana pingamizi ubunge Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mwanajamii, Mar 9, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wagombea Wa CCM na CHADEMA Wawekeana Pingamizi Ubunge Arumeru Mashariki
  Taarifa za hivi kutoka Arumeru Mashariki jioni hii zinasema vyama vya siasa CCM na CHADEMA vimewekeana mapingamizi kwa wagombea wao.

  CCM kimemuwekea pingamizi mgombea wa CHADEMA katika Jimbo la Arumeru Mashariki kwa madai ya umri na, CHADEMA kimemwekea pingamizi mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Sioi Sumari kwa madai kwamba si raia wa Tanzania, na tuhuma nyingine za rushwa.

  Kwa mujibu wa habari hizo, CHADEMA wamedai kupata barua ya siri yenye Kumb/ No AR/C/32/VOL1/85, ya Feb 29/2/2012, kutoka kwa Ofisa Mfawidhi wa Uhamiaji mkoa wa Arusha, kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ikifafanua uraia wa Sioi.

  Vyanzo vya taarifa vinadai CHADEMA imenasa barua ya siri yenye Kumb No.AR/C/32/VOL1/85,ya Feb 29/2/2012,kutoka kwa Afisa Mfawidhi wa uhamiaji mkoa wa Arusha,kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha,ikifafanua uraia wa Sioyi,na katika ufafanuzi huo Ofisi ya uhamiaji inakiri kuwa kwa yeyote aliyezaliwa nje ya nchi,ukomo wa uraia wake ni pale anapofikisha miaka 18,na baada ya hapo anapaswa kuukana uraia wa nchi alipozaliwa.

  Kwa tafsiri ya haraka ni kwamba CHADEMA inaweka pingamizi kwamba kwa kuwa Sioi Sumari alizaliwa Kenya, na kuwahi hakuwahi kuomba uraia wa Tanzania, basi si raia wa Tanzania kwa mujibu wa ufafanuzi wa ofisi ya uhamiaji. Na CCM imemuwekea pingamizi mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari kwa hoja ya umri.

  www.tzforums.com
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Pingamizi la chadema kwa siyoi lipo sahihi na lile la ccm dhidi ya nasari halina mashiko,kama vp Felix mkosamali,godbless lema na ernest david silinde wasingekuwa wabunge
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kuwa Nassari ana umri mkubwa sana kugombea au..hapo haijafafanuliwa vizuri.
   
 4. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  JF leo kuna porojo nyingi. au ndo mnataka tusahau kuhusu mgomo mahospitalini?
   
 5. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Joshua Nassari alizaliwa 1985 na aligombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA 2010 akiwa na umri wa miaka 25. Kwa nini CCM wanafadhaika? Katiba yetu na Sheria ya Uchaguzi vinatamka Mbunge awe na umri usiopungua miaka 21.

  Siyoi Sumari angeomba uraia wa Tanzania na kukana uraia wake wa Kenya alipofikia umri wa miaka 18 hangekuwa na tatizo leo.

  NEC should disqualify him for irregularity in his citizenship. We should have Nassari and the other candidates from the other political parties.
   
 6. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Feedback ni hivi eti nassari mdogo.kuna mtu alipata kusema viongozi wa ccm ktk chaguzi huwa wanaweka akili zao timamu pembeni na kuvaa zile za ki-bakwata
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hili la umri halijawekwa sawa, ni mdogo au mkubwa sana, au amedanganya. More info is needed.
   
 8. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijaelewa pingamizi la umri kivipi mkubwa, amedanganya umri au nini? Hii kitu haipo sawa.
   
 9. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Niliwaambia Mwigulu kaleta vielelezo mkabisha na mtaona mengi mwaka huu,hiyo barua si ilikuwa katika kikao cha sekretariet uliza imefikaje Chadema, piiiipoooooozzzz
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Jamani eeee! Mbona hili pingamizi alilowekewa Nassary limekaa ki-bakwata fulan hivi.
   
 11. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  tunamwomba mgombea wetu NASSARI atueleze amewekewa pigamizi la umri kivipi?
   
 12. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sijaelewa kuhusu joshua mleta uzi hebu njoo utoe ufafanuzi
   
 13. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Niliwaambia Mwigulu kaleta vielelezo mkabisha na mtaona mengi mwaka huu,hiyo barua si ilikuwa katika kikao cha sekretariet uliza imefikaje Chadema, piiiipoooooozzzz
   
 14. a

  alpha5 JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  hiyo imekaa vizuri ama sheria za uchaguzi zitafwatwa vizuri basi SIOI lazima ile kwake,
   
 15. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kama suala ni umri hilo si tatizo labda kama amedanganya
   
 16. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Na itakula pia kwa magamba si kidogo,kwa furaha nlonayo ngoja nipite bondeni arachuga nipate rumbesa ya veve njilie raha zangu
   
 17. J

  Juma Bundala Member

  #17
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sheria zetu hazikubali waongo na watoa rushwa hivyo basi Sioyi kama amedanganya kuwa ni raia na kuna ushaidi kuwa ametoa rushwa achukuliwe hatua mara mmoja kwa hiyo CDM wapo sawa,lakini pingamizi la CCM dhidi ya CDM ni wivi tu umri wa kuwa MBUNGE ni kuanzia miaka 21,jamani Joshua hajafikisha hiyo miaka?
   
Loading...