Siyo Viburi; Ukweli ni kwamba watoto wetu ni kizazi dhaifu; tuwahurumie wanapogoma kupisha wakubwa siti za daladala

Ikiwa nyote mnalipa nauli sawa sawa unategemea upishwe ukae? Sasa kama watoto wa siku hizi wapo legelege basi wawaachie hao watu wazima walio strong kusimama tu. Yaani nimekuona kwenye mwendokasi nimelipa sawa na wewe sababu upo 50s na nipo 20s nikupishe?? Utasimama tu mzee mla ugari na makande.

Ndukiiiii ‍♂️‍♂️‍♂️

Kua uyaone...unalomtendea mwenzako nawe utatendewa the same
 
Ukiona gari imejaa usipande, mfano mie natoka Posta mpaka kariakoo kwa mguu na nalipa nauli mara mbili nizunguke na gari ili tu nikae kwenye siti halafu atokee mzembe mmoja tu apandie mnazi mmoja kiboss alipe jero eti nijikute nampisha tu kisa kaenda age. Let a spade be a spade not a big spoon!

Huo utoto sifanyi!!!
 
Nilishasema kuna vitu ikiwa mtu ataamua kuniona ni mtovu wa nidhamu wacha iwe tu, Potelea Pote. Unamkuta mmama au mdada na mtoto saa mbili au moja jioni ana mtoto halafu katoka kusalimia tu ndugu, hapo anajua kabisa kawaida ya mida hiyo inavyokuwa hapo anataka apishwe akae sababu ana mtoto

Unakita mtu mzima kias au mzee nae anakomaa kusulubiwa kisha anaangalia waliokaa kwa huruma. Ifike mahali tuache utamaduni huu wa kipumbavu. Kama unajiona umri umekwenda au upo katika hali isiyomudu kusimama, mara zote wahi kutoka uliko ufike nyumbani mapema, vinginevyo tusisumbuane.
 
Huko ulaya unapotolea mfano wazee wanawapisha vijana wakae kwenye matreni..
 
Kuku wa kisasa

Watoto wanachomwa chanjo zaidi ya Tisa(9) hadi kwa magonjwa yasiyokuwepo, tena kwa lazima
hivi kweli jamani kwa hali hii kuna kizazi mbeleni?.....
 
Kuku wa kisasa

Watoto wanachomwa chanjo zaidi ya Tisa(9) hadi kwa magonjwa yasiyokuwepo, tena kwa lazima
hivi kweli jamani kwa hali hii kuna kizazi mbeleni?.....
ndo maisha ya sasa
 
Kama umekuwa ukitumia daladala au Mwendokasi kwanamna zinavyojaa hata ukisogeza mguu huna pakuuweka huwezi pata mawazo ya kupisha.

Mwendokasi hata siti za wazee,preg women,walemavu hawapati nafasi.

Daladala za kawaida nazo zinajaa sana na foleni juu inachosha zaidi.

Nawatetea watoto hasa wa shule hasa Dsm,wanawahi sana Shule na asilimia kubwa kwenye gari wanakuwa wamesinzia kwa kuchoka.....ukijua adha ya usafiri Dsm huwezi kumlaumu yeyote ila utawaza upambane upate usafiri wako
 
Ikiwa nyote mnalipa nauli sawa sawa unategemea upishwe ukae? Sasa kama watoto wa siku hizi wapo legelege basi wawaachie hao watu wazima walio strong kusimama tu. Yaani nimekuona kwenye mwendokasi nimelipa sawa na wewe sababu upo 50s na nipo 20s nikupishe?? Utasimama tu mzee mla ugari na makande.

Ndukiiiii ‍♂️‍♂️‍♂️
Kiukwel hua nawapisha wajawazito,mgonjwa anaeonekna kbsa kusimama hataweza na wenye watoto wachanga tu....haya makund mengine watanisamehe tu
 
Back
Top Bottom