Siyo siri wanawake tunawatesa kila jambo tunataka wao wawe chini sisi tuwe juu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siyo siri wanawake tunawatesa kila jambo tunataka wao wawe chini sisi tuwe juu!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Gosbertgoodluck, Mar 8, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Leo nataka niwaunge mkono wanawake katika harakati zao za kujikomboa na mfumo dume. Hivi kwa nini wanaume tunapenda kuwa juu kwa kila jambo?? Ni juu juu juu tu kila jambo. Mmhhh, siyo fair jamani inafika mahali wanachoka. Ebu tuwape nafasi na wenzetu.
   
 2. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Muumba wetu ndio alietuweka wanaume juu....... Mwanaume utakula kwa jasho, mwanamke atazaa kwa uchungu....... FYI, biblia inakuambia Adam na Hawa walizaa watoto watatu, wote ni vidume - unafikiri hiyo couple haikuwa na watoto wa kike? Walikuwepo lkn hata Bible haimtambui mwanamke....... But things are fastly changing...... Tanzania tu ktk kila nyanja - si sawa three decades ago...... Wanawake hawatakiwi kupewa nafasi - nafasi zipo tayari, wanatakiwa kutumia fursa zilizopo km wanaume tunavyozitumia as we as men our thinking and attitudes towards women has really changed.......
   
 3. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  hata maandiko ya Mungu yanasema Mwanaume ni kichwa cha familia/nyumba. tusiende kinyume na maandiko ya Mungu.
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  well said
   
 5. m

  muhanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mmmh nani kakwambia sie tuko chini na nyie mko juu!!!???? msipotoshe maandiko jamani, kilichotajwa kwenye bible ni kuwa mwanamume aliumbwa kwanza na kutoka kwake Mungu akaumba mwanamke, lakini the same bible inasema mwanamke alikuwa mwerevu kuliko mwanamume hata akamrubuni wale tunda la mti, kuwa kichwa cha nyumba doesnt mean kuwa wewe uko juu ya mume, msichukulie mfano wa binadamu kasimama basi kichwa kiko juu ya mwili eti ndio kikubwa kuliko moyo ambao anytime ukiacha kufanya kazi hata kichwa hakiwezi kusimama tena, MWANAMKE NI MOYO wa familia, sasa kichwa bila moyo kinawezaje kuishi???? hujawahi kusikia mtu anakuwa declared kuwa is clinically dead kwa sababu ubongo wake ulioko KICHWANI haufanyi kazi lakini amri ya mwisho ya maisha ya mtu ni pale MOYO unapozima kufanya kazi na sio KICHWA! THINK again utagundua behind every successful man there is a woman ' a strong and brave woman for that matter' BIG UP WANAWAKE WOOOOOTE popote mlipo, mko juuu hata shetani analijua hilo!!!!!!!!!!!!
   
 6. V

  Vumbi Senior Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni kweli wanume tumepewa nafasi ya kuwa kichwa cha nyumba lakini je tuna wajibika kwa nafsi hiyo? wanawake wanafanya kazi kuliko wanaume hasa katika mataifa masikini hebu angalia wanawake wanavyofanya kazi vijijini mfano kulima, kupika, kutunza watoto, kuteka maji, kupeleka watoto hosipitali etc sehemu kubwa ya majukumu yetu tumewabebesha wao na ndio maana katika mataifa yaliyo endelea majukumu ndani ya familia ni 50% by 50% ili kupunguza mzigo kwa mwanamke. Nawashukuru sana wazazi wangu kwa kunilea katika makuzi ya kuwathamini wanawake leo hii na mke na amekuwa ni mchango mkubwa sana wa mafanikio ya maisha yangu. Nawapenda sana wanawake mungu azidi kuwapa hekima ili mjenge familia bora.
   
 7. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
   
 8. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45

  hili swala la 50% 50% kwa wanaume na wanawake siyo sahii.. itafika siku watadai na wanaume wabede mimba na jinsi technologia inavyokuwa litawezekana na hapo ndio tutakuwa tumeutafuta mwisho wa dunian wenyewe.
   
 9. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Tatizo wakipewa hizo nafasi wanaharibu, reference " MKUU WA MJENGONI"
   
 10. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,017
  Likes Received: 3,202
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa,,,au unazungumzia kifo cha mende?
   
 11. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  kifo chamende walishatupindua siku hizi wanakuwa juu
   
 12. n

  ngoko JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  eehhh kumbe kuna utata kwenye subject !!! nitarudi baadaye ku comment
   
 13. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu aliyekuumba ndo alivopanga!!!! :A S 13: Ila wewe kama unahoji uhalali wa muumba wako kupanga alivopanga ..........
   
 14. B

  Buke Senior Member

  #14
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Hapo sasa, ninapochoka mimi ni pale inapofikia suala la mwanamke kutakiwa kutimiza majukumu yanayomhusu mwanaume kisa tu ana kipato kikubwa! Kusaidiana ni mapenzi na makubaliano ya wawili. Asante Dr. kwa kutupunguzia lawama.
   
 15. B

  Buke Senior Member

  #15
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu kwa kuliona hilo.
  Pamoja na jitihada zote zinazofanywa ili kutupa nafasi katika nyanja mbalimbali za kukabiliana na maisha, bado tunahitaji sana support ya mwanaume, na mwanaume pia anahitaji support ya m/mke. Lakini hili lisimfanye mwanaume asahau wajibu wake.
   
 16. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkitaka usawa uwe usawa kweli kweli sio kwenye kupendelewa, kuna siku mtu kauliza kwa nini mwanaume anampa pesa mwanamke na hali na yeye anafanya kazi, wanawake wengi walisema lazima watupe maana wenyewe ndio vichwa vya nyumba sasa usawa huu mnautaka wapi mimi huwa sielewi. Ni mambo yepi haswa ambayo mnataka? Harafu for your information nyumba ambayo haina mfumo dume hata kidogo inaboa, maana huwezi kunidekea baadae, mambo ni usawa tu. Mwanamke mtamu ni yule mwenye woga na mnyenyekevu lakini yule mkavu du kama vile una dume lingine.

  kwaherini
   
 17. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  well said mkuu!

  napenda kurefar zaidi katika maandiko matakatifu, maandiko yanasema mwanaume ampende mkewe na mwanamke amheshimu mumewe kunatofauti kubwa sana kati ya kupendwa na kuheshimiwa....... heshima mbele

  nawashauri wakina dada msitake kutafuta usawa ambao haupo utawatesa
   
 18. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Heee! Kumbe hata kwenye suala la nonino tunakuwaga juuu!! Mmhh watu kwa kufikiria broadly! Sasa kama ndivyo basi jamani wanaume tumezidisha. Ebu tuwaachie nafasi nao wapumue sasa
   
 19. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna wakati tuna kuwa chini ila hatusemi
   
 20. M

  Mary Chuwa Senior Member

  #20
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa katika Maandiko imeandikwa kama mlivyonukuu wapendwa mliotangulia lakini katika Kitabu cha Mwanzo ni kuwa Mungu alimuumba msaidizi wa kufanana naye na si kijakazi kama ilivyo sasa,na zaidi na baada ya Mungu kuona kuwa kuna kilichopungua na umuhimu wa mwanamke ndiyo akafanya hivyo hivyo sisi wanawake tuna nafasi kubwa sana na si dhaifu kwani Biblia hiyo hiyo inasema
  'Bwana ameumba jambo jipya duniani mwanamke atakuwa mlinzi wa mwanaume"
  ni jukumu ambalo tunalo kwa wanaume ndiyo maana hatulemai katika suala la kujali familia.
  Kwa kufikiria tu kawaida wanaume wengi wamekuwa wanakwepa majukumu ya familia zao sana,na je ukijiuliza Adamu alikuwa wapi mpaka mkewe akadanganywa? ndiyo hayo tunayaona katika maisha ya kila siku wanaume wengi kutokuwepo pamoja na wake zao hivyo wajifunze kupitia baba Adamu na kuwepo karibu na wake zao.
  Suala la usawa hapa siyo la jinsi bali la jinsia ambayo imejengwa na mazingira ya tunayoishi,taratibu,mila na desturi ambazo kila kukicha kunakuwa na mabadiliko.
  Soma kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo kwa wale Wakristo hakuna sehemu Mungu aliainisha kazi tunazofanya kuwa ni za kiume au za kike,bali ni sisi tulifanya hivyo wanadamu.
  Suala la heshima ndiyo wanawake tuwaheshimu waume zetu,heshima haitasimama peke yake kama huna upendo ndani yake,na unatii yale yenye Utukufu kwa Mungu
  Kwa wamama Mithali 11:16a inasema
  "Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima"hivyo ukiheshimu nawe utaheshimiwa.
  Suala la Upendo wanaume wawapende wake zao kama Kristo alivyolipenda kanisa nahata kulifia,Upendo wa kweli hauhesabu mabaya,hukupa kusamehe na siyo kulipiza kisasi je ni wanaume wangapi hufanya hivyo au mboga ikiungua kidogo amani imetoweka ndani ya nyumba.
  Kila mtu asimame kwenye nafasi yake na siyo kuwa tunadai usawa ambao kwa tafsiri za wengi umepotoshwa aidha kwa matendo ya baadhi ya wanawake au wanaume wasiotaka wanawake waweze kufaidi mema ya nchi kama viumbe tulioumbwa sawa
  Mbarikiwe
   
Loading...