Siyo sahihi utangaze hali ya hatari Mh.Rais ?

Chifu Ihunyo

Member
Jul 3, 2006
63
10
Umeme wazidi kuleta kilio
Serikali huenda ikakopa fedha BoT
Noti mpya kuchapishwa
Mfumuko wa bei kuongezeka
Maumivu mtindo mmoja


na Mwandishi Wetu


SERIKALI huenda ikalazimika kuchukua fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa ajili ya kuiwezesha kufanya mambo mbalimbali, ikiwamo kulipa mishahara ya watumishi wake kwa mwezi huu, imefahamika.


Hatua hiyo inatokana na kutarajiwa kushuka kwa kiasi kikubwa kwa mapato ya serikali mwezi huu, kulikosababishwa na kuongezeka kwa makali ya mgawo wa umeme.


Vyanzo vya habari vya gazeti hili vimebainisha kwamba, kwa vyovyote vile, mapato ya serikali kwa mwezi huu hayatafikia sh bilioni 225.6 zilizokusanywa Juni mwaka huu.


“Viwanda havizalishi kama kawaida na hii maana yake ni kwamba hata kodi itakuwa kidogo. Kama kodi ni kidogo maana yake serikali itakuwa na fedha kidogo kulinganisha na mahitaji yake,” alisema mchumi mmoja aliyezungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki.


Hata hivyo, mchumi huyo aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema hatua hiyo ya kuchukua fedha BoT inaweza kuwa na athari mbaya kwa Watanzania wenye kipato cha chini.


“Kwa vyovyote vile, serikali haiwezi kukubali mwezi upite bila ya kuwapa watumishi wake mishahara katika kipindi hiki ambapo hali ya maisha kwa Watanzania ni ngumu.


“Itakachofanya..., na inaruhusiwa kisheria, ni kwenda kuchukua fedha BoT ambayo ndiyo kimbilio lake wakati mazingira ya namna hii yanapojitokeza.


“Tatizo lililopo hapo ni kwamba BoT inaweza kulazimika kuchapa fedha nyingi zaidi na kuziingiza kwenye soko ili kufidia pengo hilo lililoletwa na serikali.


“Ikifikia hapo, ninawaonea huruma wananchi kwa vile ni lazima mfumuko wa bei uje. Sasa hivi tu hali ni ngumu, na huo mfumuko ndiyo itakuwaje?” alihoji.


Kwa kipindi cha wiki mbili sasa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetanua makali ya mgawo wake ambao sasa maeneo yote nchini yanayopata umeme kupitia gridi ya taifa, hayapati umeme kwa saa 12 kila siku.


Kwa sehemu kubwa, mapato ya serikali hutegemea sana kodi inayokusanywa kutoka kwa wafanyabiashara na wenye viwanda ambao mgawo huo umewaathiri kwa kiasi kikubwa.


Tayari baadhi ya viwanda nchini vimetangaza kupunguza kazi wafanyakazi wake katika kile kinachodaiwa kupunguza matumizi kwa vile hakuna kazi inayofanyika.


Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, idadi ya Watanzania wanaofanya kazi mbalimbali inakadiriwa kufikia milioni 17, kati yao ni milioni moja tu walioajiriwa.


Mgawo huu, unamaanisha kwamba watu milioni 16 walio katika sekta binafsi, ukiondoa wakulima, wameathiriwa moja kwa moja na mgawo huo.


Watu hao wanafanya kazi viwandani, kwenye sekta ya watoa huduma, ujenzi, saluni, masuala ya barafu kama wauza samaki, nyama, maji pamoja na internet café.
 
Back
Top Bottom