SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,121
- 7,877
Siyo sahihi kumuweka mtu mahabusu kwa kisingizio cha usalama wake
Nimeona hii trend mpya kwa mahakama kumrudisha mtu rumande kwa kisingizio cha usalama wake mwenyewe. Eti kwamba wakimuachia huru anaweza kudhuriwa na wabaya wake!
Hili sidhani kama ni sahihi kabisa kwa sababu serikali ina uwezo na inatakiwa kutoa ulinzi kwa mtu yoyote aliye victim, hasa kama mtu huyo ni muathirika kwa mambo muhimu ya kisheria na kikatiba kama 'uhuru wa kuongea' na haki nyingine za msingi za binadamu. Kama serikali na vyombo vya dola vinashindwa kulinda watu wa namna hiyo, ina maana kuwa umma kwa ujumla haupo salama na hakuna chombo cha dola kiko tayari kusimamia katiba ya nchi, kitu ambacho ni hatari sana.
Hivi serikali kweli haina uwezo huo au hii inatumika tu kama sababu ya kukomoa watu? Hivi serikali haina safe houses (nyumba za siri zilizo salama mfano kwa mashahidi muhimu)? Na wanapokuwa huko jela wanapodai ndiyo salama zaidi kwao, wanakuwa wametenganishwa na wafungwa wengine?
Tuliwezaje kuwaweka watu kama Aboud Jumbe katika ulinzi kwa miaka mingi tushindwe kumlinda mtu kama Joseph Mbilinyi 'Sugu', ambaye hana hata maadui, isipokuwa wale ambao wangeweza kumpata hata huko huko jela? Serikali inashindwaje kumlinda mtu kama Abdul Nondo huku akiwa anaendelea na masomo yake wakati kesi yake inaendelea kusikilizwa? Nakumbuka kuna mwanasiasa zamani enzi za Nyerere alirudishwa kijijini kwao na akazuiwa kabisa kutoka, huyo alilindwaje?
Hili jambo haliingii akilini na ningeomba kwa ujumla wetu tulikemee. Tukiliacha hili, watu watakuwa wanatupwa jela waozee huko huku kisingizio kikiwa 'upelelezi na kesi bado unaendelea na hatuwezi kumuachia kwa usalama wake mwenyewe'.