Siyo kweli kwamba Zitto na Makamba wanawahurumia watanzania, wana ajenda zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siyo kweli kwamba Zitto na Makamba wanawahurumia watanzania, wana ajenda zao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theophilius, Feb 1, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Si kweli kwamba lengo la Januari makamba na zito kabwe kuhusu hoja zao binafsi wanazotajia kutoa bungeni ni kutokana na huruma yao kwa watanzania… kama ambavyo wao na wapambe wao wanavyotaka ionekane bali wanataka ku- divert attention ya watanzania kutoka kwenye masuala muhimu yanayogusa maisha na ustawi wa taifa.

  Hii haina maana kwamba hoja hizo si za muhimu! La; lakini ikilinganiswa na masuala kama vile mabadiliko ya sheria ya maandalizi ya katiba mpya, sula la ufisadi, hususani lile la Jairo na wenzake, sula la bei ya umeme, na ufisadi wa EPA, Richmondo/Dowans n.k, hoja za wapangaji, mkonge na huduma za kibenki zinaweza kusubiri au kufanyiwa kazi kwa njia zingine ikiwa kweli wana nia na lengo la kuboresha maeneo hayo.

  Hii ni strategic plan ya ‘Mafia'(soma mafisadi) wa Tanzania waliojaa serikalini ambao wanaona kila siku zinaibuka hoja zinazowatishia amani, wameamua kuwatumia hawa vijana, ili waingize hoja ambazo wanadhani zitameza hoja za msingi ambazo watanzania wamechoka kusubiri ufumbuzi wake kutoka serikalini.

  Ili vyombo vya habari na bunge watumie ‘air time' ya kutosha kujadili hoja hizo at the expense ya hoja za msingi zaidi zinazotakiwa kupewa kipaumbele.

  Nawasihi wanaharakati, wapambambanaji, na wote wanaoitakia mema taifa hili, wasipoteze muda kwenye hoja hizi, na niseme tu sina imani na hawa watu kutokana na wanaowazunguka na mienendo yao huko nyuma, sina shaka kwamba hata hoja hizi zikipita, sheria ikatungwa kukabiliana na masuala hayo, hali itabadilika- uongozi wetu upekuwepo na unaona jinsi kilimo cha mkonge kinavyokufa hawafanyi lolote, Zito atawapa nini wazinduke na kufanya yanayotakiwa kufanywa ili kuendeleza zao hilo,

  Labda cha msingi wangekuwa wanapendekeza tuwaondoe madarakani viongozi na serikali ambayo haionekani kufanya lolote, wakati kilimo cha mkonge kinakufa, au haichukui hatua yoyote kukomesha unyonyaji wa wenye nyumba na mabenki na vyombo vya fedha.

  Maana siyo kwamba hizo ni hoja mpya zimejadiliwa vya kutosha na watu mbalimbali, na tafiti mbalimbali zimefanywa kwa gharama za kodi ya wananchi lakini serikali hii na viongozi hawa hawa wanaopelekewa hoja hizihizi na zito na januari, hawakufanya lolote, wako bisy na mambo yao ya kukwapua rasilimali za umma.
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  makamba ni mzalendo kuliko zitto
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  theophillius , kinachokusumbua ni uelewa mdogo na kutumika bila kujua, huna hoja sasa hivi hatutaki SIASA za akina jairo, ricmond nk ambazo mara nyingi ni kupoteza muda, tunataka wabunge waje na hoja za kutatua matatizo ya msingi ya watanzania kama anavyofanya ZITTO na MAKAMBA, ningekuwa mod. ningekuban kama MS
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kwako si muhimu lakini kwa wengine ni muhimu
   
 5. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyu mtoa mada naona sijui ni **** au katumwa tu na magamba kumwaga upupu wake hapa. Hajui asemalo wala sielewi alifikiria nini kabla ya kupost
   
 6. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nafikiri katumwa na wanaounga mkono hoja ya posho maana hawa vijana wamegeuka kuwa "sumu" kwao
   
 7. theophilius

  theophilius Senior Member

  #7
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hayo ni maoni yako!, maoni yangu na wengine ni kwamba bila na kuwa viongozi wenye dhamira ya kuleta maendeleo, usanii wa aina hii hautaisha, hadi hapo watakapoondolewa madarakani kwa njia 'wanayoitengeneza' wao

  ndiyo maana lazima tuwazonge kila kona hadi wafanye kile tunachokitarajia, haiwezekani serikali inayokubali watendaji wake wa ngazi ya juu kama katibu mkuu waibe alafu wasichukuliwe hatua huku wahasibu wadogo wakikosea mahesabu zikapotea laki kadhaa wanapelekwa polis na hatimaye mahakamani, ikatekeleza japo nusu ya yale ambayo wananchi wake wanatarajia!
   
 8. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mtoa mada una point, vilaza wengi hawataweza kukuelewa, zitto na makamba hakuna lolote, wao ni game za kisiasa tu.
   
 9. H

  Hussein Mustafa Member

  #9
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mtoa mada nae ni janga jingine! msameheni bure hajui alitendalo
   
 10. theophilius

  theophilius Senior Member

  #10
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  **** kikweli kweli ni yule asiyependa kusikiliza maoni tofauti.. Uelevu ni kujibu hoja kwa hoja, matusi yatoka kwatu wanaoshindwa kujenga hoja, achilia mbali kuchambua, kufikiri, na hatimaye kujenga hoja, kwao njia ya mkato, kutukan
   
 11. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Toa utumbo wako hapa. how sure you are kuwa slaa, sita, mwakyembe, mbowe, lembeli na wengineo wengi wanawahurumia watanzania. Hivi kuna watu wakati mwengine huwa wanatumia downstairs kufikiria? sina hata hamu ya kusoma huo utumbo wako.
   
 12. mpiganiahaki

  mpiganiahaki Senior Member

  #12
  Feb 1, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  zitto najua alishanunuliwa siku nyingi! .. . . Sasa naona wameamua kuunganisha nguvu na J. Makamba ili watuingize shimoni Watz, ila bahati mbaya wamechelewa sana! Wote lazima waangukie pua
   
 13. J

  Jonas justin Member

  #13
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana jipya kama waliomtuma..
   
 14. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  January makamba hana uzalendo wowote. n wala hana mashabiki. Anaingia Jamiiforums na ID zake 25 anajiandikia mada na kuanza kujisifia. Mwandishi wake wa Habari Mange Kimambi ameanza kutamba mitaani jinsi january alivyoingilia kesi yake na Zadock Magai na kumfanya Magai alionje joto la jiwe. Kwa hiyo january hana jipya zaidi ya kuendeleza ufisadi. Kumbukeni huyu alivyo na siasa za majungu.

  Anamuandama Ngeleja na Membe ili aonekane msafi ilhali hana usafi wa aina yoyote. Huyu mtu akipewa madaraka watanzania watakoma, mawazo yake ni uwaziri serikali ya Lowassa na Urais 2025. akafie mbali.

  Zitto naye ni mchumia tumbo tu Chadema walishamshtukia. Huyu mtu baada ya kutoka Ikulu akaanza siasa zake za kuwatukana wafanyakazi wa Ikulu kwenye mitandao. TISS wanalifahamu ili lakini hawataki kuchukua hatua.

  Tuone kama 2015 atalipata tena jimbo la bumbuli anakopita anajifanya amelala ili vijana wasimuone. Siku yake inakuja Kalagabahu
   
 15. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Theophilus!

  Unataka tujadili nini kwenye hiyo hoja yako? Watu yaani January na Zitto, au hoja zao, au hisia zako juu yao, au unafiki wako unaosomeka wazi wazi kwenye hoja yako?

  Muda upi wa wabunge unaopotea? Muda wa wabunge kusinzia? Kisha kupokea posho ya shs 330,000/- kwa kusinzia? MB John Komba CCM yuko Arusha leo anakusanya posho kwenye mkutano wa NSSF, hana mchango wowote, wakati vikao vinawangoja Dodoma, je hivi ndivyo wana thamini muda?

  Theophilus, "give us a break" kama wewe ni kuwadi wa mafisadi... waambie umekuta JF kuna thinkers.
   
 16. theophilius

  theophilius Senior Member

  #16
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  anayefikiri kutumia downstairs ni yule asiyependa kusikiliza maoni tofauti.. Uelevu ni kujibu hoja kwa hoja, matusi yatoka kwa watu wanaoshindwa kujenga hoja, achilia mbali kuchambua, kufikiri, na hatimaye kujenga hoja, kwao njia ya mkato ni matusi,
   
 17. N

  Ndusty JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  tatizo la watanzania ni ubinafsi na uelewa mdogo.mtu mwenye akili zake timamu lazima anaona wazi mchezo wa maigizo wanaoufanya zitto na wenzake.kwanini hatuoni chadema wakija juu kupinga hoja ya posho? Pia tulisikia comments za mnyika baada ya posho kupandishwa.posho za wabunge hazitafanya maisha ya wananchi yaawe bora.

  Zitto ana vyanzo vya income vingi tu hivyo hawahitaji hivyo vijisenti vya bungeni.lakini kwa mmbunge wa kawaida ambaye hana source nyingine yoyote ya income kweli anastahili kuongezewa posho.

  Wanafanya kazi kubwa sana.mara nyingi misaada mingi wanayotoa majimboni huwa wanaingia mifukoni mwao.hivyo akina zitto wasitake kuleta issue za kitoto bungeni ili kupoteza attention ya wananchi kwenye issues za maana. Yoyote unayewatetea una lako jambo..be blessed!
   
 18. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nashawishika KATIBA MPYA NI HOJA YA MSINGI NA MAMA wakati huu, ila unapoint mtoa mada. Time will tell acha wengine wakurukie maana ndo zetu.
   
 19. TODO

  TODO JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yaani unapenda malumbano yasiyoisha ya kina jairo unakata hoja za kukuza kukuza uchumi.wewe ni hufai kuitwa mwanajf maana huna fukra pevu.hujui kuwa tz tumetumia miaka kama mitatu hivi kulumbana tu pasipo kuwa msingi wa hoja za maendeleo.sasa watu wanakuja na hoja za kututoa hapa tulipo wewe unaponda.kweli tz tunakaz ya kufanya
   
 20. theophilius

  theophilius Senior Member

  #20
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  you are not among them!, great thinkers tolerates others thinking, of course every one has right to to think!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...