Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,276
Siyo kwamba Rais Magufuli hamuelewi Tundu Lissu, isipokuwa ni analinda maslahi yake kisiasa. Anayoyasema Mhe. Lissu yana manufaa kwa nchi kuliko hata anayoyasimamia Magufuli mwenyewe, na Mhe. Lissu ameonesha uzalendo wa hali ya juu kuliko kawaida, Ila kwa kuwa Magufuli anatetea maslahi yake kisiasa, anatumia nguvu kubwa kumkandamiza Mhe. Lissu asiuzungumze ukweli au asieleweke na kuungwa mkono na watanzania, lakini watanzania wa sasa wametambua na wametoka kwenye ujinga, wanafahamu kuwa nchi hii ni nchi ya watanzania, sio ya Magufuli wala ya kundi la wachache CCM, wala vinginevyo.. watanzania wanahitaji viongozi wa aina ya Mhe. Lissu na si vinginevyo, wanahitaji kuambiwa ukweli na si blah blah, wanahitaji maendeleo ya kweli na sio vitisho, hawahitaji ukali, matamko wala kauli za ajabu ajabu za ubaguzi na ukandamizaji wa haki.