Siyo kila kifo kinasababishwa na Corona

kichoroba89

Senior Member
Oct 3, 2019
197
57
Watanzania tumejisahau sana kuhusu vifo,kabla ya Corona watu walikuwa wanakufa kama kawaida,kuna watu walikuwa mahututi tayari Mahospitalini lakini kwasasa wakifa wote tunawajumuisha katika idadi ya Vifo vinavyotokana na Virus vya Corona. Tunajipa taharuki kubwa wenyewe badala ya kuchukuwa Tahadhari tunabaki kuwa na Hofu ambayo ni hatari hata kuliko hofu ya Ugonjwa wenyewe.

Tukumbuke kuwa, wapo watu wanaoumwa Presha,pumu,kisukari na hata Malaria Kitakwimu
zinaongoza kwa Vifo Duniani.

TUPUNGUZE UZUSHI,TUCHUKUWE TAHADHARI DHIDI YA CORONA
 
Haikua desturi yetu kuzika watu usiku huku wahudumu wa afya wakiwa ndani ya PPE
 
Hatukuwa na mambo za kupangiana idadi ya waombolezaji msibani.... msibani tulijazana... tulikunywa uji na kula wali maharage.... kwa wingi wetu.... leo hii wapendwa wetu wanazikwa na Serikali
 
Lakini tusikubali kukubaliana na kila Uzushi mtandaoni,wanaoposts hawana uhakika
Leo hata mimi nikifa nitazikwa na watu wasiozidi kumi kuepuka msongamano,kwasababu hata kama sijafa na Corona inawezekana katika kundi la wataokuwa katika mazishi kuna wenye virus ila hawajathibitisha hivyo ni rahisi kuambukiza wengine
 
Hawana uhakika kwasababu hawapati habari kamili. Mawasiliano kati ya viongozi na raia yakiwa mazuri na wananchi wawe huru kuuliza maswali na kupewa maji u ya kuridhisha hakutakuwa na uvumi.
 
Barakoa ndio Tahadhari mojawapo
 
Hawana uhakika kwasababu hawapati habari kamili. Mawasiliano kati ya viongozi na raia yakiwa mazuri na wananchi wawe huru kuuliza maswali na kupewa maji u ya kuridhisha hakutakuwa na uvumi.
Hapo upo sahihi dada nimekuelewa vizuri sana
 
Watanzania tumejisahau sana kuhusu vifo,kabla ya Corona watu walikuwa wanakufa kama kawaida,kuna watu walikuwa mahututi tayari Mahospitalini lakini kwasasa wakifa wote tunawajumuisha katika idadi ya Vifo vinavyotokana na Virus vya Corona. Tunajipa taharuki kubwa wenyewe badala ya kuchukuwa Tahadhari tunabaki kuwa na Hofu ambayo ni hatari hata kuliko hofu ya Ugonjwa wenyewe.

Tukumbuke kuwa, wapo watu wanaoumwa Presha,pumu,kisukari na hata Malaria Kitakwimu
zinaongoza kwa Vifo Duniani.

TUPUNGUZE UZUSHI,TUCHUKUWE TAHADHARI DHIDI YA CORONA
Ni sawa lakini hii kasi ya vifo kwa akili yako imechangiwa na nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini mbna wana zikwa usiku na wana zikwa sehemu moja kwani hawana kwao
 
Nimevaa,ahsante kwa ukumbusho,ila Elimu ya uvaaji hatuna,kuna mtu anavaa barakoa lakini anapoongea anaishika anaishuka kwenye kidevu anaongea akimaliza anapandisha,kama mikono ina virus au barakoa ina virus Tayari anasambaza katika maeneo ya mwili
 
Watanzania tumejisahau sana kuhusu vifo,kabla ya Corona watu walikuwa wanakufa kama kawaida,kuna watu walikuwa mahututi tayari Mahospitalini lakini kwasasa wakifa wote tunawajumuisha katika idadi ya Vifo vinavyotokana na Virus vya Corona. Tunajipa taharuki kubwa wenyewe badala ya kuchukuwa Tahadhari tunabaki kuwa na Hofu ambayo ni hatari hata kuliko hofu ya Ugonjwa wenyewe.

Tukumbuke kuwa, wapo watu wanaoumwa Presha,pumu,kisukari na hata Malaria Kitakwimu
zinaongoza kwa Vifo Duniani.

TUPUNGUZE UZUSHI,TUCHUKUWE TAHADHARI DHIDI YA CORONA
Kaka hata akifa mmoja kwa CORONA hatutanyamaza, serikali inapaswa ifanye wajibu wake. Unataka wafe Watanzania wafe wangapi ndiyo serikali ishtuke?
 
Kwahiyo kwenye mazishi tu ndo kunaepukwa misongamano ila makanisani,masokoni,kwenye mabasi uko kwenyewe virus haviwezi kupata watu. jombaa hebu acha basi.bora ungekaa kimya tu.

Back
Top Bottom