. . . . . "Siwezi kumuachia hela nikisafiri" . . . . .!!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,702
Huyu jamaa anaishi na mwanamke wake kinyumba,ni kama mke na mume.
"
Wakati wanakutana,mwanamke alikua tayari ana watoto wawili aliozaa na wanaume wawili tofauti.
"
Tatizo ni kuwa mwanamke amekuwa analalamika kuwa jamaa huwa haachi matumizi.
Sasa leo ndo nimekutana na jamaa huyo na kumuuliza kulikoni?
Nae alijibu ifuatavyo;
"Sio kweli kuwa simpi hela ya matumizi ila ninaponunua mahindi debe moja likiisha nae anatakiwa anunue kwa kuwa anafanya kazi!
Tatizo la mke wangu huyu ananilazimisha nikisafiri anataka nimwachie hela,sasa nimwachie hela ya nini wakati mimi sipo na sina watoto pale"?
"
Sikujua hasa nimuulize nini,lakini jamaa aliposema kuwa hawezi kulisha watoto ambao sio wake na anapogharamia chakula wakati yupo ni kwa sababu na yeye anakula ndipo nilipomuelewa.
"
Lakini nilimuuliza kuhusu kumgharamia mkewe hata kwa kiasi kidogo kwakuwa yule ni mkewe,jamaa akasema angefanya hivyo kama mkewe angekua hana kazi!
"
Huyu jamaa haamini kama ni sahihi kumpa matumizi mwanamke mwenye ajira.
"
Lakini pia hataki kugharamia familia isiyo yake.
"
Je huyu yuko sahihi?
Kama yuko sahihi inawezekana hii ikawa sababu ya baadhi yetu kuwakimbia wanawake wenye watoto!!
 
Yuko sahihi nadhani. Labda kama kulikuwa na makubaliano hapo mwanzo tatizo wanawake nao wanapenda miteremko sana
 
Wakati anamleta ndani ya nyumba yake alijua mwanamke ana watoto wawili ambao sio wake
hatujui wakati wanakaribishana waliambianaje kuhusu malezi na matunzo ya hao watoto
Kama anaona hawezi kutunza familia isiyo yake je na yeye akipata mtoto itakuwaje
dah hapo pagumu aise na hatujui makubaliano ya hao wawili
Kweli wajanja wawili wamekutana hapo
 
kwani wakati anamuoa huyo mwanamke hakujua anawatoto?au alijua anaoa mbunye tu,wellan fine ,hapa duniani tunapita tukusaidi amtu au watu nivizuri sana na kama msalaba huwezi ubeba wala usiusogelee.
 
Hayuko sahihi kabisa! Huyo jamaa ni ****, inawezekana wanamsaidia kutunza huyo demu
 
Kuna ugumu sana hasa pale mwanamke ana watoto kwani kibishi mwanamme anaweza kukubali nitawapenda tena kama wanangu ila kihalisia ni wachache sana wanaoweza kuwapenda, pia huyo mama anapaswa kumzalia jamaa mtoto kwani nalo laweza kuchangia jamaa kuhisi upweke ndani ya hiyo familia.Ila huo hautakuwa mwarobaini ila mara nyingi kutarudisha ile kujiamini kama mwanamme na kuamini nami nimeduu hadi nina wangu hawa wote wanastaili kuishi kwa raha. But ITS SOME HOW COMPLICATED
 
Dah, hizi hadithi bana. Inakuwa sawa na ya jana clouds njia panda, jamaa wanagombea mimba!
 
Kutoa ni moyo mkuu, na jamaa anakosa baraka za bure tu apo, Japo kuna kusaidiana lakini Mwanaume ana wajibu wote wa kuhakikisha nyumba yake inajitosheleza kimahitaji, wife yeye anacomplement na sio wajibu wake wa msingi.
 
Ndo maana nikasema jamaa ni F.A.L.A
 
Hivi wewe mdogo wangu, unawezaje kumuuliza mtu kwa nini hamuachii hela ya matumizi mkewe? Wakikudunda usiniite
 
Hivi wewe mdogo wangu, unawezaje kumuuliza mtu kwa nini hamuachii hela ya matumizi mkewe? Wakikudunda usiniite

Hujui siku hizi mi baba ushauri?Ila kiukweli huyu jamaa ametoa mpya!!
 
Kutoa ni moyo mkuu, na jamaa anakosa baraka za bure tu apo, Japo kuna kusaidiana lakini Mwanaume ana wajibu wote wa kuhakikisha nyumba yake inajitosheleza kimahitaji, wife yeye anacomplement na sio wajibu wake wa msingi.

Kwa wanaume wa kileo na wanawake independenti,hii ngumu kuwesa aisee!
 
Hii ni ile kushea paa moja na mwanamke, bt no any love particle is left btn them.
Huyo mwanamke nae anazubaa nn, si amlengeshee jamaa akinge kimoja cha ukweli azae ili sarakasi zote za huyo mhuni ziishe?.
 
kwani wakati anamuoa huyo mwanamke hakujua anawatoto?au alijua anaoa mbunye tu,wellan fine ,hapa duniani tunapita tukusaidi amtu au watu nivizuri sana na kama msalaba huwezi ubeba wala usiusogelee.
Bora huo Msalaba asiusogelee kabisa kwani, mm ningemshauri atafute Msalaba wake kwani inasemekana anaishi naye KINYUMBA hajamuoa
Kawaida ya wapenzi wa namna hiyo huwa wanarudiana na wapenzi wao waliozaa nao, sasa kwa nini mm ndio niwalishe na wakikuwa hawawezi kuniheshimu hata kidogo
 
Hii ni ile kushea paa moja na mwanamke, bt no any love particle is left btn them.
Huyo mwanamke nae anazubaa nn, si amlengeshee jamaa akinge kimoja cha ukweli azae ili sarakasi zote za huyo mhuni ziishe?.

Lakini kama mama nae ana kipato labda hakuna haja ya kupewa matumizi wakati mume anasafiri?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom