Siwezi kuisahau siku ya jana-mwanamke ajifungua kwenye foleni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siwezi kuisahau siku ya jana-mwanamke ajifungua kwenye foleni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by njija, Jul 5, 2011.

 1. n

  njija Senior Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wadau maisha ya mtanzania siku hadi siku yanazidi kuwa magumu,kwa upande wa Dar miongoni mwa mambo ambayo yanaendelea kututesa na kutupotezea muda mwingi barabarani ni foleni za magari, katika siku ambazo zimeniumiza mimi ni jana, nilikuwa nikitokea posta mpya kuelekea tandika nikiwa kwenye daladala, tulipofika kituo cha baharini mama mjamzito alipanda katika gari ambalo nilikuwepo,tulipovuka usawa wa mnazimoja basi likiwa limejaa sana mama yule ghafla alilia kwa uchungu, mwanamke mmoja aliyekuwa karibu naye alimuliza vipi akajibu naumwa dereva akaelezwa asimamishe gari, wakati anajaribu kupaki ili watafute taxi na watu wampishe ashuke yule mama akashindwa hata kusogeza mguu kilichofuata akakaa ktk ngazi ya mlangoni mara mtoto akalia wanawake walio kuwa karibu yake wakamsaidia kupokea mtoto watu wote wakiona ikawa shida watu kushuka, ikabidi dereva kuendesha gari mpaka hosp iliyokuwa jirani abiria tukiwepo, kweli sipendi kuendelea kwani inaumiza sana MUNGU ATUSAIDIE WATANZANIA, sasa kwa tukio la jana nikajiuliza vipi kuhusu zile bajaji zilizonunuliwa maalumu kwa wajawazito kuna sehemu ya nurse kukaa ikitokea dharura aweze kumsaidia mama? au zina ukubwa gani kumwezesha mama mjamzito kulala vizuri wakielekea hosp? nawasilisha
   
 2. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli ni habari ya uchungu sana.
  nadhani na mama hakua makini lakini. ukianza kusogea karibu ya tarehe ya kuzaa kwa nini utembee peke yako tena kwenye daladala? Machungu yanaanza mapema kidogo hivo angeweza kujipanga mapema kidogo.
  Bahati yake mlimsaidia na akajifungua salama.
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Inaumiza sana mkuu.

  Labda siku wake zao wakijifungulia kwenye foleni au mitaro watazinduka....Na hapo inabidi kumshukuru Mungu kwamba amejifungua salama. What if kungetokea complications?

  Hii nchi inakera sana kwani watu wengine tumechukuliwa kama viumbe tusiopumua. Tunaonekaa kama mjitu ya ajabu ajabu kiasi kwamba hata mijusi ni bora zidi yetu!!
   
 4. n

  njija Senior Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hata mimi niliwaza hivyo, lakini muda tulio kaa ktk foleni lazima ingekuwa hivyo hata kama angekuwa kwenye taxi angejifungua njiani hakuwa peke yake alikuwa na binti yake ila hakuwa na la kufanya kwasababu ilikuwa kama kitendo cha dakika kumi tu mtoto tayari akazaliwa.
   
 5. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hii inaleta uchungu sana, yaani mtu anajifungua akiwa kwenye daladala iliyojaa abiria!! our country will soon become evil land.
   
 6. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... baya zaidi ni kweli kwamba pamoja na udhalimu huu, habari ya kusikitisha, ya kutia huzuni kama hii inasahaulika na kuyeyuka mithili ya petroli kesho yake. Inawezekana mama huyo mjamzito hakuwa na choice ya kubaki nyumbani au kwenda kliniki akijua siku imesogea kutokana na makali ya maisha. Mbaya zaidi ni future inayomsubiri huyo aliyezaliwa ikiwa mabadiliko ya haraka hayafanyiki nchini.
   
 7. u

  ureni JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,273
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Haya mambo yanatokeaga na yanaweza kutokea kwa masikini hata tajiri kwa sababu kutokana na hizi foleni mwanamke anaweza kuwa katika gari yoyote daladala au gari ndogo,ni mambo yanatokeaga hata wanawake wengine wanajifunguliaga mpaka kwenye ndege
   
 8. F

  Froida JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Nadhani unakufuru kama wewe umejaliwa uwezo wa kutembea na teksi shukuru mungu wanawake wengi tuuuuuuuu wanapanda daladala kabla na hata baada ya kujifungua mambo ambayo zamani hayakuweko pale ocean road walikuwa wanarudisha majumbani mwao na ambulance,hata wakipiga simu ambulance ziliwafuata ndio Tanzania baada ya miaka 50
   
 9. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maisha haya!
   
 10. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Very bud
   
 11. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Dah! Tutafika kweli....
   
 12. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari ya kuhuzunisha, polen mama. Folen ni janga .Hapa tusiangalie indicators za kwenye makaratasi. Tunafundishwa early self referral lakin access ya kuzifikia hakuna. Then wabunge wanapongezana kwa kupunguza vifo vya wajawazito. Ujinga mtupu.
   
 13. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,576
  Likes Received: 12,860
  Trophy Points: 280
  pole mamy,ila kinamama nasi tupende kwenda kliniki huwa mara nyingi wanakadiriaga muda utakaojifungua na ni vyema kuuzingatia ili mambo kama haya yastokee!
   
 14. MANI

  MANI Platinum Member

  #14
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,872
  Trophy Points: 280
  Flora mleta mada hapa ameweka vitu viwili. Kuna hili la foleni sasa hata kama angekuwa anakwenda huko hospitali na hizi foleni zetu zisizo tabirika jibu sitakuwa hilo hilo!
   
 15. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Pole kwa tukio hili na wanaojaribu kulaumu kwa kusema akuwamakini kuangalia tar za makadirio fikirieni Mara 2 Akuna anaependa hadha Kama hii
  msiba usikiege kwa mwenzako tu
   
 16. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unafikiri kuna mama wa mjini asiyeenda clinic kwa sasa?sio mara nying wanakadiriaga NI LAZIMA WAKADIRIE , Imagine imetokea 2weeks before?? Na kama alikuwa anaenda hospital? Unazijua hospital zetu zilivyo na msongamano? Watu wanarudishwa majumban kisa uchungu haujakuwa mkubwa kupisha nafasi. Jaribun kwenda kwenye hospital za government mjionee hali halisi.
   
 17. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  huyu mama hastahili lawama wamama wengine uchungu mara moja wala hauchukui muda mrefu. Clinic nyingi hazina ultrasound hivyo ni ngumu kukadiria na hata wakikadiria wakati mwingine haiwi sawa mfano shemeji yangu walikadiria 13 februari lakini alijifungua tarehe 24 januari na kadiria yenyewe ni ya ultrasound
   
 18. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kuna jitu naona anasema mama hakuwa makini..... Hivi wewe ukiwa na uwezo wa kuchukua tax unadhani wote wanaweza
   
 19. M

  Mom 2b Member

  #19
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 1, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchungu hauna taarifa mpendwa,unaweza kuanza popote tena ghafla hasa mimba ikiwa ni ya pili na kuendelea. Af kingine kutokana na ugum wa maisha mtu huwez kukaa kisa et unakaribia kujifungua,lazma kutafuta. Dala dala ndio usafir wa walio wengi hapa jijin so hiv vitu ni vya kuomba Mungu tu visikukute
   
 20. Amina Thomas

  Amina Thomas JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 272
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ndugu yangu uzazi hauna kujipanga. Unaweza kuzaa wakati wowote. Kwa wanawake waliozaa wanaelewa zaidi. Unaweza kushikwa uchungu hata mimba ya miezi 7! Nampa pole sana huyo dada.
   
Loading...