Siwezi kabisa -- mambo yamenishinda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siwezi kabisa -- mambo yamenishinda!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jan 27, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Wadau – mambo yamenishinda kabisaa. Mimi na familia yangu tumeamua kila siku kuzima main switch ya umeme nyumbani mchana kutwa kuanzia saa moja asubuhi ninapotoka hadi saa 12 jioni ninaporudi.

  Kama ni siku ya kukosa umeme kutokana na mgao, well and good.

  Isipokuwa Jumamosi na jumapili of course. Gharama za umeme zimenishinda kabisa – siwezi.

  Hivyo nyumbani kwangu umeme natumia usiku tu. Sina AC, nina kafriji kamoja ambako kanaweza kusubiri umeme wa jioni. TV, redio ni usiku tu.

  Kupiga pasi ni weekend tu, lakini nafikiria kuwa naweka nguo zangu chini ya mchago (mto) baada ya kuzikunja vizuri.

  Nawashauri wadau wenzangu mfanye hivyo ili muokoe matumizi ya hela zenu, najua wengi wenu mna matatizo kibao.

  Pia tuwashikishe Tanesco adabu kwa kuwakosesha mapato – maana wanajidai wajanja – kumbe siye wateja ndiyo wajanja zaidi.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  taa-betri na solar
  jiko-gas
  pasi-mkaa
  computer-ofcn
  simu-nachaji ofcn
  friji-gas/kerosene
  radio-nasikiliza ktk gari
  tv- naangalia baa
  yaani naenjoy kweli.......
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hata mkisema mnawashikisha adabu wasipate pesa kupitia sisi Serikali bado itatoa ruzuku................
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Karibuni ktk chama cha watumia Solar Power,pale kwangu moro-kihonda aaaaaaaaaah familia yangu ipo powa tu niliwapatia pannel za mchina watt 90 betery zao mbili,charger controler na ka inveter ka watt 60,maishaaaaa safiiiiii
  poleni mnao umia na tannesco,mi nilipata tabu siku ya mwanzo tu kusubiri jua lakini sasa safiiiiii


  SOLar power kwa maisha bora

  mapinduziiii daimaaaaaa:clap2:
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Nadhani niko karibu kuuungana nawe -- lakini hili la kupiga pasi mchagoni halijatulia! Kwani pasi za makaa hakuna? Nitajaribu kuangalia madukani.
   
 6. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  leo wamekata na kurudisha asubuhi wameniulia radio yangu panasonic ya chumbani uuwwiiii!
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi nauliza: kam,a theluthi moja ya wateja wa tanesco wa majumbani wakiamua kuzima main switch kwa masaa 12 kila siku -- shirika hilo laweza kuikwama kimapato?

  Ni swali tu.
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Mbona umechelewa sana kuchukuwa maamuzi ya busara? mimi nilishajifunga mkanda siku nyingi, kuna rafiki yangu alitaka kunipa ac sprint unit used bure, nilimshukuru tu nikamwambia asante kwa kunijari lakini nikiifunga kwangu itakuwa ni urembo tu maana haitotumika, umeme bei yake haikamatiki tena, na kuhusu friji hilo nalo nina mpango wa kuliuza maana halina kazi tena, maji siku hizi tunanunuwa barafu za shilling 50 then unaweka kwenye jag, unazimuwa na maji ya kawaida unapata mji safi bariiidi kabisa. na hapa ndipo nafikiria kurudi kwenye asili ya mtanzania nataka kununuwa mtungi ndio litakuwa friji langu.
  Ushauri: tuachane na bulb zilizopitwa na wakati zile za watts 100, hazifai ni hasara, nunuweni ernegy server za watts 4.ni bei kubwa zaidi lakini inasevu matumizi.
   
 9. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tutavuna tulichokipanda wakati wa uchaguzi:coffee:
   
 10. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hakutakuwa na mgawo siku yapili, Ni jibu rahisi.
   
Loading...