Siwezi amini hichi kitu kinaweza kutokea..(soma kisha hiki) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siwezi amini hichi kitu kinaweza kutokea..(soma kisha hiki)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mwenda_Pole, Oct 5, 2009.

 1. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Leo mida ya saa mbili usiku nilikuwa nasikiliza Radio Maria na walikuwa wanajadili hichi kisa ambacho kimenishangaza sana.

  Kisa chenyewe ni hichi: Kuna jamaa alikuwa na mke wake wa ndoa na waliishi kwa kipindi cha takribani miaka 3 hivi lakini bahati mbaya hawakufanikiwa kupata mtoto muda wote huo. Sasa baada ya kuona miaka inakwenda lakini na mambo sio mazuri, familia za pande mbili walianza kulaumiana. Upande wa mume wanambwambia mtoto wao kuwa umeoa mke asiyezaa na upande wa mke nao wanamwambia mtoto wao umeolewa na mwanaume suruali. Baada ya presha hiyo kuzidi ili kujilindia heshima mwanaume akaibuka na wazo kwa mke wake kuwa amuombe rafiki yake (rafiki ya mwanamume) ashiriki na mke wake ili awasaidie kutafuta mtoto na wafanye siri yao. Baada ya kukubaliana na kweli haikuchukua muda jamaa akawa anakula na anapatiwa na support juu kimaisha kwani huyu mume (mwenye mke) alikuwa anajiweza na yule jamaa (Msaidizi) mambo yake yalikuwa sio mazuri kimaisha. Jamaa aliendelea kula kama kawaida na hatimaye wakafika watoto watatu. Kadri muda ulivyokuwa unaenda mke akawa hana heshima tena kwa yule mume wake na pia mambo ya yule jamaa (msaidizi) yakaanza kuwa mazuri na hatimaye anataka kuchukua watoto wake pamoja na mama yao (mke aliyezaa nae) ili aishi nao na kuwatunza mwenyewe. Jamaa ameshaamua kama noma na iwe noma lakini lazima achukue watoto wake, kutokana na hali hiyo jamaa sasavwameshakuwa maadui kabisa na yule.

  Nimekuta kipindi kipo katikati lakini kifupi ni kuwa Msaidizi anamtolea vitisho vya hali ya juu huyu jamaa aachie watoto na mke nae heshima ndio imekwisha kabisa kwa mume wake na amekwishafika kwa yule jamaa (msaidizi).

  Jamaa alikuwa anaomba wasikilizaji wamshauri afanye nini, anajilaumu sana kwani ameshagundua kuwa aliochukua haukuwa uamuzi mzuri wa kumuachia jamaa ajinafasi na wife wake na anajilaumu sana juu ya uamuzi huo.

  My Take:
  Hata kama sina uwezo wa kuzalisha lakini kumtafuta mume mwenzangu tena rafiki yangu na kumkabidhi mke hii ni zaidi ya kutokuwa na uwezo wa kuzalisha.
  Wadau nyinyi mnasemaje kuhusu hii? manake sio siri mimi nilitamani kuibamiza chini na kuivunjilia mbali radio yangu.

  Hivi mtu unapoomba jamaa akusaidie mke unakuwa anafikiria nini? Na mambo huwa yanakuwaje? Yaani jamaa anakuja nyumbani kwako unampisha chumbani na wewe kwenda kulala sebuleni ? au utajisikiaje mkeo anapokuaga asubuhi wakati akienda kazini kuwa leo ninajisikia nina hamu sana nikitoka kazini nitachelewa kurudi nitapitia kwa jamaa ama nitalala huko huko tutaonana kesho...damn...!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! yaani mpaka key kwenye keyboard hapa sizioni.

  Unatarajia huyo mke ataendela kukuheshimu? Na hao watoto watakaozaliwa utawaitaje hata kama wao wanakuita baba?
  Tusaidiane kwa mawazo kina dada pia mnalionaje suala hili.

  NB : Hichi ni kisa cha ukweli na mtangazaji alikuwa pamoja na huyo jamaa yaliyomkuta.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu..ila bado sijaona connection na siasa kuifanya mada hii ifuzu kubandikwa kwenye jukwaa la siasa.Mods pls do the needful ili ipewe uzito stahiki.Jukwaa la mahusiano lingeweza kufaa zaidi na kule kuna wataalamu ambao wengine jukwaa la siasa ni kituo cha polisi.
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ^^^

  :D:D:D si utani!
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mtu utaachiaje mkeo aliwe na mwanaume mwingine? Na mwanamke utakubalije kufanya mapenzi na mtu asiye mumeo? Nadhani hisia ziligubika upeo wao wa kufikiri kiasi cha kuto kuona kitu kilicho dhahiri. There plan was bound to cause the mentioned results.
  Pia hii ni fundisho kwa familia zetu. Msiingilie ndoa za watu wawili. Wameapa wenyewe sasa nyie mnaingilia vya nini?
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Whaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaat!!!!!
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mwana F1
  Haya mambo ya kulazimisha kuzaa/kupata watoto hufikisha watu pabaya.Nina mifano mingi sana na majanga yaliyowapata watu kwa sababu hii.Tungeanzisha thread kulijadili hili na kubadilishana uzoefu nadhani tungeshangaa.
  Kitu watu hawajui ni kwamba siyo kila mtu kaandikiwa kuzaa/kupata watoto!Unapilazimisha matokeo ni haya.
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I agree with you 110% mkuu. Kitu ambacho watu hawaelewi ni kwamba ndoa 1st and for most is husban and wife. Once you are husband and wife then there you already have a family. Children don't build the family but rather add to the family which was initially husband and wife. I think the problem is people not seeing a husband and wife as already a family unit and thinking that only with the presence of children can a family truly be a family. Nadhani kwa wengi tatizo ni definition yao ya what makes a family.
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kukosa watoto kuliwachanganya sana wanandoa wale. Unajua waafrika tunavyoweka mkazo mkubwa wa kupata watoto katika ndoa kiasi kwamba kwa wengi watoto ndiyo ndoa. Kumbe bila watoto - kwao- ndoa haina maana wala furaha. Ukosefu wa watoto kwa ndoa hii pamoja na zile kelele za ndugu zao ndizo ziliwapoteza akili ndipo wakajikuta wanafanya hayo waliyoyafanya ili wapate watoto.

  Ni kweli katika mazingira ya kawaida si rahisi mtu kumwachia rafiki mke wako. Lakini ujue hawa wanandoa walibanwa sana na tatizo lao na kuona bora wamshirikishe rafiki yao katika kutatua tatizo hilo. Tujue kwamba mtindo wa kusaidiana kupata watoto ulikuwepo hata miaka ya zamani hasa kati ya ndugu wa ukoo/familia kama mmoja wao alishindwa kuzaa au alikuwa hana nguvu za kiume. Leo hii watu wengi wanaamini sana rafiki zao hasa wale walioshibana nao. Si ajabu mtu akamshiriisha rafiki yake badala hata ya ndugu yake amsaidie kupata watoto kama walivyofanya wanandoa hawa.

  Hakika kimaadili hawakufanya jambo jema. Walipaswa kujua kwamba ndoa ni ya wawili, na watoto ni zawadi ya Mungu. Kumbe hata wasipopata watoto ndoa bado iko palepale na wanapaswa kuendeleza upendo wa kindoa kati yao. Wananadoa hawa walisahau hili ndo mana wakaingia kusiko.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kweli definition ya family iko na utata - hakuna a general one to cater for all.Kuna watakaosema kuwa familia ni ile nucleus family - baba, mama na huongezea humo na watoto.Kuna watakaosema kama wewe kuwa familia ni baba na mama.Kuna bado watakaosema ni hao pamoja na extended family members - wakwe, shemeji/mawifi, wasaidizi etc.Waafrika wengi hawaoni kama mke na mume ni familia tosha na hivyo hudhani lazima watoto wawepo ndipo ikamilike.
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  NA ZAWADI HAILAZIMISHWI hata kama unaitamani vipi,.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,288
  Likes Received: 19,438
  Trophy Points: 280
  Jamaa akichukua watoto wake mshikaji ataaibika kinoma sasa solution ni kumloga jamaa apotee zake huko manake yeye aliombwa msaada ...msaada wenyewe adimu kama huo halafu anataka kuharibu kila kitu ni kummaliza tu
   
 12. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mhh mbona utata jamni binafsi siwezi kukubali kabisa kutembea na rafiki wa mume wangu!! Ndoa ni sheria kuzaa na majaliwa jamni!!
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Yaani ni kumfungia safari za Bagamoyo na Sumbwawanga tu, kama ataendeleza ubishi saaaana, aelekee visiwani kule Pemba, anunuwe Popobawa wake mmoja,ajipige amtafute yule mwenye nanihiii ndeefu kidogo, amrembelee jamaa...kwisha kazi,atakuwa baradhuli maisha yake wala hatasema kuwa ana watoto...maana watu watajuwa tu jamaa ni "mtoto" tokea zamani.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  lakini Pia huyo mwanamme hana mamlaka ya kuwachukua watoto wale watoto wamezaliwa ndani ya ndoa

  Lakini haya maisha mbona kuna watu wana maamuzi ya ajabu sana
  Mtoto ni mapenzi toka kwa mola yeye aliyewapa ndoa ndio atawajaalia mtoto pia kwa wakati autakao
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Solutions nyingine jamani mbona ni shortlived!
  Uchawi siyo kumaliza tatizo bali ni kuongeza tatizo..... jamaa akishapotea/dhurika, ina maana huyo mke aliyetaka kusepa ndio atampenda tena mume? Huenda akasepa jumla na watoto.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kwi kwi ....nicheke mie
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Yaani!
  FL humu kuna mambo usicheke shosti.
   
 18. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Duniani kuna mambo, sasa kama unaona una matatizo na wewe ulioa kwa sababu gani? Maana inaonyesha jamaa alijua kuwa ana matatizo thats why akaomba mkewe atembee na rafiki yake. sasa badala ya kuficha aibu yake, ila ameumbuka zaidi
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  What use is all that if the woman doesn't love you or respect you any more and non of the children are yours? You will do all the voodoo you want but it won't solve anything. Kwanza, kwa nini umuachie mwanaume mwenzako amzalishe mkeo in the first place?
   
 20. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,790
  Likes Received: 2,452
  Trophy Points: 280

  Jamani kama mumefuatilia vizuri ni kwamba hata mkewe pia tabia imebadilika na obvious itakuwa hivyo.Heshima kwa huyo mumewe haipo tena na kule kwingine ndo amekolea kinoma nyie jamani hata akimroga mke ataharibu tu kwa kuwa atakuwa amemuondolea rijali wake.

  Kwa hiyo wazo la kwenda sumbawanga halitatatua tatizo hilo.
  kikubwa jama aende kanisani atubu kwa kosa alilolifanya na aombe kutengana na mkewe kwa hiari au kama anaweza ajiuwe kuficha aibu hiyo au apotee kwa kuwa hata nafsi itamsuta kung'ang'ania watoto wasio wake.

  Jama akiamua kwenda mahakamani shahidi wa kwanza atakuwa mke ambaye ameshamkubali kwa kuonyesha dharau hata kwa huyo anayemwita mume suruali.
   
Loading...