Siwema wa Ney awekwa jela miaka miwili kwa kesi ya kutukana

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,422
Mahakama kuu ya mkoani Mwanza imemuhukumu Siwema ambaye ni mzazi mwenzake na Nay Wamitego miaka miwili jela kwa kesi ya kumtukana mtu kwa njia ya mtandao.

Siwema alituhumiwa kumtukana matusi kwa njia ya mtandao mlalamikaji ambaye anafahamika kwa jina la Deo.

Akizunguza na kipindi cha Jahazi, kinachoruka kupitia Clouds FM, Nay Wamitego alisema ‘napambana kile nitakachoweza kuangalia kama kunauwezekano wa kumpa msaada’.

“Kuna vitu nafikiria kuvifanya ili kujaribu kumsaidia, baada ya kupata hizi taarifa kidogo kama siko sawa hivi. Ni mzazi mwenzangu mimi nay eye tulikaa muda mrefu, napambana kile nitakachoweza kuangalia kama kunauwezekano wa kumpa msaada mwingine kwa njia yeyote ili asiwe kwenye mazingira ambayo tayari ameshawekwa. Anayemshtaki najua anaitwa Deo, jina jingine silifaham,” aliongezea.

Nay na Siwema walifanikiwa kukaa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kupata motto mmoja, Curtis kabla hawajachana na kila mtu kushika njia yake.

Chanzo: Muungwana
 
Huyo Deo si ndo yule alimvalisha pete pale kempisky wanamuita obasanjo le mutuz kavuta sana kwa Jamaa asimtoe ktk blog yake. Siwema hawezi shindana na we ye Pesa wa Mafuta
 
Huyo siwema naye alimtapeli huyo baba, akawa anamdai matumizi makubwa kila siku mara akadai anunuliwe gari ili asimwambie mkewe kuwa anatembea nae, sasa baba akachoka akaamua kumfikisha mahakamani. Akitoka huko atajifunza kula pesa ya jasho lake,
 
Black mail !!! huo ni ushetani kabisa una mfanya mtu mtumwa wa kukupa ni zaidi ya chuma ulete.
 
Sass Ney badala ya kwenda kutoa msaada Mwanza anaongea radio Dar, au kujikweza watu wamuone mtu WA maana sana
 
Sass Ney badala ya kwenda kutoa msaada Mwanza anaongea radio Dar, au kujikweza watu wamuone mtu WA maana sana
Sasa kama kapigiwa simu kuhojiwa asiongee mkuu, alisema alikua na ratiba za shoo inabidi astopishe then ndo aende mwanza ulitaka akurupuke tu kwenda..
 
Sass Ney badala ya kwenda kutoa msaada Mwanza anaongea radio Dar, au kujikweza watu wamuone mtu WA maana sana

Huyo Ney kwa statement yake tayari anaonekana elimu hana, ni mswahili mshamba tu anayetafuta umaarufu wa ushamba na unjinga. Angalia alichosema ndipo ufahamu ni taifa la watu wenye ufahamu wa aina gani lilikuw alinajengwa na awamu ya mswahili. TISS, tume ya uchaguzi na majeshi ya usalama, ninaomba mlihurumie taifa la Tanzania kwa kuepuka kumpa uraisi mswahili tena. Nchi hii ilikuwa imekufa kabisa kwa kila kitu.
 
Back
Top Bottom