Siwema adai kuachwa kumempa Akili

Mideko

JF-Expert Member
Mar 30, 2015
35,642
192,310
siwema1.jpg


Mzazi mwenziye na mwanamuziki Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amefunguka kuwa kama asingepitia misukosuko ya kimapenzi na mzazi mwenziye huyo mpaka kuachana basi asingepata akili ya kujibidiisha kibiashara.

Siwema mwenye makazi yake jijini Mwanza, alisema baada ya kupata misukosuko alitafakari na kuamua kupiga moyo konde na kusimama kama mwanamke ili afanye kitu ambacho kitamsimamisha na kuendelea na maisha yake.

“Unajua ukikumbwa na misukosuko hasa ya kimapenzi akili inatanuka, nilijiongeza haraka na leo hii nina duka langu kubwa la nguo hapa Mwanza na maisha yanaendelea, ningekaa kulilia mapenzi ningechemka,” alisema Siwema.

Chanzo :Gpl
 
Huyo mdada si alitapeli gari mpka kupelekwa police,halafu ukikutana nae uso kwa uso juu mkubwa chini hana balance mwili kma kiboko
:D:D:D:D
Jamani eti mwili kama kiboko, umenikumbusha warumi aliwahi kumsema penny eti kichwa kikubwa kuliko mwili, kichwa kipo kama mfuko wa cement
 
Back
Top Bottom