Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Kwa kweli sielewi kabisa misimamo ya wana-ccm, wakati ule mara tu alipoingia madarakani mwaka 2016, Rais wa wakati huo, Hayati Magufuli, alipopiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, huku akijua wazi kuwa anaisigina Katiba ya nchi, walijitokeza wana-ccm kibao, waliopongeza hatua hiyo na kuiita ya kishujaa na kuvisihi vyama vya upinzani, vikachape kazi, Kwa kuwa muda wa kufanya siasa ulikuwa umekwisha!
Nimeshangazwa pia safari hii, wakati Rais wa awamu ya 6, Samia Suluhu Hassan, alipoiruhusu mikutano hiyo na akaeleza wazi kuwa ni ukiukwaji wa Katiba kuipiga marufuku mikutano hiyo, Kwa kuwa ni haki yao kikatiba, vyama hivyo kuifanya mikutano hiyo na wao kama Serikali, Kwa kutumia Jeshi lake la Polisi, wajibu wao mkubwa, ni kuilinda mikutano hiyo, Ili ifanyike Kwa njia ya amani na utulivu.
Nimeshangazwa pia kuwaona wana-ccm wale wale, wakitoa pongezi nyingi Kwa Rais Samia na kusema kuwa huyu mama ni mwana-demokrasia, Kwa hiyo anapaswa kupewa pongezi nyingi Sana!😎
Ndipo hapo ninapojiuliza hivi Hawa wana-ccm wanajielewwa kweli?
Ni kwanini wakati ule Mwenyekiti wao wa CCM, ambaye pia alikuwa ndiye Rais wa nchi, alipopiga marufuku mikutano hiyo, hawakuweza kumuhoji kuwa kitendo anachofanya, ni Cha kukiuka waziwazi Sheria za vyama vya kisiasa nchini, kama walivyofanya viongozi wa upinzani na kueleza wazi kuwa Mwenyekiti wa CCM, anatumia vibaya madaraka yake, Kwa kuvinyima haki yao ya kikatiba ya kufanya mikutano hiyo ya hadhara?
Tabia hii ya ukinyonga na unafiki inayofanywa na viongozi wa CCM, ambao wanashindwa kuwa na msimamo mmoja, ndiyo inayoweza kuliangamiza Taifa letu!
Mungu ibariki Tanzania