ungonella wa ukweli
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 4,210
- 555
Ndugu wana jf, kama mjuavyo taifa letu liko katika mchakato mzima wa kujipatia katiba mpya! Ingawa kwa sasa kuna sintofahamu juu ya sheria ya mabadiliko ya katiba iliyopitishwa juzi bungeni kwa wabunge wa ccm na mzee mrema, kuna hili bunge maalumu kama inavyojulikana kuwa wajumbe wa bunge hilo wanatarajiwa kuwa ni wabunge wa bunge la muungano, wajumbe wa baraza la wawakilishi na wajumbe 166 watakaoteuliwa na rais kama muswada wa sasa unavyosema! Wasiwasi wangu zaidi upo kwa wabunge, kama watanzania wenzangu mjuavyo wabunge wetu wamekaa kimipasho zaidi, wengi masuala ya kitaifa huyachukulia kichama zaidi,tumeshuhudia wabunge wengi wakiuchapa usingizi mchana kweupe wakiwa bungeni badala ya kuwawakilisha wananchi waliowachagua, pia watanzania ni mashahidi wabunge wetu wengi ni wavivu wa kuchambua nyaraka za serikali bungeni, pia wabunge wetu ni mabingwa wa mipasho na lugha za matusi bungeni badala ya kujenga hoja kwa maslahi mapana kwa taifa letu, pia bunge letu la sasa limejaa ushabiki wa vyama badala ya utaifa zaidi, mbaya zaidi asilimia kubwa ya wabunge wetu ni watuhumiwa wa wauzaji wa madawa ya kulevya, pia wabunge wengi wameingia bungeni kwa rushwa za hapa na pale. Bunge lililopita tumeshuhudia ngumi za waziwazi bungeni. Je kwa mapungufu hayo hapo juu, je kweli watu hawa wanaweza kuwawakilisha watanzania kwenye bunge maalumu la katiba? Binafsi siwaamini watu hawa hata kidogo! Watanzania wenzangu kwa muundo huu wa bunge maalumu ni bure kabisa! Nawasilisha.