manywangari jean malonkwa
Senior Member
- Mar 17, 2016
- 193
- 188
Mjadala umekuwa mkubwa kuhusu bunge kuonyeshwa live, mm binafsi siungii mkono wabunge kufanya mjadala wakiwa wamejifungia, ktk dunia ya karne hii. Lkn mm napingana na hii hoja ya kwamba Magufuli anaogopa serikali yake itaumbuliwa, kwa kuwa kama ni mwoga inakuwa VP anaruhusu report ya CAG ambayo imeonyesha madudu kibao ya serikali itolewe, kwa lugha nyingine kama anaogopa asingemuruhusu CAG kufanya kazi yake kwa uhuru na uwazi kwa sababu ubavu huo anao. Kwa maoni yangu nadhani mkuu wa kaya anapaswa kupewa pongezi kama CAG anavyopewa. Kuna mwingine atasema report ya CAG hawez kuizuia, lkn mtu huyo huyo atakuja na kusema rais anazuia bunge, hv kama rais anaweza kuzuia mhimiri wa bunge kufanya mambo yake anashindwaje kumuzuia CAG ambaye ni mteule wake kuianika serikali. Itakuwa ni ujuha kuzuia bunge eti kwa kuwa litakuumbua wkt huo huo unamruhusu mteule wako akuumbue, sawa na nwanamke ambaye haogopi kuvua nguo sokoni lkn anaogopa watu kuzungumzia yeye kuvua nguo sokoni