Siumii kukosa ajira ila napata 'stress' kutoka kwa wanaosubiri niajiriwe

Aisee mbona ni kawaida sana tu hiyo ijapokuwa ukiyapa nafasi hayo maneno yanakuuma kwa kiasi fulani ila hicho ulichonacho kitumie vizuri na piga kazi za halali update zaidi mzee baba maisha siyo rahisi hata kidogo hasa hasa ukiwa huna kipato cha uhakika ila yatapita kwani mangapi makubwa yamepita ndugu we piga kazi usisikilize maneno yao watu washaambiwa maneno makali huko nyuma kuwa "huna ajira kazi yako kuzurura na kutembeza dudyu tu"
Ndio hivyo kupambana tu
 
Nakumbuka 2013 nilimaliza chuo kikuu fulani nchini badae nikaenda kwa bro DSM kuangalia upepo unaendaje huko huku nyuma tayari nilikuwa nimempa demu wangu mimba tukiwa chuoni na tukamaliza chuo pamoja, sasa ile kukaa kwa bro bahati nzuri nikawa nimejishikisha kwenye hardware hivi ambayo kwa mwezi nilikuwa nikilipwa laki 250,000.

Siku moja bwana nikasikia shemeji yangu (Mke wa Bro) ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii ngazi ya kata akimwambia Braza kuwa rafiki yake kapata kazi lakini fulani (mimi) bado tuuu hadi sasa yawezekana kuna warogi wamefanya yao ili asipate kazi. Kauli hii iliniuma nikasema Mungu Yupo ipo siku watakuja kunipigia magoti.

Basi bwana nikaamua kuhama pale kwa braza kwenda kutafuta geto mtaani baada ya maneno maneno kuzidi kuhusu mimi kwa kuwa nilionekana ni kula kulala tu. Kufika geto nikamvuta demu wangu na bahati nzuri akawa amejifungua tarehe kama ya leo (11.12.2013). Tukaishi kama bibi na bwana kwa mwaka mmoja.Badae Mungu si Juma wote kwa pamoja tukapata kazi kwa GOT tena Vitengo Vizuri na tumeoana. Sasa hivi tunakula bata na Mjengo tayari tumeshanyanyua umekamilika, Maviwanja mengi tumenunua. So kijana usikate tamaa ipo siku utafanikiwa cha msingi usikate tamaa na mtegemee Mungu kwa kila jambo hayo ni mapito tu. Haitaisha miaka 10 hujapata kazi yenye maslahi mazuri.
Amina
 
Graduate wanaweza wakawa wanaongoza kuwa na stress
Na vijana ambao hawajasoma waache maneno kwa wasomi mana wao wakipata boda boda used au kibajaji cha mtu kuingiza mia mbili mia mbili basi za Kula na kuvaa wanajikuja tayari wameyapatia maisha
Kiuhalisia vijana wengi ambao hawajasoma wamefanikiwa kupata pesa ya Kula na kuvaa na kulipa kodi tusidanganyane kuwa wametoboa ni waangaikaji wa wakawaida
Pitia viwanda vingi vya wahindi watu wanalipwa hadi elfu 80 kwa mwezi halafu wanakuja kucheza vijana wasiokuwa na ajira
Kwel kabisa. Dogo tu kisa boda boda dharau kibao. Afu sijui Kwann yan, mtu ambaye hajasoma anaona fursa nyingi kuliko hata wewe uliosoma.

Utaskia anakwambia, yan na elimu yako bro chuo kikuu huna ajira?
 
Mkuu nadhani kutafuta pesa nje ya ajira tena ukiwa umetoka kutoka shule ni ngumu? Au wewe unaonaje? Unaweza ukawa smart darasani ila mtaani usiwe smart, hichi ndicho kinachotukwamisha nadhani.
Kwel ila bado unaweza kupambna mtu kivingne na kutoboa
 
Wengi mnapenda kuajiriwa mkavae moka na mashati yakubana huku suruali mzibane ndio mnajiona hapo ndio penyewe...lakini kuingia mtaani kupambania kombe mnaona mtaonekaana je...

Ila ndio lengo la kusoma ni tupate ajira ila tukikosa tusilalamike tutafute njia zingine
Nimependa Ulivyo maliza. Umemaliza kila kitu
 
Safi
Mimi niliwablock watu kibao, nilikuwa nikipokea simu ya mtu, baada ya Salam , swali linalofata ni " bado hujapata kazi". Sasa hivi naishi kwa amani, Nina marafiki wapya ambao hata hawajui Kama nilipitaga chuo.
 
Sure
External Noise ni nyingi mno, unaweza kuharibika kisaikolojia. Hawajui kila mtu na bahati yake, kuna ambao wana kila kitu kuanzia uzoefu, GPA safi, Connection nk lakini hawaajiriki. It’s a matter of destiny
 
Na ukiajiriwa usiwape taarifa wala kuwasaidia pesa mara kwa mara, baadaye watakusumbua hasa majukumu yako yatakapo ongezeka, utaanza kuambiwa una roho mbaya au umerogwa na mkeo, wanaenda kukupigia ramli au kukupiga kipapai kabisa.
Duh hii balaa
 
Akili zako zimegawanyika Mara mbili,nusu ya kwanza ni timamu na nusu iliyobaki haina akili..
Nusu ya Kwanza=Umesema tayari umeshagundua hali ya upatikanaji wa ajira ikoje kwa sasa na hujutii kuikosa sababu tayari unafanya mambo yako japo si kwa ukubwa unaoutaka.Hii ni akili timamu maana yake umeshajitambua.

Nusu ya Pili=Unasema unapata Stress sababu ya kelele za ndugu na jamaa sababu ya kukosa ajira..Come on buddy,hao wanaokusema bado hawajajitambua,so kupata stress sababu ya MTU ambae hajajitambua ni kukosa akili maana yake anakuendesha ww uliejitambua..cha kufanya ni kutowajibu chochote na kuwapuuzia hizo kelele zao ww komaa na hicho unachokifanya utatoboa mana una uelewa wa kwann unafanya na malengo yako ni yapi..Mbeleni ikitokea ajira its okay utaenda kufanya ila naamini ajira sio solution ya kukutoa kwenye umaskini,ajira ni hatua ya awali ya kujipanga ktk kufikia mafanikio ya kweli yanayopatikana ktk kufanya kazi binafsi..mm sio muumini sana wa kuajiriwa ndio mana nimeshangazwa na ww kupata Stress sababu ya watu wasiojielewa..

Naomba ukomae ndugu yangu na hicho unachokifanya,hizo kelele zao zitakutoa kwenye reli usipoangalia mwishowe ukose bara na pwani..maneno ya watu kamwe hayatoisha ktk dunia hii kwa chochote kile utakachofanya.Hata ukipata hiyo ajira nakuhakikishia bado hutoepuka maneno ya kejeli fedheha na kukatisha tamaa ikiwemo ktk hiyo ajira unayoiwazia.Nina mengi ila niishie hapa.
Asante ndugu. Umenena mengi mazur. Barikiwa
 
Back
Top Bottom