Sitta: Wananchi msidanganyike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Wananchi msidanganyike

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ICHONDI, Sep 14, 2010.

 1. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Tabora, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samuel Sitta, ameelezea kushangazwa na kauli za baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani kwamba watafuta kodi na kufafanua kwamba hakuna serikali ya aina hiyo duniani.

  Sitta ambaye Spika wa Bunge la Tanzania lililomalizika hivi karibuni pia aliwataka wananchi wasihadaiwe na wagombea wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakitoa lawama badala ya kueleza wakipewa madaraka watafanya nini.

  Akizindua kampeni za CCM katika jimbo hilo katika Kata ya Usoke, mbali na kuomba kura ili aendelee kuwa Mbunge, pia alimuombea kura mgombea wa urais wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete na wagombea wa udiwani wa chama ahicho.

  “Hotuba za wapinzani zimejaa lawama na kutumia lugha za matusi mambo yanayodhihirisha kuwa hawana sera walizoziandaa kama dira ya kuwatumikia wananchi endapo watachaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao,” alisema Sitta.

  Mbali na kushangazwa na kauli hizo za kufuta kodi, Sitta ambaye alikuwa akishangiliwa na wananchi hao pia alielezea kushangazwa na ahadi za wapinzani za kutoa huduma ya elimu na afya bure.

  Kutokana na hadaa hizo, Sitta aliwataka wananchi kuwapuuza wapinzani kwa kuwa wameonesha hawana ukomavu katika ulingo wa siasa na hawajui wananchi wa jimbo hilo wanahitaji mambo gani ya msingi katika kuwaboreshea maisha yao.

  “Mimi ni gia kubwa, msichague gia ndogo zitawachelewesha kupata maendeleo zaidi kutoka hapa tulipofikia katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

  “Nimekuwa kiongozi wa Bunge na nimetambulika ndani na nje ya nchi na nimeliwezesha Bunge kujijengea heshima kubwa kitaifa na kimataifa, nimejenga uhusiano mzuri na viongozi wa kitaifa na nitatumia fursa hiyo kujenga hoja za kuharakisha maendeleo katika Jimbo la Urambo Mashariki,” alisema Sitta alipokuwa akielezea rekodi yake.

  Aliwasisitiza wananchi waliohudhuria uzinduzi huo kutofanya mzaha katika kupiga kura kwa kuwachagua viongozi goigoi wasio na uwezo wa kujenga hoja na kushindanisha sera na badala yake wajitokeze kwa wingi wawachague wagombea wa CCM.

  Sitta alisema, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita akishirikiana na mkewe, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta wamekuwa wakiwasomesha watoto yatima 200 kwa kuwalipia ada na mahitaji mengine.

  Aliahidi kuwa atawasomesha watoto yatima 40 wanaomaliza darasa la saba kila mwaka, ili wasikose elimu ambayo ni haki yao ya msingi kwa kisingizio cha kukosa fedha za kulipia ada pamoja na mahitaji mengine ya msingi.

  Mbali na ahadi hizo, pia alielezea mafanikio ya uongozi wake katika miaka mitano iliyopita ukiwepo mradi wa matrekta madogo aina ya ‘power tiller’ yaliyogawiwa katika kata zote za jimbo hilo ambao ulitokana na jitihada zake binafsi.

  Soma maoni ya wasomaji kwenye link hii hapa, utafurahi mwenyewe lol
  HabariLeo | Sitta: Wananchi msidanganyike
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Ni kweli '2010 HATUDANGANYIKI' Slaa for president
   
 3. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  "Sita anasema kipindi cha miaka mitano iliyopita yeye akishirikiana na mkewe walisomesha yatima 200"

  Hee Bwana Sitta, nadhani ulitakiwa useme kuwa Serekali kupitia kwako na mkeo mlisomesha wayatima 200. Hizo ni fedha za serekali, wewe na mkeo mmezichukua kwa njia ya ujanja, marupururu, masurufu, forgery ya risiti za matibabu etc. So kumbe elimu ya bure inawezekana, nakushangaa unakataa kuwa wapinzani hawawezi kutoa elimu na matibabu ya bure wakati weye na mkeo pekee kupitia ukwapuaji wa fedha za walipa kodi mmeweza kusomesha yatima 200?
   
 4. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Nimependa maoni ya wadau,SITTA 'Mnaa' tu,hamna lolote. Lakini bahati mbaya si wote walioisoma na kuisikia habari hii kwenye magazeti na redio wanaweza kuichambua kwa kiasi hiki.Watanzania wengi wakishasikia kitu flani jukwaani na kusoma kwenye magazeti wanabaki nayo kichwani bila critical thinking wakiamini kile kilichosemawa. Ndiyo maana hata wao wanamshangilia tu.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa hapa tu sina haja ya kumsoma zaidi, yaani mzee huyu anazeeka vibaya sana...
   
 6. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  amezeeka vibaya mno, anaona haiwezekani kusomesha bure kwa sababu serikali ya ccm imeruhusu uporaji wa rasilimali za nchi na wizi kwa viongozi umekubuhu hivo hakuna fedha za kusomesha wananchi wake. chadema itatumia rasilimali na mapato ya ndani na nje kwa uangalifu na kuzingatia vipaumbele na pia kuanzisha vyanzo vipya vya mapato, kutokuwa na mzaha katika ukusanyaji kodi, no msamaha wa kodi, mbona mihela mingi sana tu. naona huyu sitta anataka wao waendelee kuiba na kudanganya umma kwamba wanasaidia wakusomesha watoto wasio na uwezo, kwa nini wasishauri selikali itumie mapato vizuri ili hiyo kazi ya kusomesha hao 200 ifanywe na serikali. yaani waachwe waibe ili eti kafungu kadooooogo wajidai wanasaidia wasiojiweza. big sh..t.
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Watu kama Sitta nyakati kama hizi wangetakiwa wakae kimya lakini wapi, unafiki, uwongo na ulafi wao hauwezi kufichika kwani ndio jadi yao. Woga pole pole unaanza kuwaingia na wasiwasi wa kukosa vya kunyonga unaaza kuwajaa na wanaanza kubwabwaja ovyo bila mpangilio. Kama anajiamini asubiri kishindo cha Dr. Slaa siku atakapotua Urambo, bila shaka ataamka kutoka usingizini na kugundua kumbe alikuwa anaota tu ! Sadly it will be too late to salvage anything, pole sana Sitta.
   
 8. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  2010 hatudanganyiki na sisiemu.....
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Sita atuonyeshe kwanza kiwanda chake cha kuchapia noti za kitanzania ambazo amekuwa akitumia kuwasomesha watoto 200 kwa mwaka na mkewe.
  Ninawachukia watu wa aina ya Sita na nimekuwa nikiwapiga vita sana. Wamezoea kutembea Ulaya na bakuli wakiomba omba na wanawazoeza wadanganyika tabia hiyo hiyo ya kuomba.
  Kwani kwenye katiba yetu kazi za mbunge ni ufadhili? shitttttttttttttttttttt
   
 10. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2010
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Hiyo on red ndio sera yetu OMBA OMBA
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu hivi Chadema wamesema hawatatoza kodi au?.. tufahamishane...
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu CHADEMA hawajasema kwamba hawatatoza kodi zote. Unajua uandishi wa habari wa Bongo una matatizo. Dr. Slaa alisema kwamba ili kufanya vifaa vya ujenzi viwe affordable, watapunguza kodi kwenye vifaa hivyo ili watu waweze kujenga nyumba bora. CHADEMA na Dr. Slaa hawajasema watafuta kodi zote, hiyo inatumika kuwa-mislead wapiga kura na gazeti la HabariLeo kwa kuwa liko upande wa CCM haliweki details zote kwa kuwa wakiweka wanakuwa kama vile wanawaunga mkono CHADEMA na kuwaumbua CCM.

  Mfano mwingine, JK nimeona ana-spin swala la elimu bure kuanzia chekechea mpaka F6, anasema kuna kiongozi amesema shule zote atazifanya ziwe za F6, sasa anauliza hivi jamani overnite unaweza kuamka na kukuta shule zote zimekuwa za F6? Basically wanacheza na akili za wapiga kura na ni kwa kuwa wapiga kura hawawaulizi maswali na pia waandishi wetu wanaandika habari kwa ushabiki.

  So kodi zitaendelea na zitakazofutwa/punguzwa ni zile ambazo zina malengo ya kuboresha maisha ya walalahoi. Wachimba madini na wawekezaji kutoka nje wajiandae kuondolewa misamaha ya kodi, maana walishafanya hii nchi ni kama shamba la bibi ambaye hana uwezo wa kulilinda hata nyani wakija wanajilia mahindi yao kwa nafasi na hakuna anayewabughudhi.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Shukran sana mkuu kwani ndivyo nilivyokuwa nikifahamu mimi sasa hawa CCM maadam wameanzisha vita hii nadhani ipo haja kubwa sana ya Chadema kurudisha mapigo. Kwanza pasipo kubishana na CCM au kujaribu kujibu hoja, Chadema wanatakiwa kuwataarifu wananchi kuwa CCM inapinga kuondolewa kodi sehemu ambazo Chadema wanataka kuziondoa ili kuboresha maisha ya wananchi. Na wazitaje sehemu zenyewe huku wakihamakisha wananchi kuwa CCM wanataka kodi zaidi... na wito kwa wananchi baada ya kila kipengele - CCM ZIII.

  halafu maneno ya Sitta mwenyewe yatumike zaidi hasa pale anapojinadi kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakisomesha watoto 200 kwa kuwalipia ada na matumizi mengine (BURE). Halafu pasipo aibu anapinga serikali kusomesha watoto bure wakati yeye mwenyewe anajisifia kusomesha watoto 200 bure... Hii kweli akili?

  Huyu mzee amepata wapi fedha za kusomesha watoto 200 kama sio kodi za wananchi ana biashara gani na kweli analipa kodi ipaswavyo? Fedha hizi anazipata wapi kama sii kodi za wananchi ambazo serikali yake wanajilipa mishahara minono kiasi cha kukufuru. Huyu Sitta anafikiri huu ni utawala wa Kisultan!..(unagangamala kabisaaaa huku kijisho kinakutoka)

  Hii nchi haina matabaka na kama tutaendelea kujenga taifa la matabaka ambalo litakuwa na watu wenye uwezo wa kusomesha watoto 200 kama sifa za utendaji kazi wao basi hatuna sababu ya kuwa na serikali. Serikali ya nini ikiwa huduma muhimu zinaweza tolewa na matajiri kama kina Sitta ambao wameingia Bungeni hawana utajiri huo leo hii wanajivunia kuweza kusomesha watoto 200.

  Yaani wee acha tu sipo ktk Kampeni ya Chadema ningemmaliza mzee huyu kwa wananchi kiasi kwamba angetafuta majibu mengine
   
 14. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mfa maji haishi kutapatapa, ama kwa hakika anguko kubwa la majambazi na mafisadi limewadia.
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkandara kudos, hili ni bonge la jiwe............... Sasa tuje ratiowise, kama Sitta na Mkewe vipato vyao ni say milioni 100 kwa mwaka na pamoja na mambo mengine wanaweza kuisomesha bure watoto 200. Je sirikali yenye trillioni 11 kwa mwaka kama bajeti itasomesha watoto wangapi bure ktk mchanganuo huo???????????

  100,000,000 = 200, je 11,000,000,000,000 = ?

  Jibu linakuja = 22,000,000. Watoto milioni ishirini na mbili

  Je tuna watoto wangapi wanosoma??????
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi kwa mwaka ( Tuchukue average figure) Mzazi analipa kiasi gani cha school fees kwa Mtoto mmoja anayesoma shule za Uma? Na je kwa mwaka kunakuwa na Wanafunzi wangapi wanaosoma katika shule za Uma? Je ni Jumla ya kiasi gani cha pesa ambacho Serikali kupitia Wizara ya Elimu inawakamua Wazazi kama Ada za Wanafunzi? Je hicho kiasi kinalingana na Fedha za EPA.

  Fanya hesabu rahisi ukipata jibu utaona kama inawezekana kusomesha watoto mpaka form six bure
   
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Assume idadi ya Wanafunzi wote kwa mwaka mmoja nchini Tanzania ni milioni mbili (2000,000), and Assume kwamba kila mwanafunzi hulipa kiasi cha shilingi 50,000 ( Kumbuka Primary ni bure O level ni 20,000 na A-level ni 70,000)

  Hii ina maana kwamba kwa mwaka serikali huchukua jumla ya kiasi cha shilingi 2000,000 * 50,000 = bilioni 100 kutola kwa Wanafunzi hawa maskini kabisa

  sasa tujiulize?

  How much wa EPA?
  How much was RICHMOND?
  How much was KIwira?
  How much was IPTL?
  How much was Meremeta?
  .....

  Hivi kweli tukiweza kuokoa hizo pesa hapo Kweli Serikali itashindwa kuwasemehe hao maskini hizo Bilioni 100?
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hivi ni kwanini CCM wanaona kuwa ni ngumu sana kutoa AFYA na ELIMU bure ukiishazoea kuiba basi utaona vitu fulani hauwezi kuvitekeleza kutokana na kuwa ile hela amabayo inapswa uielekeze kwenye hayo maendeleo wewe ndio unaitumia kwa mambo yako binafsi na kujinufaisha wewe mwenyewe sishangai anaposema kwamba amesomesha watoto 200 ingekuwa vizuri ajiulize kama hiyo hela imetoka mfukoni mwake mwenyewe bila kufanya forgery zozote zile au kutembeza bakuli na kwenda kwa wahisani kuomba hela halafu baadae unakuja una claim mbele za watu kuwa unasomesha watu kwa kutoa hela yako mfukoni kumbe its the other way round
   
 19. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  ni uhaini kwa mhe samwel sitta kudai kuwa alishirikiana na mkewe (aliyekamatwa kwa rushwa na takukuru) waliwalipia ada watoto yatima 200 ilihali pale bungeni alikuwa akiendesha ufujai wa mali za umma. Mfano ni matumizi mabaya ya gari land cruiser stk 3002 amabyo ni maalum kwa ajili ya kuhudumia nyumba ndogo ya kinondoni karibu na kanisa alilochangia rostam azizi. Gari hili la serikali hutumika kwa safari za binafsi na ufuska wa pika huyu kama vile kupelekea maua katika graduation ya watoto wa nyumba ndogo hii katika mikoa mbali mbali kwa gharama za serikali ikiwemo mafuta, posho za dereva na matengenezo ya gari husika.

  Ufisadi wa matibabu kwa kutumia stakabadhi hewa; ununuzi wa samani hewa n.k
   
 20. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndege ya Uchumi thnx for your analysis...it is simple and clear hata kwa mkulima kuelewa
   
Loading...