Sitta vs. Lowassa

Tumain

JF-Expert Member
Jun 28, 2009
3,154
70
Mjadala unaoendelea ndani CCM kati ya Sitta na Lowassa has something to do with 2015 presidential candidancy...naona hii imekuwa tayari ni kambi za kugombea uongozi zaidi ya kupinga ufisadi?

Naamini Sitta au Lowassa wanajiandaa kuchukua nchi baada ya JK..kwa hiyo haya mapambano yataendelea miaka mitano ijayo hata baada ya uchaguzi...

Common denominator (wote ni wanasiasa, wana CCM, wanapenda Madaraka na fedha wanayo) siku wakiamua kuwa wamoja na kugawana vyeo (compromise) kama alivyofanya JK wananchi tutegemee maumivu miaka mingi under CCM rule

Wakiendelea kuwa wagomvi itakuwa faida kwetu kama nchi .. Just curious...
 
Mie nimesikia kuwa Bernard Membe ndio anaandaliwa kuchukuwa nchi lakini fununu tu!!!!
 
Anaandaliwa au anajiandaa?

Nasikia alitolewa katika ofisi ya balozi kimya kimya akaja kupewa nafasi agombee ubunge nasikia yuko katika pipeline apewe urais. Maana analelewa na system mpaka aonekane anafaa kuingoza nchi kama alivyolelewa JK
 
Raisi atakuwa Pinda kwani ni mwaminifu.

Uaminifu bila vision ya maendeleo ni sawa na sifuri.

Uaminifu bila ujasiri wa kupambana na ufisadi nayo ni sawa na sifuri.

Kwa kifupi ni kwamba kama Pinda ni muaminifu, bado hafai kuwa rais kwa kuwa jamaa ameishaonyesha kwamba ni mwoga. Alisema mafisadi inabidi kwenda nao taratibu. Hivi kweli serikali iliyo na polisi, jeshi na vyombo vingine vya dola bado Waziri Mkuu anaweza kusema hizo pumba?

Juzi kawaambia wananchi wa Igunga wampe kura Rostam Azziz, hivi kweli PM mzima unasimama kuomba kura kwa ajili ya mtu ambaye image imeishaharibika mbele ya jamii?

May be Bwana Kamundu unatania.
 
Lowasa na sita nani sii mwoga

Lowassa ana ujasiri wa kifisadi (quote from Mwakyembe Report).

Sitta kaufyata baada ya kuona CC na NEC wanavizia vikao vyao. Kwa hiyo huyu nae ni mwoga tu.

Kwa kifupi si Lowassa wala Sitta anayefaa kuwa Rais wa Tanzania. Laiti kama Lowassa asingekuwa na sifa mbaya ya ufisadi, angekuwa kiongozi mzuri sana. Tatizo ni hilo doa la ufisadi, usiniulize ushahidi, maana hata Nyerere alisema hivyo hivyo na jamaa akashindwa ku-justify utajiri aliupata wapi.

Tanzania ya sasa inahitaji mtu mwadilifu, msafi, mwaminifu, asiye na dosari za hapa na pale, mtu jasiri asiyeogopa mtu, mtu asiyeendekeza urafiki na ujamaa, mtu anayeteua wasaidizi wake kwa kutumia merit na si vinginevyo.

Hao wawili + Bwana Pinda hawana hizo sifa. Hata hao wengine wanaotajwa huko CCM kwamba wanaweza kuwa potential candidates come 2015 bado sijaona mwenye hizo sifa. Tatizo lililo CCM ni mambo ya "huyu mwenzetu" ndiyo yametufikisha hapa tulipo.
 
Mi naona wote hawafai, inabidi tutumie approach aliyotumia Nyerere kumuibua Mkapa ambaye watu hawakuwahi kumtabiria. Au approach aliyotumia mkapa kumuibua Dr Shein ambapo watu walitabiri sana lakini hawakumtaja na akaibuliwa akawa Vice President.
 
Membe analow IQ. Rais gani, ndio hatukatai JK anamtaka amrith henchman wake lakini to be honest yule mtu sio kiongozi kabisa. Hatutokaa tuendelee kabisaa..
 
Wote Lowasa, Sita, Membe, Pinda hawafai kabisa kuwa marais wa nchi hii, wote wameshika madaraka makubwa na matokeo ya kazi zao na hulka zao yanadhihisha kabisa jinsi wasivyofaa.
Binafsi nakereka sana na watu wanaojiandaa muda mrefu namno hiyo kuwa maraisi tuna uchaguzi mwaka huu , wao wanamaandalizi ya mwaka 2015 ni upuuzi.
Sasa hivi tunahitaji watu wapya sio hawa waliokaa madarakani muda mrefu walishachoka sasa wapumzike na waachie wengine
 
Kwani Dr Salim atakuwa mzee sana wakati huo? Najua hayuko kwenya mtandao, ila watanzania tumwombee yeye atakuwa na vision zaidi!!
 
Mi naona wote hawafai, inabidi tutumie approach aliyotumia Nyerere kumuibua Mkapa ambaye watu hawakuwahi kumtabiria. Au approach aliyotumia mkapa kumuibua Dr Shein ambapo watu walitabiri sana lakini hawakumtaja na akaibuliwa akawa Vice President.

Dr. Shein na Pinda nani mwadilifu zaidi? Kiongozi bora na si bora kiongozi ni muhimu akawa na sifa hizi:-

1. Uadilifu
2. Ujasiri
3. Upeo
4. Uzalendo
5.
6.
7.
8.
9.
 
Ngoja mimi nianze kumuandaa Dr. John Pombe Magufuli!............

Nadhani huyu atawafaa, kwani akipewa, hata bakora anaweza kutembeza ili mambo yaende.....ha ha haaaa!.......
 
SITA.JPG


Kaa chonjo mzee hapo
 
SITA.JPG


Kaa chonjo mzee hapo



Yani hapo yote wanayoongea hayatoki moyoni.Ndiyo wanasiasa walivyo,wakimaliza wanaita wapiga picha,tabasamu meno yote nje utafikiri wanawiva kumbe kutwa kucha kuwindana kama ndezi..
cheki Sitta anavyomsikilizia El kiuzushiuzushi hapo..
 
Mi naona wote hawafai, inabidi tutumie approach aliyotumia Nyerere kumuibua Mkapa ambaye watu hawakuwahi kumtabiria. Au approach aliyotumia mkapa kumuibua Dr Shein ambapo watu walitabiri sana lakini hawakumtaja na akaibuliwa akawa Vice President.
Naona mawazo yako yalitumika mkuu ila yametuletea hatari kubwa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom