Sitta umetwishwa zigo,onyo kwa viongozi wengine ccm kueni macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta umetwishwa zigo,onyo kwa viongozi wengine ccm kueni macho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Japhari Shabani (RIP), Apr 11, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tumekua tukishuhudia maamuzi,kauli na vitendo vingine vingi vya ajabu na aibu kutoka kwa viongozi wa CCM na serikali.Ni kweli kuna wanaotoa kauli,kuunga mkono au kushiriki katika maamuzi bila kujua au kwa upeo mdogo wa kuelewa,mazoae na ushabiki ,hawa tunaweza kuwasamee.Kuna kundi lingine la viongozi katika CCM ambao tunaweza kuwahita wanaupeo na uwezo wa kushauri au kupambanua lipi sawa na lipi sio sawa.Viongozi hawa wanapokaa kimya na kunyamazia yale yote mabaya yanayotendeka katika CCM na serikali ni wa SALITI Kwani wanashiriki katika maamuzi ambayo ni hatari na mzigo kwa taifa.Hawa tunawezakusema wako huko kwa ajiri ya matumbo yao na si kwa manufaa ya Taifa Kilichotokea kwa Mh.Sitta huko Visiwani liwe funzo kwa viongozi wa CCM ambao tunazani bado wanachembe ya uchungu wa Taifa.Niwazi Mh.Sitta alielewa zigo analolibeba(mswaada wa katiba)Kama mwanasheria,linamapungufu makubwa na umeandaliwa kwa makosa lakini akaamua kulibeba.Huku ni kujidhalilisha hivyo onyo kwa viongozi makini kama mpo mliobaki CCM msikubali kubeba madudu ya ajabu.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. N

  Nyota Njema Senior Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfumo wa vyama vingi ulikuja ili kutoa nafasi pana kwa kila mwanasiasa kuchagua jahazi la kusafiri nalo, kinachoshangaza ni huyu Sitta kuendelea kung'ang'ania jahazi bovu kwa sababu ya mkate wa kila siku.Watanzania aina ya Sitta ni hatari kwa ustawi wa jamii yetu, wanaelewa ukweli lakini wanabaki na utumwa wa kunyenyekea watawala kwa lengo la kuendelea kunufaika na makombo yanayodondoka kutoka mezani kwa mkubwa, hii ni aibu sana.Kama atashindwa kusoma hizi alama za nyakati, natumaini anasubiri magumu zaidi kutoka kwa huyu nyoka aliyejivua gamba!
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Magamba yanawana CCM hayavuliki
   
 4. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wazi kabisa mkuu. Nilisikitika saana kuona mtu kama 6 anafanya jambo kama hilo ambalo nathubutu kusema ni la "KIUMAMUMA". Hii licha ya kudhalirisha taaluma ya sheria ambayo Mh. 6 anayo, pia inatia shaka juu ya nia halisi aliyo nayo yeye 6. TUNAMATATIZO MAKUBWA!!!
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Kile alichofanyiwa Unguja kuchaniwa mswada na kuambiwa aondoke kwani hakuna cha kujadili kwa kweli kimemweka pabaya lakini ndio hivyo tena atafanyaje maana inahitajika uamuzi ugumu kuchkua !
   
 6. m

  majege Senior Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mh Sita alijua fika nini kinaweza kutokea, na yeye akavaa uhusika wa kuwa messenja tu. kwani inafahamika kuwa Sita ni mmoja wa wapinzani wachache wanaopambana ndani ya CCM. hata kwa haya madudu yaliyotokea Zanzibar na huku Bara. Naamini sita kimoyomoyo anasema (msg send and delivered). kwani hawezi kuwa anapiga kelele kwa kila jambo wakati mwingine unaachia Nature ifanye kazi na ndicho kilichotokea.
   
 7. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wazanzibar wengi nafikiri hajatulia na kufikiri, yaani mnataka kupoteza urai wa nchi kubwa? unajua ukifa muungano heshima yenu itakuwa haina tofauti na raia wa Commoro?
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mimi si mzanzibar lakini mkuu hili ni tusi nchi ni nchi tuuu ukubwa jina mkuuu! Hadhi kwenye medani za kimataifa ipo palepale!
   
Loading...