Sitta-tuibane serikali isisamehe mambo ya hovyohovyo! Mambo yakiwa magumu CCM si mama wa baba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta-tuibane serikali isisamehe mambo ya hovyohovyo! Mambo yakiwa magumu CCM si mama wa baba yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by luckman, Oct 11, 2011.

 1. l

  luckman JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Wanajamvi, huyu mtu kwa jicho la tatu namuona anachosema ana uhakika nacho!kajitokeza na kwa hekima na busara, mwenye kujiamini amesema yuko tayari kwa lolote dowans isilipwe na kasisitioza ni genge la wahuni!KASISITIZA, KUPANUA GOLI ILI MPIRA UPITE HUO SIO MCHEZO BALI NI FOUL!KASISITIZA DOWANS HAINA UHALALI WOWOTE WA KULIPWA,KAENDA MBALI NA KUSEMA NI LAZIMA TUSHIRIKIANE KUUBANA UONGOZI USISAMEHE MAMBO YA HOVYO HOVYO!
   
 2. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kwangu mimi Viongozi kama Sitta naanza kuwaona kama wasanii fulani..Badala ya kufunguka na Data kila siku unakuwa unasema tu ''Dowans ni genge la wahuni''....kivipi??
  Ni kama vile unalalamika nyumba inavuja wakati wa masika ikifika kiangazi hueiezeki wala nini??..Huyu Sitta analalamika, serikali inalalamika, CCM inalalamilka...hivi atakayechukua maamuzi ni nani??...Kama wanaona hawawezi kuchukuliana Hatua ..basi wairudishe Serikali kwa Wananchi ili wenyewe tujue tunampa nani dhamana ya kutuongoza...Shame on you guyz!!!
   
 3. peri

  peri JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tusubiri tuone. Mwisho wa siku ukweli utajulikana tu.
   
 4. l

  luckman JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  No, brother, huyu mtu ni waziri, yupo serikalini, kelele anazopiga zinashutua wengi, walianza kwa kubeza lakini leo kaendelea na msimamo wake?na ujue ukiwa nje utadhani mambo marahisi no sio hivo!wangapi umewaona wanafunguka kama yeye!?alafu kusema hivo lazima sisi tuelewe!sio lazima ataje make anasema washamshauri uongozi juu ya hili na bado kamalizia mambo yakiwa magum ataamua mambo mengine!tusichulie mambo marahisi kaka!sita ashakuwa speaker moja ya mihimili mikuu mitatu ya nchi so ni mtu sensitive sana!namkubali na amethubutu na walio wengi wameelewa!wanaompinga watokeze na watanzania wawaulize maswali yao uone nani msaliti!sitta alifanya kazi yake, ngazi nyingine zilitakiwa kuyakamilisha, wakawapiga mkwara na kuzima sasa mlitegemea fanye nini wakati hayupo kwenye uamuzi na chi yetu na mfumo wake mnauelewa?????????????????he is a good man and wise!
   
 5. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ngoja tuone hizo nguvu zake maana urais 2015 unakodolewa macho sana
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Mkuu SnowBall.

  Nadhani mwenye matatizo ni wewe unaangalia kauli ya kupinga malipo ya Dowans kasema nani ?.Mpaka leo bado unasubiri data za Dowans kweli waTanzania wana matatizo nilidhani ungekuwa wa kwanza kuunga mkono kauli ya Sitta badala ya kuibeza.Juzi tulisikia kauli ya waziri wa fedha mhe M Mkullo akikataa kulipa Dowans sitashangaa akibezwa.Mkuu Sitta na Mkullo wakiungana na Mawaziri wengine kupinga malipo ya Dowans na kuzipeleka maeneo mengine kwaajili ya maendeleo ya taifa bado tutawabeza ?.   
 7. l

  luckman JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Nadhani ni mitazamo tu ndo inayotugawa laiti tungejua umuhimu na thamani ya utu wetu kamwe tusingembeza mheshimiwa sitta!ametufungua mawazo walio wengi!nashangaa hii nchi hata muundo wake waserikali! Hadi anayetakiwa kulipa hajulikani!serikali inakataa na tanesco inakataa sasa jamani hii nchi au?????bado hamjajua kuwa huu ni usanii wa genge la wahuni?????mnabeza tu!!!!!!!ok one day!ninachosema, kuna mambo mengi hawa waheshiwa pamoja na mpiganaji aliyepelekwa india, wanajua mambo mengi na kama wangeyasema bungeni sidhani kama pangekalika!lakini inafika muda lazima busara zitawale!!!!!!!!!!!!!!na hiyo ndo sifa ya kiongozi mwenye iq nzuri !
   
 8. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mkuu hapo umenena. Kwani aliyezuia kuendelea mjadala kuhusu dowans bungeni ni nani? Mfadhili mkuu wa CCJ ni nani? Tumesahau anavyovizodoa vyama vya upinzani bungeni hata kwa jambo lenye maslahi ya taifa? Muda wote huo anasubiri nini kujiuzulu kama anaona hapati suport kwenye baraza la mawaziri kuhusiana na sakata la Dowans? Si lazima ajiunge na upinzani, lakini kitendo cha kujiuzulu tu kinatosha kuonyesha umma kuwa kwa kweli yeye si mwezao. Kama si usanii ni nini basi?

  Binafsi mimi sitofautishi kauli hii na turufu ya urais 2015. Kwanini asiwe muwazi tu, tumwelewe mbona kuna watu wengi tu watamuunga mkono?
   
 9. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Asante Mzee Sita, kama vita ya ndani kwa ndani haina dalili ya ushindi ni afadhali kugeuza mbinu na uingie kwenye gorrilla war.
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Mkinipa nchi kwa mwezi mmoja, mtu wa kwanza kumpeleka mahakani atueleze kwanini ametumia madaraka yake vibaya hata kuwaingiza watanzania kwenye matatizo makubwa ni huyu mzee anayezeeka vibaya, ni huyu SITA. Tazama, yeye ndiye aliyeipokea richmond wakati huo akiwa boss wa TIC, so alijua ni kampuni ya wahuni watatu lakini akaishauri serikali iipokee kampuni hii na sasa anasema ni wahuni, atuleze ni wapi wanafanyia uhuni wao na huu uhuni kwa nini hakuuona wakati ule?,. Pili: wakati akiwa spika, aliendesha mjadala wa hovyohovyo juu ya richmond matokeo yake ili taarifa ya kamati ni NON-BITING kwa sababu pamoja na kutumia fedha nyingi taarifa haikuleta tija kwa wananchi. Tazama pia aliendesha mjadala wa kihuni juu ya kufuta mkataba wa DOWANS siku 60 kabla ya mkataba kufa natural death- hii inaigharim serikali Bild on taxpayers money. Kama ana ugonvi na JK au EL juu ya kukosa u-PM isiwe sababu ya yeye kuhamishia maumivu kwa walipa kodi, ni juavyo mimi he remains a looser hata mwisho wa dahari.
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  How good, how wise?, yeye hukaa kwenye kikao kikuu kinachofanya maamuzi kila wiki - cabinet, mbona asikatae au kumshauri boss wake right there badala yake ana back-bit?, huyu yafaa afungwe jiwe la kusagia shingoni mwake kisha atumbukizwe katika bahari ya kina kirefu- yeye ndo chanzo cha matatizo na ni imani yangu kuwa anapaswa kulipia gharama ya mateso wanayopata walipa kodi kwa sababu ya unafiki wake.
   
 12. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Mkuu, unajua gharama ya kukataa kutimiliza hukumu/mkataba kutoka chombo cha sheria cha kimataifa?, it too expensive kwa responsible party than you can imagine: moja ya madhara ni muhusika(nchi/kampuni) kutopewa direct contracts whith foreign cos yaani ukutaka kununua kitu lazima utumie third part na pia mdai anaweza kukamata mali yoyote ya mdaiwa iliyopo mahali popote. Kwasasa yeyeote anayesema DWNs isilipwe hajui anachosema.
   
 13. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Naenda Bagamoyo kuangalia shamba langu la mananasi hiyo Dowans mtajiju(?) he kweli ama kweli shamba la bibi sasa linazidi kwisha sasa sijui watahamia shamba la nani
   
 14. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,948
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Je lile la kusema Dowans limeingia mlango wa nyuma kupata huo mkataba ambao Idrisa (sio serikali)aliufuta je halina mshiko ,itabidi tumutafute wakili nguli Fungamtama atueleze bana
   
 15. l

  luckman JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hayo yote yanawezekana iwapo mkataba utakuwa halali, zipo sababu nyingi sana zinazoharamisha mkata huu fake wa genge la wahuni!huwezi kusema hatulipi hali huna vigezo utakuwa punguani sisi tunaosema hatulipi tuna sababu za kuseam hivo! Hila nyingi zimefanyika kuanzia usajili wa kampuni, umiliki wake, price standards, hali ya mitambo yenyewe na mambo kadha wa kadha!nchi haiwezi kuangalia pesa zetu walipa kodi zinaenda kwenye mikono ya walanguzi kama serikali husika haiwezi kuchukua hatua basi walipe!!!!!!!!
   
 16. l

  luckman JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Gama-wewe nadhani una mambo yako na hii saga hata huijui ndo maana hata unachoongea nadhani hukijui vizuri bwana gama! Sita kaja lini tic na kaondoka lini???hii kampuni imekuja na kusajiliwa lini???msiwe mnapenda kufurahisha uma kwa post zenu za kinafiki, wameshauri wangapi hii serikali,wamekataa mangapi lakini umeona hii serikali ina masikio???nakuuliza umeona hii nchi inawasikiliza wataalam wetu si ndo maana nchi iko hapa leo?????unachotaka kutetea ni nini bwana! Uliza basi tukwambie!mzee sitta anachosema anakimaanisha!hawa ni wahuni na hawasitaili hata cent moja!ka unabisha basi walipe waone!itakuwa turning point ya mabadiliko tunayoyatafuta!WHERE COMPANY LEGITMACY?JE INA NGUVU YA KISHERIA??IT DOESNT MATTER SHILINGI NGAPI KINACHOONGALIWA NA UHALALI WA MKATABA!HIYO NI SHERIA NA SHERIA SI PRINCIPLE KUSEMA HAIBADILIKI!KINACHOANGALIWA NA UHALALI WAKE!
   
 17. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ibaki kueleweka kwamba siasa uchwara na makundi ndani ya CCM ndiyo yaliyopelekea hili la DOWANS kufika hapa lilipo. Kama Taifa tunapaswa kulipa hiyo pesa lakini lazima wote waliohusika na kadhia hii wawajibike. List yangu ya watu wa kuwajibika ni kama ifuatavyo;
  1. Wale wote waliohusika na uamuzi wa kupokonya kazi ya procurement kufanywa na TANESCO na kufanywa na Wizara
  2. Kamati ya Dk.Mwakyembe yote kwa kutotoa ushauri mzuri wa kitaalamu/kisheria kuhusu namna nzuri ya kuuvunja mkataba ule
  3. REX attorneys (sijui hawa tunawafanyaje maana ni kampuni binafsi) kwa kuishauri serikali kuhusu kuvunja mkataba wa TANESCO na DOWANS bila kuangalia madhara yake kama vipengele vyote vya sheria visingeangaliwa vizuri.
  4. Spika Samwel Sitta kwa kushabikia na kutuaminisha kwamba kuvunjwa kwa ule mkataba kusingekuwa na tatizo lolote
  Kwenye hili nadhani hao hapo kwenye list hawapaswi kukwepa lawama kwa kadhia hii.Sitaki kuwabebesha mzigo waanzilishi wa hii sinema.
   
 18. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu Sitta nilikuwa namwelewa sana siku za nyuma lakini siku hizi hata simwelewi kabisa, you know he's part of serikali anayotuambia tuibane sasa kama anasema tuibane serikali basi tuanze na yeye.. AINERUGABA Msemakweli (Sijui kama nimepatia jina la kwanza) alitoa tuhuma na akataja watu na sasa kesi iko mahakamani kashitakiwa, Sitta anabaki kusemea kwenye vyombo vya habari tu na bila kutaja hao anaosema ni genge la wahuni. Huyu mzee ni kati ya watu waliolifikisha taifa hapa. Laiti kama ripoti ya kamati teule ya bunge chini ya mwakyembe ingekuja na ripoti yote bila kuiedit JK kwa sasa asingekuepo madarakani. Sasa imebaki kusukuma siku tu kila siku richmond tukitulia kidogo baada ya miezi 3 rich tena anakuja, tumechoka.
  Hao genge la wahuni wawaseme mana wanawajua na ili dowans wasilipwe basi kina sitta hawana budi kusema siri waliyonayo vinginevyo richmond akilipwa wao wataonekana ndio genge la wahuni. Wananchi wanajua ushiriki wa EL, JK, RA ktk hili, sasa 6 anaogopa nn kuataja?
   
 19. l

  luckman JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Nani tumwelewe sasa!waliofanya utafiti na kubaini maovu kibao na kuleta ushahidi mezani na kutoa nafasi kwa kila mtu aliyesingiziwa afate vyombo vya sheria na dk pamoja na kamati yake wakasema watajiuzulu iwapo watagundulika wamedanganya umma au wale ambao wanaongelea kwapani na kutumia pesa nyingi kuhalalisha haramu???tumepewa akili ya kutambua na kupambanua mambo bwana lazima mjue!hila nyingi zimefanywa kuficha ukweli brela!haya yote kama kampuni ni halali kwanini sasa haya yafanyike???ninachosema ni hivi>?mahakama kusema hii pesa ilipwe sio msumari wa mwisho bado nafasi ipo ya kudhihirishia uma kuwa hukumu hiyo haina mashiko!!!!!!!ndo maana hata wanasheria waandamizi wamejitolea kuhakikisha haya malipo hayafanyiki kwani ni uhuni wa genge la majambazi ya nchi!!!!!!!!!!!!!!
   
 20. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Hao mawakili wanaotetea DOWANS kwa nini wasiwe wazalendo wakajitoa kwenye hili shauri kwa faida ya Taifa letu? au hii ni vita ya tabaka la juu kupora tabaka la chini?
   
Loading...