Sitta: Tuache kuwaza Urais kila siku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Tuache kuwaza Urais kila siku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bitabo, Dec 23, 2011.

 1. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema anachukizwa na tabia ya baadhi ya watu kukaa na kufikiria urais kila siku huku wakiacha kuutumikia umma.Kauli ya Sitta ambaye alitangaza kwamba kwa sasa hana nia ya kuwania urais 2015, inakuja kipindi ambacho baadhi ya wanasiasa hasa ndani ya CCM wamekuwa wakipigana vikumbo kwa ajili ya mbio za kumrithi Rais Jakaya Kikwete.

  Juzi akiwa ziarani jimboni kwake Urambo Mashariki, Sitta alisema urais ni jambo linalokuja lenyewe kwa watu waadilifu hivyo hakuna haja kwa watu kila siku kufanya harakati za urais.

  "Urais unakuja wenyewe kwa watu walio waadilifu. Nachukizwa na watu ambao wao kila siku wamekuwa na mawazo ya urais na kuacha mambo ya msingi ya kutumikia wananchi wa Tanzania," alifafanua Sitta.

  Sitta ambaye pia alikuwa Spika wa Bunge la Tisa, alisema yeye binafsi anachukizwa pia na kuhusishwa katika harakati za urais wa 2015 na kusema hadi sasa, bado ni mapema na kutaka wanasiasa kutumikia wananchi.

  Aliongeza kwamba wapo ambao hata wanajaribu kutengeneza uongo kwamba, amekuwa akienda makinasani na misikitini kwa ajili ya kutaka urais lakini akasema;"Hawa ni wale wale mafisadi wanaoeneza ajenda zao za hovyo kila siku."

  Sitta alifafanua kwamba suala la yeye kusaidia shughuli au kujumuika katika Kanisa au Msikiti ni jambo la kawaida na hakuanza kulifanya leo wala jana bali ni muda mrefu.

  Alisema wapo watu wanaojaribu kujenga taswira kwa umma kwamba, kujumuika kwake katika baadhi ya shughuli za makanisa au misikiti ni sehemu ya mbinu za kusaka urais kitu alichosema ni upotoshaji kwa kuwa hakuanza leo kujumuika na wana dini.

  Waziri huyo mwenye dhamana ya Uhusiano wa Afrika Mashariki, alisema ni vyema wanasiasa wakajikita katika mambo ya msingi ya kusaidia wananchi, kusimamia maadili na kuonyesha uadilifu kuliko kuwaza urais kila kukicha.

  Alienda mbali akisema, kama ni urais ameshiriki kusaidia baadhi ya wagombea na baadhi walifanikiwa kushika wadhifa huo hivyo haoni sababu za watu kumhusisha na mbio za urais 2015 pale anapotumikia umma.

  "Nimeshashiriki sana kusaidia wagombea urais, baadhi yao walifanikiwa. Hivyo, sina tamaa na urais ninayofanya ni kutumikia umma na taifa langu. Lakini, wapo wanaopitapita na kutaka kuonyesha wananchi kwamba ninavyotumikia umma na msimamo wangu kutetea maslahi ya taifa, kama ni kampeni za urais, lakini hawa ni wale wale maadui wa kila siku," alifafanua Sitta.

  Alisema suala la urais siyo la kukimbilia wala kulitafuta kwa nguvu na mbinu chafu, kwani siku zote watu waadilifu wanafahamika na hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi kuutafuta madaraka hayo ya juu ya nchi.

  "Haya mambo ya urais kila siku hayana maana. Kibaya zaidi watu wanahamisha mambo ya msingi na kuyapeleka katika fikra za ovyo. Hebu ufike wakati tuangalie matatizo ya wananchi kwanza tusifikirie vitu ambavyo havimsaidii mwananchi wala taifa," alisistiza.

  Hivi karibuni Sitta amekuwa alitajwa kama mmoja wa watu wanaoutaka urais 2015, lakini mwenyewe hivi karibuni alipozungumza na kituo kimoja cha luninga nchini alisema, "kwa sasa sijafikiria urais."

  source: Mwananchi ya leo
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  waadilifu wapi mbona huuu mtutu unatupelekapeleka tuuu kama mazuzu hatuludii kosa bana!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  anautaka huyu ndio maana anaongea ongea kila kukicha
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kwa nini yeye anaenda kwa wananchi kuwaeleza habari za urais badara ya kuzungumzia kero zinazowasumbua.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Anawapiga mkwara wenzake wasiwaze, wanamwacha yeye akichanja mbuga. siasa bana!
   
 6. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,655
  Likes Received: 3,307
  Trophy Points: 280
  Basi tumeacha mkuu
   
 7. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Uku ndio kuzeeka vibaya!hapo ukimwambia anazeeka vibaya atasema unamtusi..
   
 8. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Ure right mr six... Bt what are u doing up there?
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Aupeleke chooni huo unafiki wake!
   
 10. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Silence is a weapon as any other weapon......we can read between lines you mr sitta xo no need of barking if u dont wanna be a president! We know now how to separate wheat from the chaff! Damn it!
   
 11. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnafiki wetu sitta ndani urambo kwenye jumba lake lilojengwa kwa kodi zetu!!zee linazeeka na unafiki wake.
   
 12. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hahahahaha! Wenzake wakienda Makanisani wanautaka urais, yeye akienda anaenda kwa wananchi, Sitta bana!
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Big up made Sitta. Tumechoka na electioneering ya kila siku. Tuchape kazi
   
 14. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ni kweli anautaka tatizo hajawa muwazi !
   
Loading...