Sitta:Tabaka linamhujumu JK

one activist

Senior Member
Oct 13, 2012
114
14
Dar es Salaam. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kuwa kuna tabaka la wenye fedha lililojengeka, ambalo linahujumu utendaji wa Rais Jakaya Kikwete ili aonekane hajafanya lolote katika kipindi alichokaa madarakani.

Aidha, Sitta amesema kuwa wako pia wasomi na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wameungana na viongozi wa Serikali katika mbio hizo za kumsaliti Kikwete. Waziri Sitta aliyasema hayo jana katika Mahafali ya Tatu Chuo cha Ualimu Kibamba (KTC) kilichopo wilayani Kinondoni, nje ya kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

"Hali kama hii haiwezi kukubalika kwani watu hawa ni hatari, tena baadhi yao wanadiriki hata kuhamisha fedha za umma kupeleka kwenye benki za nje ili wasigundulike," alisema Sitta na kuongeza: "Kuiachia hali iendelee ni sawa na kubeba maji kwenye kikapu.

Hivyo basi mimi kama ‘Mzee wa Viwango nina mifano mingi ya kuwataja watu hawa lakini kwa sababu ya muda sitoweza kuwataja tena wengine ni wasomi wakubwa hapa nchini wapo kwenye mkumbo huo."

Alifafanua: "Watu kama hawa kwa nchi kama ya China wananyongwa, lakini ukija hapa kwetu utasikia haki za binadamu huku watuhumiwa wakiendelea kupata usingizi mnono; kwa hali kama hii hatutaendelea. Jamani tuige mfano wa China, hivi hizi haki za binadamu ni kwa viongozi tu?"

Alisema kuwa hali hiyo inatokana na watu hao kusahau maadili aliyoyaacha Mwalimu Nyerere na kwamba wizi na ufisadi umezoeleka na kuwa sehemu ya maisha akihimiza wanannchi waungane kuitokomeza hali hiyo.

My observation:
Ni huyuhuyu Sitta alietamka siku chache zilizopita kuwa amechangiwa pesa na akina Magufuli kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya kanisa moja pale Mwanza, baadae Magufuli amekanusha vikali taarifa hiyo, huyu mzee kama si umri umemuelemea basi ni tapeli wa kisiasa, leo amekuja na hilo hapo juu, kama kweli ana dhamira ya dhati kwa nini asiwataje watu hao? Na kama kati ya wanaomhujumu JK wapo ndani ya serikali yake, mbona yeye ameendelea kuwaamini na kufanyanao kazi?..Mbona husemi JK alivyokuhujumu wewe kwa kutokukupa uwaziri mkuu kama alivyokuahidi na akampa Lowassa?

Yaani ndani ya CCM watu wanapishana koridoni kumlamba miguu mwenyekiti mradi tu kutafuta ushawishi wake, si watu wazima kama akina mzee Sitta, wala si wadogo kama akina Nape, hii ni aibu kwa chama kama CCM kukosa demokrasia namna hii, kuna watu wanatofautiana kiitikadi na JK ndani ya mioyo yao lakini kwa nje wanajionyesha ni watu wanaompenda kwelikweli na kukubaliana nae kwa kila jambo, hakuna mjinga anaeweza kukubaliana na wanasiasa kama hawa wanaotafuta madaraka kwa njia za kinafiki kama akina Sitta, Lowassa nk, wakichukua nchi hawa hawatoweza kufanya mikakati na maamuzi magumu yatakayofanya tulipe deni la taifa.
 
Ni maono yake nadhani kwenye vikao vyao vya chama atawataja wahusika.
 
Ni maono yake nadhani kwenye vikao vyao vya chama atawataja wahusika.
Kinachoudhi hapo ni kwamba hakuna sehemu atakapowataja hao watu, kama angekuwa na tabia hiyo ya kuwataja hata huko vikaoni ingekuwa afadhali, zaidi ni porojo tu za kutafuta umaarufu wa kisiasa.
 
Mpendazoe si alisema ofs za CCJ na furniture alilpa sita badaye walposhtukiwa akawatoroka wenza altoa wap pesa..uzee unampelekesha huyu na stres
 
Sasa akina Mwigulu, Nape, Juliana Shonza na Mwampamba Mtela badala ya kuanza kuwashambulia wanaohujumiana wao kwa wao ndani ya chama chao cha zamani wao kazi yao kutwa kulala kuamka wasipomtaja Dr Slaa siku haijaisha...absolutely ridiculous!! Wenye chama watagawana kila mtu kipande chake wawaache wakibwatukabwatuka hovyo ooohooooo!
 
Samwel Sitta akiwa Kanda ya Ziwa wiki kama mbili zilizopita alisema alimuunga mkono Jakaya 2005 bila ya kujua kuwa ni kiongozi mbovu tena akafanabisha na mchumba laiebadilika mara baada ya kuchumbiwa akamtuhumu kuwa ndio aliempokonya "Uspika wake" leo, leo anageuka eti Jakaya ana hujumiwa baada ya kuona Jakaya hana Time nae, Jakaya hana cha kupoteza iwe Serikali 2,3 au hata Mia moja, Wapo waloshadadia Eti Rais apunguziwe madaraka wakidhani yatapunguzwa madaraka ya Jakaya kunbe any changes kwenye katiba mpya haina cha kufanya na Urais wa kikwete, Sitta anaweweseka akina Mzee Mengi wamejiunga kambi ya ushindi ya Mzee Ngoyai. mnaopoteza nguvu kumchambulia ni sawa na kuukimbiza upepo, Waige style ya Rais mtarajiwa wa Tanganyika Mzee Ngoyai hana muda wa kushambulia watu yeye anashambulia Hoja!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom