Mkusa
JF-Expert Member
- Dec 14, 2010
- 549
- 209
Who the Hell is this yknown as Dr Banna, Hivi huyu ni msemaji wa Magamba???????
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Dk Benson Bana aliliambia gazeti hili jana kuwa CCM imedhihirisha ni chama dume, chenye demokrasia na ukomavu kisiasa.
La Lowassa Chenge limewashindaAkifafanua, alisema: "Uchaguzi unadhihirisha wazi kuwa CCM bado inadunda na dhana ya kujivua gamba inatekelezwa, watu zaidi ya 5,000 walipitishwa Dodoma huku sura mpya zikijitokeza, miongoni mwao ni vijana, wazee hata wakulima".
Ngoja nisiseme,naweza pewa BannDk Bana alisema hatua hiyo imedhihirisha mianya ya rushwa kudhibitiwa ndani ya chama hicho, baada ya kuona magwiji wa siasa akiwamo Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, wakiangushwa, jambo linaloashiria hakubaliki kuwania urais.
Amekataliwa na CCM na sio Wa Tanzania, hivi huyu Mzee ni Poyoyo???"Hakuna asiyejua mbio za Sumaye kutaka urais, sasa kama jimbo la Hanang watu wachache wamekukataa, si rahisi Watanzania wakupe urais, namshauri sasa arejee kutumika katika nafasi yake ya siasa kama Waziri Mkuu mstaafu, maana Watanzania wameamua kufanya mabadiliko," alisisitiza Dk Bana.
Holy Cra.p, Lowassa labda akawe Rais wa Monduli
"Uchaguzi 2015 tutarajie mambo makuu mawili; Katiba mpya ndio pekee itatoa mwelekeo wa kitakachotokea, lakini pia CCM inateua nani kuwania urais wakati huo, hii itabadili mtizamo wa siasa, wakiteua vizuri, watawafunika wapinzani," alisisitiza Dk Bana.
Dk Bana alivunja ukimya na kueleza wazi kuwa, hivi sasa ndani ya CCM kuna mtu anayenukia urais, ila bado ana madoa anayopaswa kuyasafisha ili akubalike. Alimtaja mtu huyo kuwa ni Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.
Namslikitikia kwa Sababu CCM ni sikio lililo Kufa afadhali hata lingekuwa ni la Kufa."Hawa wana kambi zao ndani ya chama, wanataka kumvuruga Katibu Mkuu Mukama (Wilson) kwa kauli zao, wasipewe nafasi waadabishwe kurejesha nidhamu," alihimiza Dk Bana aliyekuwa akitoa maoni yake kuhusu uchaguzi unaoendelea CCM.