Sitta: Sisubiri ruhusa ya mtu yeyote, nani asiyejua kuwa Chenge ni mtuhumiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta: Sisubiri ruhusa ya mtu yeyote, nani asiyejua kuwa Chenge ni mtuhumiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Baba Mkwe, Oct 4, 2012.

 1. B

  Baba Mkwe Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeelezwa kuwa utabiri mwema kwa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kutokana na kuingiza sura mpya huku vigogo wakibwagwa.

  Aidha, baadhi ya waliong'ara katika uchaguzi huo wametabiriwa neema kushika nafasi za juu katika Serikali ukiwamo urais mwaka 2015 ikiwa watakuwa tayari kusafisha madoa waliyonayo.

  Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Dk Benson Bana aliliambia gazeti hili jana kuwa CCM imedhihirisha ni chama dume, chenye demokrasia na ukomavu kisiasa.

  Akifafanua, alisema: "Uchaguzi unadhihirisha wazi kuwa CCM bado inadunda na dhana ya kujivua gamba inatekelezwa, watu zaidi ya 5,000 walipitishwa Dodoma huku sura mpya zikijitokeza, miongoni mwao ni vijana, wazee hata wakulima".

  Dk Bana alisema hatua hiyo imedhihirisha mianya ya rushwa kudhibitiwa ndani ya chama hicho, baada ya kuona magwiji wa siasa akiwamo Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, wakiangushwa, jambo linaloashiria hakubaliki kuwania urais.

  "Hakuna asiyejua mbio za Sumaye kutaka urais, sasa kama jimbo la Hanang watu wachache wamekukataa, si rahisi Watanzania wakupe urais, namshauri sasa arejee kutumika katika nafasi yake ya siasa kama Waziri Mkuu mstaafu, maana Watanzania wameamua kufanya mabadiliko," alisisitiza Dk Bana.

  Kuhusu madai hayo, alipoulizwa Sumaye jana, alisema, "najua unataka habari ya uchaguzi, sasa hivi sisemi lolote ila nitakuja Dar es Salaam kati ya siku mbili au tatu hivi, utaniuliza na hilo swali lako nitakapozungumza nanyi waandishi wa habari."

  Akizungumzia harakati za urais mwaka 2015 kutokana na uchaguzi huo wa CCM, Dk Bana alisema CCM itang'ara katika uchaguzi ujao ikisimamia mweleko wa sasa, lakini hatima yake imesimama katika mambo mawili; Katiba mpya na uteuzi wa atakayepeperusha bendera kuwania urais.

  "Uchaguzi 2015 tutarajie mambo makuu mawili; Katiba mpya ndio pekee itatoa mwelekeo wa kitakachotokea, lakini pia CCM inateua nani kuwania urais wakati huo, hii itabadili mtizamo wa siasa, wakiteua vizuri, watawafunika wapinzani," alisisitiza Dk Bana.

  Dk Bana alivunja ukimya na kueleza wazi kuwa, hivi sasa ndani ya CCM kuna mtu anayenukia urais, ila bado ana madoa anayopaswa kuyasafisha ili akubalike. Alimtaja mtu huyo kuwa ni Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

  Hata hivyo, Dk Bana aliitaka CCM iwaadabishe baadhi ya wanachama, baadhi ni viongozi wa nchi akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta na Peter Kisumo (Mdhamini wa CCM) kwa alichodai, wanazungumza bila kufuata utaratibu.

  "Hawa wana kambi zao ndani ya chama, wanataka kumvuruga Katibu Mkuu Mukama (Wilson) kwa kauli zao, wasipewe nafasi waadabishwe kurejesha nidhamu," alihimiza Dk Bana aliyekuwa akitoa maoni yake kuhusu uchaguzi unaoendelea CCM.

  Akijibu tuhuma hizo jana, Sitta alisema: "Nimezoea, kauli zangu hazijawahi kuwafurahisha hata siku moja mafisadi, nataka wajue hivi; nitazungumza mpaka tone la mwisho la pumzi yangu, nimefundishwa kukemea maovu na Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere)".

  Sitta alijigamba kuwa, alijiunga na TANU Oktoba 3, 1960 akiwa kidato cha tatu na sasa ni miaka 52 ndani ya chama, hajavunja utaratibu wowote katika kukemea maovu na wanaotaka anyamaze, anawakera kwa kuwa amewagusa.

  "Sitachoka kusema mafisadi, maana wanaharibu nchi yetu, hata Ilani ya chama inanilinda nikemee maovu, sisubiri ruhusa ya mtu yeyote, nani asiyejua kuwa Chenge (Andrew-Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM) ni mtuhumiwa, haiingii akilini eti amepita bila kupingwa Bariadi, watu 11 waliochukua fomu wamefutikia wapi?" Alihoji Sitta.

  Sitta, Spika mstaafu alipotakiwa kufafanua hoja hiyo, alisisitiza kuwa inajulikana wazi ndani ya chama na wachache wenye ujasiri kama yeye, ndio wana uwezo wa kusema na kusisitiza kwamba hatanyamaza mpaka pumzi yake ya mwisho.

  Hata hivyo, alikiri kuwa uchaguzi wa CCM umekwenda vizuri ila hivi sasa yapo baadhi ya maeneo bado rushwa inatumika kupindisha matokeo na kusisitiza kwamba ikiwa rushwa itakemewa ndani ya chama na viongozi halali wakapatikana, hata dawa hospitalini zitapatikana na ndilo tamanio la wapenda maendeleo.


  Waandishi: Almasi, Thobias Kadome na Mercia Emmanuel.
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,469
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mwenyekiti wake( Sitta) ameshasema njia ni nyeupe kwa wasioridhika na mambo yanavyokwenda ndani ya CCM kuondoka. Bahati mbaya tu Sitta wetu hana pa kwenda.
   
 3. Root

  Root JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 22,361
  Likes Received: 7,862
  Trophy Points: 280
  Chama dume heeee
  Sitta kaongea la maana sana kuhusu chenge

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Dr. BaNA aendelee hivyo hadi CCM ife kabisa. Awasifie tu.
   
 5. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 6,905
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  Rangi ya Bana sasa inaonekana vizuri
   
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,163
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  sitta asijikoshe.si alijishaua kubadilika msimamo,wembe ulele,magamba ondoa wanafiki wanaojidai wazalendo feki,mbaki mafisadi peke yenu wenye phd ya wizi wa mali za uma.sasa wale pande mbili nasie wazalendo hatuwataki huku,wanabaki wanaelea juujuu,wakianguka wataangukia pua.
   
 7. peri

  peri JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  sita nae ni mnafik tu,
  alisha yasema hayo kwenye vikao vya chama?
  Kama hawayafanyii kazi mbona haondoki, anasubiri nini?
   
 8. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,290
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  Haya Dr. Bana! Lakini 2015 si mbali. Tutaona hayo madoa-doa yatakavyo safishika. Utashi wa wanaMonduli si utashi wa Watanzania!
   
 9. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,166
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  well said sitta kuhusu Chenge lakini kama wewe kweli si mnafiki mbona hujawataja ridhiwani na salma ambao nao wamepita bila kupingwa?
  Utasema Chenge ni fisadi ok! Mbona ridhiwani ni fisadi na ni mtoto mdogo kichama mpaka apite bila kupingwa? Wewe sitta una tatizo moja kubwa wewe ni "mnafiki" usiyejua kujipanga.
   
 10. M

  MR.PRESIDENT Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Simwamini Sita hata kidogo.Ni kama kinyonga
   
 11. M

  MTK JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,798
  Likes Received: 2,706
  Trophy Points: 280
  Benson Bana yuko kundi gani? kwani anaonyesha wazi hapa kwamba hata yeye ni gamba linalonufaika na matunda ya ufisadi kutoka kundi fulani; most likely la EL!!
   
 12. O

  Original JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sitta ni mnafiki na ni hatari kupita kiasi. Huwezi kukemea ufisadi ukiwa ndani ya mafisadi. Achana nao ili umma wa watanzania ukuelewe.
   
 13. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,044
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Hivi Sitta anaingia mkutano mkuu wa NEC??
   
 14. ma2mbo

  ma2mbo JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Uyu sijui Bana ana phd ya nini??
  Kweli wasomi wa bongo ni watumwa wa wanasiasa.
   
 15. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Benson Bana naye ni mchumia tumbo hana lolote na kama na wewe ni mhadhiri wa chuo kikuu naomba acha kuuaminisha umma watanzania kuwa ccm itashinda na EL ndie rais 2015 naona hauna huruma na watanzania hata pengine elimu yako haikusaidii na haisaidii kuelimisha watanzania
   
 16. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,523
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Bana akale wapi wakati anajua fika kuwa akiipinga CCM wazi kitumbua chake kitatiwa mchanga!

  Huu ndio unafiki wa watanzania wengi ambao hawawezi kusimamia kile wanachoamini ni cha kweli.
   
 17. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  elimu ya benson ninayomashaka sana naomba manao mfahamu mtupe detail zake maana nao kama hakupita kwa desa basi itakuwa kwa fatomu au kwa simbi maana PhD haiwezi ongea ujinga kiasi kama hiki ndio wasomi wetu tunaowategemea waliondoe taifa hapo lilipo na kwenda kwenye maisha bora kwa kila mtanzania lakini kwa style hii tutaendelea kuwa watumwa wa wenye nacho mpa siku ya mwisho
   
 18. N

  Nyota Njema Senior Member

  #18
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sitta ni kama nyumba ya udongo inayomomonyoka pole pole kwa chini ambayo mwisho wake huwa ni kuanguka na kuteketea kabisa. Jamaa huyu amepewa ushauri mara nyingi na watu makini (Dr. Slaa na wengineo) lakini amekuwa sikio la kufa.
  Kitendo chake cha kung'ang'ania kubaki CCM ikiwa ni pamoja na kukubali huo uwaziri aliopewa ilikuwa ni kukubali maji yanayopita kwenye huo msingi wake wa matope. Tusubiri kuona anguko lake!
   
 19. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 25,252
  Likes Received: 7,069
  Trophy Points: 280
  Sasa Msekwa anasema dhana ya kujivua gamba imeisha huyu Bana anasema ipo na inatekelezwa. Sasa kuwa na statement zinazokinzana si uwendawazimu kweli
   
 20. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 9,831
  Likes Received: 3,104
  Trophy Points: 280
  nutty professor bana
   
Loading...