Sitta:Sijafanya upendeleo katika mijadala

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, amesema hajawahi kufanya upendeleo katika kuchagua wachangiaji wakati wa mijadala mizito.

Kauli ya Sitta imekuja siku chache baada ya baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumtuhumu kuwa amekuwa akiruhusu mijadala mizito inayoisumbua serikali ya chama hicho, katika vikao vya Bunge.

Kumekuwa na kelele kutoka kwa wanaCCM na viongozi wengi ambao wamekuwa wakidai kuwa Sitta amekuwa akiruhusu wachangiaji ambao wanaisumbua serikali katika mijadala mizito.

Jana kabla ya wachangiaji wa sakata la Richmond, Spika huyo alisema kazi ya kuwachagua wachangiaji inafanywa na makatibu wa vikao.

"Hapa naomba nieleweke kuwa mara nyingi nimekuwa nikiambiwa kuwa naruhusu au kuchagua wachangiaji, lakini si kweli kwani ukweli ni kwamba majina ya wachangiaji hata mimi ninaletewa kutoka kwa makatibu," alisema Sitta.

Mbunge huyo wa Urambo Mashariki, alionyesha wasiwasi huo baada ya orodha ya wachangiaji wa taarifa kuhusu sakata hilo, kuonekana kwamba ilikuwa imejaa wapiganaji ambao mara nyingi wamekuwa wakijipambanua na kama wapambanaji katika vita dhidi ya ufisadi.

Baadhi ya watu waliitafsiri hoja hiyo na kile walichokiita kuwa ni mtego mwingine kwa kiranja huyo wa Bunge kuwa huenda angehusishwa na kitendo cha upendeleo kwa wabunge.

"Hawa jamaa wamekuwa wakimuandama sana Sitta na ukizingatia kuwa leo ni siku ya Richmond ndio maana unaona ametanguliza kutoa onyo hilo mapema," alisema mmoja wa wabunge ambaye alikaata jina lake lisitajwe.

Mbunge huyo alitolewa mfano wa kusakamwa kwa Sitta na kile alichokiita kuwa alikuwa ametumiwa ujumbe wa kuonyesha kuwa wabaya wake, wapo baada ya moja ya magazeti ambayo yalikuwa yakigawiwa bure katika viwanja vya Bunge kusemekena kuwa lilikuja kwa ajili ya kumuonyesha kuwa hata wabaya wake wapo.

Jana katika viwanja vya Bunge kulikuwa na gazeti moja litolewalo kwa lugha ya Kiswahili lililokuwa likigawiwa bure kwa wabunge jambo lililoonyesha kumkera spika na hatimaye akaamua kuwatolea uvivu.
 
Back
Top Bottom